SIKU 30 ZA MAAJABU NA MIUJIZA. (SIKU 30 ZA MFUNGO)[Day 19].

4563054323/01/2016.

 

“KIBALI CHA KIUNGU (DIVINE FAVOR)”

Kibali ni upendeleo. Ni hali ya kukubalika na kupokelewa kwa urahisi bila kutumia nguvu au bidii kubwa.

Kati ya mambo ambayo Mungu alinifundisha mapema yanayoweza kufanya maisha yawe mepesi ni suala zima la KIBALI CHA KIUNGU (DIVINE FAVOR)!

Na niliamua kutenga muda kujifunza aina za vibali na namna ya kuzipata.
Pia namna ya kutunza vibali (how to mantain divine favor), maana unaweza kukipoteza.

Leo acha nikumegee siri hii, ishike kama uhai wako na tutakutana siku moja na utaniambia, “nimejionea matokeo ya Neno la Mungu”

AINA ZA VIBALI

1. KIBALI MBELE ZA MUNGU.

Hii ni hali ya kukubalika mbele za Mungu.
Paulo alimwambia mwanae wa kiroho Timotheo, “Jitahidi kujionyesha UMEKUBALIWA NA MUNGU (kwamba UNA KIBALI MBELE ZA MUNGU), mtenda kazi usiye na sababu ya kutahayari, ukitumia kwa halali Neno la kweli”
(2Timotheo 2:15).

Yesu pia alikuwa na aina hii ya Kibali.
” Na tazama sauti kutoka mbinguni ikisema, HUYU NI MWANANGU, MPENDWA WANGU, NINAYEPENDEZWA NAYE”
(Mathayo 3:17).
Kibali mbele za Mungu ni kuugusa na kuupendeza moyo wa Moyo wa Mungu.

*Paulo alikuwa na kibali mbele za Mungu.
(1Wathesalonike 2:4).

Nakuombea Mungu akukubali. Ifikie hatua Malaika wakija kukutembelea wanakuambia kama Danieli: “Eee…. Upendwae sana” (Danieli 10:11).
Mungu akukubali na kukupa upendeleo.

2. KIBALI CHA MUNGU KINACHOKUFANYA UKUBALIKE KWA WANADAMU.

*Waisraeli walipewa na Bwana KIBALI mbele ya Wamisri na wakapewa vyombo vya dhahabu na vya fedha walivyotaka toka kwa Wamisri.
(Kutoka 11:3).

*Mungu alimpa Yusufu KIBALI mbele ya mkuu wa gereza. Mkuu wa gereza akamfanya Yusufu kuwa mkuu wa wafungwa wote.
(Mwanzo 39:21).

*Mungu alimpa Danieli KIBALI na huruma mbele ya mkuu wa matowashi. Akapewa ruhusa ya kutokula vyakula vyenye kutia unajisi.
(Danieli 1:9).
Ni maombi yangu Mungu AKUPE KIBALI MBELE ZA WANADAMU utakaowafikia kila siku.

3. KUPATA KIBALI MBELE ZA WATU TOKA KWA WATU WENYEWE.
Hiki ni kibali ambacho Mungu hakupi moja kwa moja, bali anakwenda kwa mtu unayemuendea na kumfanya akukubali na kukupenda.

*Ruthu alipata kibali mbele ya Boazi.
Mwishowe aliolewa na huyu Boazi mbali ya kuwa hakuwa Mwisraeli na Ujane ukakoma.
(Ruthu 2:10,13).

*Daudi alipata kibali mbele ya Sauli.
“Kisha Sauli akapeleka watu kwa Yese, akasema, tafadhali, mwache Daudi asimame mbele yangu (Ikulu); maana AMEONA KIBALI MACHONI PANGU”
(1Samweli 16:22).

* Nehemia alipata kibali mbele ya Mfalme; akapewa ruhusa ya kutoka kwenda kuujenga mji wa Yerusalemu na akapewa na vifaa vya kuujengea.
(Nehemia 2:5-8).

*Esta alipata kibali na neema mbele ya Mfalme Ahusuero.
(Esta 2:17, 5:2, 7:3, 8:5).
Nakuombea Mungu akupe kupata kibali mbele ya wakuu.
Upate kibali machoni pao katika jina la Yesu.

MAMBO YATAKAYOKUFANYA UPATE KIBALI;

1. Mkono wa Mungu ulio juu yako.
“Kadri unavyoongezeka katika kiwango cha nguvu za Mungu (mkono wa Mungu) na kibali kinaongezeka”
Jifunze kwa Nehemia (2:5-8).

2. Uaminifu na Uadilifu.
Hii ndiyo ilikuwa siri ya Kibali cha Yusufu katika kila eneo la maisha yake.
“Hakukubali kupoteza uaminifu na uadilifu wake mbele za Mungu na wanadamu na alikuwa na kibali si mchezo”
(Mwanzo 39:21).

3. Kukemea uovu na kutoufumbia macho uovu.
(Mithali 28:23).

4. Hekima ya Kimungu inaleta Kibali.
(Mithali 8:11,12,35).

5. Kuoa/ kupata mke.
“Apataye mke apata kitu chema, maana apata KIBALI KWA BWANA”
(Mithali 18:22).
Kuna kitu ambacho watu hawajui kuhusu mke; Mke analeta kibali cha ajabu kama utampenda, utamheshimu na kumpa nafasi yake.
Kuna watu walioa wakiwa hawana kitu chochote na wakiwa si lolote na si chochote, lakini walipooa na kukaa vizuri na wake zao, KILA KITU KUHUSU WAO KIMEBADILIKA.
“Nioneshe mwanaume mwenye kujua thamani ya mkewe nami nitakuonesha mwanaume mwenye kibali kisichokuwa cha kawaida”
Wanaume wenzangu: Wafanye wake zenu wafurahi, maombi yenu yatajibiwa kwa speed kubwa na maisha yenu yatageuka haraka sana (1Petro 3:7).

6. Kushika na kutenda Neno la Mungu bila kujihurumia.
Watu wote waliolipa Neno la Mungu heshima ni watu wa kibali kisichokuwa cha kawaida.
Lichimbe Neno, ijue kweli, chukua Ufunuo wa Neno uishi, kibali kisichokuwa cha kawaida kitakuwa wazi maishani mwako.
(Mithali 3:1-4).

Njia rahisi ya kupoteza kibali ni kutofanya mambo hayo sita hapo juu.
Mungu akupe neema ya kuyatenda.

WEWE NI MKUU, SHUJAA NA MTU WA KURITHISHA VIZAZI VINGI VIJAVYO

Advertisements

Karibu kwenye Tovuti ya Kikristo... hapa utapata mafunzo Mbali mbali ya kukujenga kiimani ,kifahamu,kimazingira na hata kitabia Karibu Tena

Posted in Mafunzo

Toa mawazo,maoni

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out / Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out / Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out / Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out / Change )

Connecting to %s

yaliyopita
Habari iliyotazamwa sana
Ungana nasi kwenye kurasa yetu  ya facebook na like page yetu-kuweza kutangaza neno la bwana na utabalikiwa sana..kwa kazi yako kuu kwani thawabu yako mbinguni ni tele

Andika E-mail kwenye box hapo chini kisha Bonyeza (jiunge Hapa)na uweze kujiunga na tovuti hii kupitia e-mail yako utakayojisajilia,tutaweza kukupa kila taarifa,habari zinazojili kwenye hii blog yetu asanteni

Join 2,212 other followers

Upcoming Events

No upcoming events

%d bloggers like this: