SIKU 30 ZA MAAJABU NA MIUJIZA. (MFUNGO WA SIKU 30) [Day 20]

Day 20, 24/01/2016.

https://livinginfaithtogether.files.wordpress.com/2012/04/david_goliath_bible_hero_poster.jpg?w=514&h=635

“UPAKO WA VITA (ANOINTING FOR BATTLE)”

Unajua ni hatari sana kuishi kwenye uwanja wa vita na usiwe umejipanga kwa vita.
Utakufa huku unajitazama.
Kama ambavyo taifa la Israeli lilitetea uhai wake na ustawi wake kwa vita; Kanisa la Siku za mwisho haliwezi kuwa na ushindi dhidi ya kazi za kuzimu bila kuwa na UPAKO WA VITA.

Agano jipya limezungumza kuhusu vita kwa Mkristo wa siku za mwisho. Kama ulipookoka uliambiwa KWA YESU TAMBARARE hawakukosea, lakini walipaswa kukuambia pia hapa duniani ulipo ni mahali pa vita.
Yesu mwenyewe anasema: “YEYE ASHINDAYE…” akiwa na maana tuko kwenye vita au aina mojawapo ya mapambano ambayo UKIZUBAA UNAWEZA KUSHINDWA ndio maana kuna MOTISHA KWA “YEYE ASHINDAYE”

YEYE ASHINDAYE:
“Yeye ashindaye nitampa kula matunda ya mti wa uzima ulio katika bustani ya Mungu”
(Ufunuo 2:7).
Ni muhimu ujue YESU KRISTO NI MTI WA UZIMA… Kuna matunda anayo ambayo hautayapata mpaka USHINDE KWENYE MAENEO FULANI.
Usipopigana vita vizuri vya imani kuna vitu HAUTAVIPATA INGAWA YESU (MTI WA UZIMA) ANAVYO. Ni wajibu wako kupambana mpaka upate kila tunda ambalo Yesu anatoa bure kwenye maisha yako kwa sababu umeokoka!

“Yeye ashindaye NITAMPA BAADHI YA ILE MANA ILIYOFICHWA, nami nitampa jiwe jeupe, na juu ya jiwe hilo limeandikwa jina jipya asilolijua mtu ila yeye anayelipokea”
(Ufunuo 2:17).
Kuna SEHEMU YA MANA ILIYOFICHWA ambayo hautaipata mpaka upambane na kushinda.
Mana iliyofichwa ni MAARIFA YA UFALME WA MUNGU YATAKAYOIFUNIKA DUNIA SIKU ZA MWISHO KAMA MAJI YAFUNIKAVYO BAHARI (Isaya 11:9, Habakuki 2:14, Hesabu 14:21).
Kuna AINA ZA UFUNUO ambazo kanisa la kwanza hawakuzipata. Kuna siri za Ufalme wa Mungu ambazo Mungu amekusudia kuziachia siku hizi za mwisho lakini ili uweze kuzi-access LAZIMA USHINDE ROHONI.
Si kila mtu anaweza kupata FLESH MANA ambayo itageuza maelfu na maelfu ya watu, ni watu WASHINDAO TU.
Nimeshinda na naendelea kushinda ndio maana kuna REVELATION nakuja nazo kila siku ambazo hukuwahi kuzisikia au kuzisoma popote.
It takes wrestling and battling into the spirit to obtain divine revelations.
Danieli alitumia siku 21 akitafuta ufunuo.
Yesu alitumia siku 40 kabla ya kuja na Ufunuo wa Luka 4:18-19 ambao ni mwongozo wa huduma yako; Unapaswa kushinda pia ili uwe na access kwenye HAZINA ZA MAARIFA NA HEKIMA zilizositirika ndani ya Kristo Yesu!

Pia kupewa jiwe jipya jeupe lenye JINA LA MSHINDI analolijua mshindi peke yake inasimama kama KIWANGO NA DARAJA JIPYA ambalo mtu akishinda na kujiimarisha rohoni ANAJUA NA ALIYEMPA JINA KWENYE ULIMWENGU WA ROHO ANAJUA hata kama walioko chini bado wanamuona ni mtu wa kawaida!
Kwa mantiki hii usikubali kupoteza pambano lolote kama unataka kupata vitu ambavyo wanaoshindwa hawawezi kupata!

“Yeye ashindaye na KUYATUNZA MATENDO YANGU HATA MWISHO, nitampa MAMLAKA JUU YA MATAIFA”
(Ufunuo 2:26).
Watu wengi tunapenda mamlaka kwenye ulimwengu wa roho; Ukisema duniani vifanyike mbinguni.
Ukifunga duniani vifungwe mbinguni na ukifungua vifunguliwe mbinguni (kwenye ulimwengu wa roho)!
Lakini hatujui kuwa ili utembee kwenye VIWANGO HIVYO lazima USHINDE.
Unashindaje? KWA KUTUNZA MATENDO YAKE HATA MWISHO.
Yaani kwakuwa SHAHIDI MWAMINIFU WA YESU kwa maneno, matendo na kila ulifanyalo; KUWA CONSISTENT kwenye KUMUISHI KRISTO YESU!
“Ninyi ni barua ya Kristo isomwayo na watu wote…” (2Wakorintho 3:1-3).
“Yeye asemaye ya kuwa anakaa ndani yake, IMEMPASA KUENENDA MWENYEWE VILEVILE KAMA YEYE ALIVYOENENDA”
(1Yohana 2:6)
Be consistent in your walk with Jesus!
Halafu utashangaa MAMLAKA YAKO KWENYE ULIMWENGU WA ROHO itakavyoongezeka sana!

“Yeye ashindaye atavikwa mavazi meupe, wala sitalifuta kamwe jina lake kwenye kitabu cha uzima, nami nitalikiri jina lake mbele za Baba yangu, na mbele za Malaika zake”
Kushinda ni kitu cha muhimu sana kwa Mkristo.
Nilipolisoma andiko hili niliona kumbe kuna uwezekano wa MTU KUFUTWA KWENYE KITABU CHA UZIMA KAMA HATASHINDA.
Ni hasara iliyoje kufika mbele za Mungu na jina lako halionekani?
Utakuwa kama “YULE BWANA MJINGA” kwenye wimbo wa KALE NILITEMBEA.
Jitahidi ushinde kila iitwapo leo.
Usikubali kushindwa na majaribu. Usikubali kushindwa na dhambi.
Usikubali kushindwa na ubaya.
Ukishinda YESU ANAKUKIRI MBELE ZA MUNGU BABA NA MBELE ZA MALAIKA ZAKE;
Na hiyo inaufanya Ufalme wa Mungu upigane upande wako kukusaidia katika hali zote unazopitia hapa duniani!

NINI UNAPASWA KUKISHINDA?

1. Dhambi
“Dhambi iko mlangoni inakuotea lakini YAKUPASA UISHINDE”
(Mwanzo 4:7).
Kushinda dhambi si ombi NI LAZIMA.
Unapaswa kushinda kama unataka KUOKOA HATMA YAKO.
Yusufu ALIISHINDA DHAMBI akaponya hatma yake.
(Mwanzo 39).
Adamu na mkewe walishindwa na dhambi wakaharibu hatma zao na zetu hata leo (Mwanzo 3).
Yesu Kristo alijaribiwa katika mambo yote sawa na sisi lakini HAKUSHINDWA NA DHAMBI (Waebrania 4:15).
Nawe unaweza kuishinda kila dhambi na kunusuru hatma yako na vizazi vyako vingi vijavyo.

2. Ufalme wa giza
“Hatimaye mzidi kuwa hodari katika Bwana na katika uweza wa nguvu zake. Vaeni silaha zote za Mungu ili mpate kuzipinga hila zote za Shetani. KWA MAANA KUSHINDANA KWETU SISI si juu ya damu na nyama; bali ni juu ya FALME NA MAMLAKA, JUU YA WAKUU WA GIZA HILI, JUU YA MAJESHI YA PEPO WABAYA KATIKA ULIMWENGU WA ROHO. Kwa sababu hiyo twaeni silaha zote za Mungu mpate kushindana siku ya uovu, na mkiisha kuyatimiza yote kusimama”
(Waefeso 6:10-13).
Hii ni vita COMPLICATED kuliko vita ya MABOMU NA RISASI.
Hii ni vita inayohitaji ujuzi wa Kweli za Neno la Mungu ili Uweze kushinda.
Yesu amewahi kukutana na hii vita mara nyingi.
Kule jangwani alikutana na hii vita na akashinda (Luka 4:1-13).
Paulo alikutana na vita hii na akashinda (Matendo 13:6-11, Matendo 16:16-34).
Wewe pia UMESHAANZA KUPAMBANA NAZO hata kama ulikuwa hujui.
Sasa ni vema ujue ili ujue namna ya kuwa salama (kujilinda) na pia kushambulia na kushinda!
Una silaha ambazo ziko tayari kwa ajili yako utashinda kila vita dhidi ya giza ukitumia kwa imani.
Baadhi ya silaha hizo ni:

i). Chapeo ya wokovu kichwani.
(Waefeso 6:17).
Kichwani ndiko kuwaza na kutafakari kunafanyika.
Kila muda jiwazie na kujitafakari kama MTU ALIYEOKOKA.
Jaza kichwa chako kwa ukweli huu na usikubali kitu kingine chochote akilini mwako.
Kujua kuwa umeokoka itakufanya mara moja UJIJUE WEWE NI NANI NDANI YA KRISTO (2Wakorintho 5:21, Waefeso 2:19, 1Petro 2:9, Ufunuo 5:9-10, Yohana 1:12-13, 1Yohana 3:1-2), na hii itakupa JEURI YA KIPEKEE DHIDI YA KILA KAZI YA KUZIMU.
Ulinzi ulionao (Zaburi 34:7, Zaburi 91:11-12, Zekaria 2:5,8, 1Petro 1:5, Yuda 1:24).
Jizoeze kuweka kichwani mwako KWELI YA WOKOVU usivue CHAPEO YAKO YA WOKOVU (Helmet of salvation)!

ii) Kweli viunoni (Waefeso 6:14).
Neno la Mungu ni kweli (Yohana 17:17).
Jumla ya Neno la Mungu ni Kweli (Zaburi 119:160).
Kuwa MTU WA NENO ili uwe salama Shetani asije kukuweka uchi.
When he takes your BELT OF TRUTH you become naked and ashamed.

iii) Haki kifuani (Waefeso 6:14).
Hakuna kitu kinachoweza kuuvuta mkono wa Mungu kwa mtu kama kuishi maisha ya haki.
Hii ni kwa sababu;
“Mabaya hayataisogelea hema ya mwenye haki”
(Zaburi 91:10)
Lakini pia “Mungu humpenda mwenye haki…” (Zaburi 146:8c).
Maisha ya haki yanalipa rafiki yangu.
Habari njema Yesu ameshakufanya mwenye haki (Warumi 8:33:34).
Wewe ni haki ya Mungu (2Wakorintho 5:21).
Hivyo basi dumu KUTENDA HAKI maana, “ATENDAYE HAKI YUNA HAKI KAMA YEYE MUNGU ALIVYO NA HAKI (1Yohana 3:7).
Ni wajibu wangu na wako kudhihirisha kwa dunia yetu kwamba sisi ni wenye haki kwa kutenda haki.

iv)Utayari kwa ajili ya injili (Waefeso 6:15).
Hubiri injili (Mathayo 28:18-19).
Sapoti injili; Huduma za semina, mikutano na vitu vinavyosukuma injili mbele kwa pesa yako (Marko 10:28-30).
Peleka watu kuhubiri habari njema kwa mali yako (Warumi 10:14-15).
Hakikisha unasukuma injili mbele kwa kuhusika moja kwa moja na kwa kusapoti ni silaha itakayokuepusha na mashambulizi ya Ibilisi na Ufalme wake!

v) Ngao ya imani (Waefeso 6:16).
Kazi ya IMANI ni KUZIMA MISHALE YOTE AMBAYO IBILISI ANAIRUSHA KWAKO.
*Taarifa mbaya
*Kusalitiwa
*Magonjwa
*Kuharibikiwa
*Kupoteza uwapendao
Hii yote ni baadhi ya MISHALE YA MOTO YA YULE ADUI.
Hauwezi kuizima kwa kulia machozi au kwa kumlalamikia Mungu bali kwa NGAO YA IMANI.
Imani hii utaipata kwa kulisikia Neno la Kristo na habari zinazohusu matendo makuu ya Yesu (Warumi 10:17, Marko 5:25-28).
Jilishe Neno la Mungu kwa wingi kukuza imani yako.
Soma vitabu vya Kiroho.
Hudhuria semina mbalimbali.
Angalia DVD na kusikiliza VCD za Mafundisho ya Neno la Mungu na shuhuda za wengine.
Imani yako itakua na hautaweza kusogezwa na chochote na utaizima mishale yote ya yule mwovu.

vi) Upanga wa Roho (Waefeso 6:17).
Ukiisoma Waefeso 6:10-18, silaha pekee ya kushambulia iliyotajwa ni NENO LA MUNGU.
Nataka uone hii siri; NENO LA MUNGU NDILO SILAHA YA VITA YA ROHO MTAKATIFU.
Hata kama umejaa Roho mtakatifu lakini hauna Neno, Imekula kwako rafiki.
Roho wa Mungu hafanyi chochote bila Neno la Ufunuo ulilodaka na kutunza.
Lijaze Neno la Kristo kwa wingi ndani yako ili UMPE SHIDA ibilisi na majeshi yake.
“Neno la Kristo na likae kwa wingi ndani yenu” (Wakolosai 3:16).
KIWANGO CHA UTENDAJI WA ROHO MTAKATIFU MAISHANI MWAKO KINATEGEMEA KIWANGO CHA NENO ULICHONACHO.
“Neno la Mungu li hai, tena lina nguvu…” (Waebrania 4:12).

vii) Kudumu katika maombi (Waefeso 6:18).
Hapa siongelei kuomba mara moja moja.
Hapa naongelea kuwa MTU WA MAOMBI.
Kuyafanya maombi kuwa pumzi yako.
Prophet TB Joshua anasema;
“A break in prayer is a break in God because prayer brings you in His presence. The moment you switch that off you loose His frequence”
Natamani ujipange vizuri kwenye eneo la maombi.
Danieli alikuwa Waziri mkuu kule Babeli, very busy man lakini alikuwa ANAOMBA MARA TATU KWA SIKU (Danieli 6:10).
Sasa mwenzangu sijui wewe ni WAZIRI MKUU WA NINI??
Jipange, acha uzembe.
Dumu katika kuomba (Wakolosai 4:2).
Siri ya muhimu:
UNAPOOMBEA WATUMISHI WA MUNGU HASA AMBAO WANAKUVUSHA KIROHO NEEMA ILIYOKO JUU YAKO INAKULINDA.
“…Mkidumu katika kuwaombe watakatifu wote. Pia na kwa AJILI YANGU MIMI PAULO (MTUMISHI WA MUNGU) ili nipewe usemi kwa kufumbua kinywa changu, NIIHUBIRI KWA UJASIRI ILE SIRI YA INJILI” (Waefeso 6:18-19).
Usiache kuwaombe watumishi wa Mungu hasa mimi Mwalimu Dickson Cornel Kabigumila ninayekupa siri hizi.

3. Ubaya
“Usishindwe na Ubaya bali uushinde ubaya kwa wema”
(Warumi 12:21).
Nakuomba utenge muda usome Warumi 12 yote uone yakupasayo ili uushinde ubaya.
Na Mungu atakubariki unapotii na kuyatenda.

iv) Imani
“Wapenzi nilipokuwa nikifanya bidii sana kuwaandikia habari ya wokovu ambao ni wetu sisi sote, naliona imenilazimu kuwaandikia, ili niwaonye kwamba MUISHINDANIE IMANI WALIYOKABIDHIWA WATAKATIFU MARA MOJA TU”
(Yuda 1:3).
Hapa haongelei imani juu juu. Anaongelea IMANI SAHIHI YA WOKOVU.
Mstari wa 4 anaeleza ni kwa sababu kuna WATU MAKAFIRI wamejiingiza kwa siri na kugeuza INJILI YA KWELI.
Usikubali kuiuza na kuipoteza imani yako kwa wokovu wa kweli.
Pima na kukagua kila kitu kwa Neno la Mungu ili kuoba kama viko hivyo au la kama Waberoya (Matendo 17:10).
Chunguza na kupima kila kitu kwa Neno la Mungu.
Chochote kinachokutatiza na kinachogoma rudi kwenye Biblia yako; Usitafune kila kitu.

Naamini ukitulia na kuyaelewa mambo haya na kuyatenda, UPAKO WA VITA utakuwa juu yako na utashinda kila vita.
Umebarikiwa,
WEWE NI SHUJAA MKUBWA, NI MTU MKUU MWENYE MAJIBU YA WENGI.

Advertisements

Karibu kwenye Tovuti ya Kikristo... hapa utapata mafunzo Mbali mbali ya kukujenga kiimani ,kifahamu,kimazingira na hata kitabia Karibu Tena

Tagged with: , ,
Posted in Mafunzo

Toa mawazo,maoni

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out / Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out / Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out / Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out / Change )

Connecting to %s

yaliyopita
Habari iliyotazamwa sana
Ungana nasi kwenye kurasa yetu  ya facebook na like page yetu-kuweza kutangaza neno la bwana na utabalikiwa sana..kwa kazi yako kuu kwani thawabu yako mbinguni ni tele

Andika E-mail kwenye box hapo chini kisha Bonyeza (jiunge Hapa)na uweze kujiunga na tovuti hii kupitia e-mail yako utakayojisajilia,tutaweza kukupa kila taarifa,habari zinazojili kwenye hii blog yetu asanteni

Join 2,215 other followers

Upcoming Events

No upcoming events

%d bloggers like this: