SIKU 30 ZA MIUJIZA NA MAAJABU. (SIKU ZA MFUNGO)[Day 18].

 

https://i2.wp.com/www.moonlightbasin.com/images/dynamic/getImage.gif

22/01/2016.

“HUKUMU NA ADHABU YALIYO KINYUME NA MAPENZI YA MUNGU KWAKO (JUDGE AND PUNISH ANYTHING AGAINST GOD’S WILL FOR YOU)”

Kwa miaka mingi Wakristo wamekuwa wapole sana.
Shetani amewapanda vichwani na hata kunya vichwani mwao huku wanamtazama.
Wamezoea kuonewa na kukanyagwa na kufinyiliwa na hali na matukio mengi ambayo si mapenzi ya Mungu!

Utasikia “Mali zangu zimeungua, Jina la Bwana libarikiwe” au ” Mtoto wangu kapata mimba nje ya ndoa, ila Mungu atukuzwe kwa hili” ama “Mme wangu amechukuliwa na kahaba mwaka wa nne sasa, Yesu atukuzwe hata kwa hilo” na mwingine anaweza kusema, “Huu UKIMWI naona Mungu ameuruhusu, naona Mungu ananipitisha kama Ayubu”
Hizi ni sentensi ambazo zimekaa KIDINI. Tumezoea kuwasikia WALIOOKOKA (walokole) wakizitumia na zimezoeleka.

Imefikia mahali inaonekana kama KUPATWA MATESO, MABAYA, KUFILISIKA, KUIBIWA, KUHARIBIKIWA, KUSHINDWA NI SEHEMU YA MAPENZI YA MUNGU KWETU!
Ibilisi amefanikiwa kiwafanya Waliookoka wakubali UONGO NA UONEVU WAKE kwa kigezo cha SHUKURUNI KWA KILA JAMBO MAANA HAYO NDIYO MAPENZI YA MUNGU KWENU KATIKA KRISTO YESU!

Sasa wewe, mmeo anachukuliwa na kahaba halafu unasema unashukuru kwa kila jambo!
Binti yako kazalia hapo sasa huyo ni mtoto wa tatu, ana miaka 25 tu na unasema Mungu ameyaruhusu niyapitie haya!
Ulikuwa na biashara kubwa unapata faida na unagusa maisha ya wengine ila sasa umeishiwa na unaomba omba na kukopakopa na unasema, NI MAPITO NA JARIBU LANGU!

Nisikilize mtu wa Mungu, si kila jambo unalopitia kwenye maisha yako lililo baya, ovu, la kuumiza moyo, kuondoa amani na furaha ni Mungu kaliruhusu na ni mapenzi yake!

Biblia inatuambia MAWAZO NA MIPANGO YA MUNGU KWETU NI YA AMANI NA SI YA MABAYA NI YA KUTUPA TUMAINI KATIKA KILA SIKU YETU IJAYO (Yeremia 29:11).
Sasa kama Mungu anasema anakaa chini kukuwazia mawazo ya kukuvusha, kukupeleka mbele, kukutoa ulipokwama, kutimiza kila maono na ndoto njema uliyobeba, UBAKUBALIJE SHETANI NA WATU WA DINI WAKUPE ELIMU TOFAUTI NA HIYO??
Usikubali chochote kisicho chema. Kisicho cha amani. Na kisicho cha kukupa tumaini la kusogea na kwenda utukufu mkubwa zaidi.

Isaya 53:4 Biblia inatuambia kuhusu kazi mojawapo iliyomleta Yesu msalabani;
“HAKIKA AMEYACHUKUA MASIKITIKO YETU, AMEJITWIKA HUZUNI ZETU”
Yesu hakufa kwa ajili ya wewe kuandikwa kwenye kitabu cha uzima na kuepuka Jehanamu tu. Alikufa pia ili kuhakikisha anakupa UFUNGUO WA MAMLAKA DHIDI YA HUZUNI NA MASIKITIKO.
Maana yake kupitia kazi ya msalaba una haki kisheria ya kuhukumu KILA KINACHOKUFANYA USIKITIKE NA KUHUZUNIKA.
Mungu hataki kuona huzuni wala masikitiko kwako; Ameshafanya sehemu yake kwa KUKUPA YESU, ni wajibu wako KUHUKUMU KILA CHANZO CHA HUZUNI NA MASIKITIKO MAISHANI MWAKO.

Ukiisoma Yohana 10:10, utapata siri kubwa kuwa aliyeko nyuma ya hali zote mbaya na ngumu za wanadamu ni IBILISI NA MAJESHI YAKE.
“MWIVI (Ibilisi) haji isipokuwa ACHINJE, AIBE NA AHARIBU; Bali MIMI (YESU) nalikuja ili WAWE NA UZIMA (kucounter attack hizo kazi tatu za Ibilisi kwenye maisha ya watu) kisha wawe nao tele”
Ukiona:
*Uharibifu (Mambo yanaharibika)
*Wizi (vitu kuibiwa au haki kupindishwa)
*Uuaji (wa roho za watu au mambo ya watu yanakufa, ndoa zinakufa, biashara zinakufa nakadhalika)
UJUE SHETANI NA MAJESHI YAKE WAKO KAZINI.
Ila ukiona NGUVU INAYOREKEBISHA vilivyoharibiwa, inarejesha vilivyoibiwa, inahuisha na kuvipa uhai vilivyouliwa, UJUE YESU (UFALME WA MUNGU UKO KAZINI)!
Usikae tu ukamuangalia Ibilisi anakuibia ukanyamaza.
Usikae tu na ukamuona Ibilisi anaharibu chochote kinachokuhusu halafu ukatulia tu.
Usikae tu na huku unaona mauti inapita kuua watu wako au vitu vyako na ukakaa tu; INUKA NA HASIRA YA KIUNGU NA HUKUMU HIZO NGUVU ZA KUZIMU.

Biblia inasema tangu tulipookoka tumepewa HAKI YA KISHERIA YA KUHUKUMU HATA MALAIKA;
“Hamjui ya kuwa MTAWAHUKUMU MALAIKA, basi SI ZAIDI SANA MAMBO YA MAISHA HAYA?”
(1Wakorintho 6:3).
Hii ni siri ya ajabu sana ndugu yangu… Siku ya mwisho sisi tutawahukumu malaika!
Na kama tunaweza kuwahuku MALAIKA WATAKATIFU WANAOKAA KWENYE UWEPO WA MUNGU; Je, si zaidi sana MAMBO YA MAISHA HAYA??

Ni mapenzi ya Mungu tuwe na uwezo wa KUHUKUMU MAMBO YA MAISHA HAYA HAPA DUNIANI!
Unakubali kuonewa na magonjwa?
Unakubali kuonewa na dhambi?
Unakubali kuonewa na umasikini?
Unakubali kusumbuliwa na wachawi?
Unakubali makahaba wachukue mme wako hivihivi?
Unakubali mabinti zako wazalie nyumbani?
Unakubali uwe mtu wa kuanzisha biashara na zinakufa?
COME ON… INUKA…SIMAMA NA UJITETEE… HUKUMU HIZO HALI ZINAZOKUBANA NA KUKUONDOLEA FURAHA NA RAHA YAKO!
Biblia inasema: TUYAHUKUMU MAMBO YA MAISHA HAYA!

Hawa ni baadhi ya waliohukumu mambo yasiyo na utukufu kwenye maisha yao;

i) YESU
-Alihukumu upepo na dhoruba iliyotaka kumzamisha na kumuua yeye na wanafunzi wake.
(Mathayo 8:23-27).

-Alihukumu mtini aliotarajia utampa matunda lakini badala yake ukaishia kumpa majani.
(Marko 11:13-21).

-Alikihukumu kifo kilichokuwa kimeondoa uhai wa rafiki yake Lazaro akawa hai tena baada ya siku nne za kuwa kaburini (Yohana 11).

ii) Paulo
-Alimhukumu mchawi Elima aliyekuwa anakwamisha kazi yake ya Injili aliyokuwa akiifanya, akawa kipofu saa hiyohiyo.
(Matendo 13:6-12).

-Alilihukumu pepo la utambuzi ndani ya mwanamke mmoja ambalo lilitumiwa na matajiri wa mji kujipatia pesa.
(Matendo 16:16-19).

iii) Samson
-Aliwahukumu Wafilisti waliokuwa wanafurahia kufungwa kwake, akawaua 1000 kwa taya la punda (Waamuzi 15:13-16).

-Aliwahukumu Wafilis ti waliomtoboa macho na kumfanya kituko.
Walikuwa wanashangilia kumtoboa macho na kuharibu maisha yake. Akawahukumu na wakafa wote siku ile.
(Waamuzi 16:23-30).

iv) Eliya
-Aliwahukumu manabii wa Baali walioidhalilisha na kuiharibu Ofisi ya kinabii katika israeli na akawaua kwa upanga.
(1Wafalme 18:38-40).

-Aliwahukumu askari waliotumwa kumkamata na kumpeleka kwa mfalme wa Samaria, wakafa kwa moto aliouamuru toka mbinguni.
(2Wafalme 1:9-15).

Nisikilize MLOKOLE MWENZANGU…Kuna wakati wa kuwa WAPOLE KAMA HUA…Na kuna wakati wa kuwa WAJANJA/WENYE BUSARA KAMA NYOKA (10:16)!
Ndugu zangu kuna wakati wa KUNYOLEWA MANYOYA KAMA KONDOO lakini kuna wakati wa KUTHIBITIKA KAMA SIMBA ALIYE CHINI YA SIMBA WA KABILA LA YUDA!!
Anza kutumia nguvu na mamlaka yako ndani ya Yesu kuhukumu KILA KILICHO NJE YA NENO LA MUNGU (MAPENZI YA MUNGU) JUU YA MAISHA YAKO!

WEWE NI MTU MKUU, NI MBARIKIWA, NI SHUJAA MKUBWA.

Advertisements

Karibu kwenye Tovuti ya Kikristo... hapa utapata mafunzo Mbali mbali ya kukujenga kiimani ,kifahamu,kimazingira na hata kitabia Karibu Tena

Tagged with: , ,
Posted in Mafunzo
One comment on “SIKU 30 ZA MIUJIZA NA MAAJABU. (SIKU ZA MFUNGO)[Day 18].
  1. Mwalimu Dickson Cornel Kabigumila umebarikiwa sana mtumishi wa Mungu, unayagusa sana maisha yangu.

Toa mawazo,maoni

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out / Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out / Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out / Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out / Change )

Connecting to %s

yaliyopita
Ungana nasi kwenye kurasa yetu  ya facebook na like page yetu-kuweza kutangaza neno la bwana na utabalikiwa sana..kwa kazi yako kuu kwani thawabu yako mbinguni ni tele

Andika E-mail kwenye box hapo chini kisha Bonyeza (jiunge Hapa)na uweze kujiunga na tovuti hii kupitia e-mail yako utakayojisajilia,tutaweza kukupa kila taarifa,habari zinazojili kwenye hii blog yetu asanteni

Join 2,215 other followers

Upcoming Events

No upcoming events

%d bloggers like this: