SIKU 30 ZA MIUJIZA NA MAAJABU. (SIKU 30 ZA MFUNGO)[Day21].

 

Day 21, 25/01/2016.

https://i2.wp.com/conference.myonlycomfort.org/wp-content/uploads/2013/10/1012.jpg

“FUNGUO ZA UFALME WA MBINGUNI (THE KEYS OF THE KINGDOM OF GOD)”

Mathayo 16:19.
“Nami nitakupa wewe FUNGUO ZA UFALME WA MBINGUNI; NA LOLOTE utakalolifunga duniani, litakuwa limefungwa mbinguni; NA LOLOTE ambalo utalifungua duniani litakuwa limefunguliwa mbinguni”

Angalia haya maneno;

i)UNGUO ZA UFALME WA MBINGUNI
ii)LOLOTE

i) Funguo za Ufalme wa mbinguni;

1. Ni funguo ambazo zinamilkiwa na Ufalme wa Mbinguni ndiyo maana zinaitwa “funguo za Ufalme wa mbinguni (funguo mali ya ufalme wa mbinguni)”!

Ili uwe na haki ya kuzitumia lazima kwanza uwe raia wa Ufalme wa Mbinguni (Waefeso 2:19, 1Petro 2:9, Ufunuo 5:9-10).

Pili, ni lazima uwe na mahusiano mazuri na Mmilki au Mfalme wa Ufalme huo ili uweze kupata faida ya kuwa kwenye Ufalme.
Kwa lugha nyepesi; Hata ukiwa raia wa Ufalme wa mbinguni lakini ukaondoka kwenye Ufalme (Uwepo wa Mungu), hautapata faida zilizoko kwenye Ufalme kwa vile tu wewe ni raia/ mtoto wa Mfalme.
Mwana mpotevu alikuwa biological son wa Baba tajiri lakini alipotoka kwenye Uwepo wa Baba yake alipatwa na matatizo yanayopata wengine walioko nje ya eneo la milki ya baba yake.
Alijua kwa baba kuna kila kitu lakini kule kuwa mbali na kwa babaye kulimfanya akose yaliyoko kwenye Ufalme.
Mpaka aliporudi kwenye UWEPO WA BABA YAKE ndipo sherehe na maisha mazuri yalipoanza.
(Luka 15:11-27).

Hata kama utasoma hili somo la FUNGUO ZA UFALME WA MUNGU na kuona mambo mazuri yanayoweza kuwa yako; Kama uko mbali na Ufalme wa Mungu (HAUJAOKOKA) au Umeokoka lakini HUNA USHIRIKA NA MUNGU hakika utaishia kusoma na hili somo halitakusaidia.
Anza kwa kumpa Yesu maisha yako kama hujaokoka.
Na kama umeokoka lakini ulikuwa umerudi nyuma tengeneza na Mungu uanze upya.
Hii itakuwa njia pekee ya kukupa nafasi ya kupata faida za FUNGUO ZA UFALME WA MBINGUNI.
Hizi funguo zinawapa faida walioko kwenye uwepo wa Mfalme.

2. Funguo za Ufalme wa Mbinguni

Hizi ni funguo ambazo zinafanya mambo yatokee duniani na kutokea kwa mtu aliyefungulia duniani, lakini KITASA CHA KUINGIZIA UFUNGUO kiko mbinguni.
Ndio maana inasema: Utakalolifunga au kulifungua DUNIANI litafungwa au kufunguliwa MBINGUNI.
Hizi ni funguo za kipekee.
Command ya kufungua inatolewa dunia kwenda mbinguni na ikitick huko matokeo yanaonekana sekunde hiyohiyo hapa duniani!
Yaani mimi nikiwa hapa duniani, nikafuzu (nikapatia ufunguo sahihi) kwenye mlango sahihi mbinguni (kwenye ulimwengu wa roho) matokeo yanaonekana waziwazi hapa duniani.

Nikupe siri:
Funguo hizi HAZIONEKANI KWA MACHO YA NYAMA, HAZISHIKIKI KWA MIKONO YA KIBINADAMU lakini zinafungua na kufunga vitu na matokeo YANAONEKANA NA KUSHIKIKA hapa duniani!
Hii ni ajabu lakini ni kweli.
Nazipenda mno hizi FUNGUO ZA UFALME WA MBINGUNI.

ii) Na Lolote
Sifa kubwa ya Funguo hizi ni Uwezo wa KUFUNGUA LOLOTE.
Yaani ukizitumia kwa usahihi bila kuvunja kanuni yoyote inayozitawala hakika zitafungua chochote na zitafunga chochote.
Hakuna kitu ambacho hizi funguo hazina mamlaka juu yake.
Nakuombea unapopita kwenye shule hii udake siri zitakazokufanya uwe “ishara na ajabu kwa dunia yako” (Isaya 8:18).

BAADHI YA FUNGUO ZA UFALME WA MUNGU;

1. MAOMBI
“YOYOTE (lolote, chochote) MUYAOMBAYO MKISALI aminini ya kuwa mnayapokea nayo yatakuwa ya kwenu”
(Marko 11:24).
“Yoyote” MUYAOMBAYO… Hii ina maana maombi yanaweza kutumika kama ufunguo kufunga au kufungua yoyote duniani na ikafanyika mbinguni endapo kanuni ya “IMANI” itazingatiwa!
“…AMININI YA KUWA MNAYAPOKEA, nayo yatakuwa yenu (yatafungwa au kufunguliwa)”
Ufunguo huu kwa mstari huu unategemea IMANI YA MUOMBAJI wakati wa kuomba (AAMINI AMEYAPOKEA MUDA HUO), halafu akitoka kwenye maombi na kukutana na mazingira yanayoonesha kinyume na ALICHOPOKEA KWENYE MAOMBI basi awashe IMANI YA KUPOKEA NA KUZIMA MISHALE YOTE YA MOTO YA YULE ADUI.

Angalia andiko jingine kuhusu UFUNGUO HUU WA MAOMBI;
“NANYI MKIOMBA LOLOTE KWA JINA LANGU, hilo nitalifanya, ili Baba atukuzwe ndani ya Mwana”
(Yohana 14:13).
Hapa tunaona tena MAOMBI YANAFUNGUA AU KUFUNGA CHOCHOTE lakini endapo umechanganya na JINA LA YESU kwa malengo kuwa Mungu pekee atatukuzwa kupitia jina la mwanae endapo hilo jambo litafungwa au kufunguliwa.
“Ili Baba atukuzwe ndani ya Mwana”
Ukiomba chochote lakini MOYONI HAUKUKUSUDIA KUMTUKUZA MUNGU BABA uwe na uhakika UFUNGUO WA MAOMBI utagoma kufunga au kufungua hicho kitu!

Baadhi ya Mambo yanayozuia Ufunguo wa Maombi usifanye kazi;
*Kutosamehe
(Marko 11:25-26).
*Kutokuamini moyoni kuwa yamekuwa uliyoomba (Marko 11:23-24).
*Dhambi (Yohana 9:31).
*Kuwa na nia mbili/ kutokuwa na tarajio moja baada ya maombi; mtu yeyote anayesema “Huenda itakua au haitakuwa hatapata kitu kwa Mungu” (Yakobo 1:5-7).
*Kuomba ili kuvitumia uombavyo kwa tamaa zako mwenyewe; Mfano, Unaomba Mungu akubariki ili uoe na mke wa pili, hatafanya hilo kamwe!
(Yakobo 4:2-3).

2. IMANI
“…YOTE YAWEZEKANA KWAKE AAMINIYE”
(Marko 9:23).
Huu ni ufunguo wa ajabu sana ambao UNAFUNGA NA KUFUNGUA CHOCHOTE AU LOLOTE.
Lakini nao una kizuizi kikubwa kimoja ambacho kinaweza kuufanya usifanye kazi sawasawa, “KUKOSA UPENDO”
Hii ni kwa sababu;
“Imani hufanya kazi kwa upendo”
(Wagalatia 5:6).
Hakuna upendo na imani imegoma.
Imani haitendi kazi mpaka uwe vizuri kwenye upendo; Na hauwezi kuwa na upendo na ukawa haujasamehe, haiwezekani… Upendo ndio moyo wa kuifanya imani izae miujiza!
“Nijapokuwa na IMANI TIMILIFU ya kuhamisha milima; KAMA SINA UPENDO SI KITU MIMI”
(1Wakorintho 13:2).
Tengeneza UPENDO WAKO halafu utashangaa UFUNGUO WA IMANI UTAKAVYOANZA KUFUNGUA MILANGO KWA AJILI YAKO!

3. JINA LA YESU
“Ili KWA JINA LA YESU KILA GOTI lipigwe, la vitu vya mbinguni, na vya duniani, na vya chini ya nchi; na KILA ULIMI UKIRI ya kuwa Yesu Kristo ni Bwana kwa utukufu wa Mungu Baba”
(Wafilipi 2:10-11).
Huu ni ufunguo wa ajabu sana. Unaweza kushughulika na KILA ULIMI NA KILA GOTI LA KILA KITU CHA MBINGUNI (Malaika, baraka zetu zilizoko mbinguni, majibu yetu yaliyoko mbinguni, mapenzi ya Mungu kwetu yaliyo mbinguni nakadhalika), vya duniani (Watu, viumbe vinavyoonekana na visivyoonekana, hali na mazingira), na vya chini ya nchi (vya kuzimu; Shetani na majeshi yake yote)!
Huu ni Ufunguo wa ajabu ambao “KILA ALIYEOKOKA” amepewa na kumilkishwa;
“…kwa maana hakuna jina jingine TULILOPEWA wanadamu litupasalo kuokolewa kwalo…” (Matendo 4:12).
Hili ni jina ambalo TULIOOKOKA TUMEPEWA na kila ANAYEOKOKA ANAPEWA!
Na kwa utaratibu wa majina ukipewa jina linakuwa lako na linakuwa mali yako.
Baraka au laana zake zinakuwa zako.
JINA LA YESU NI JINA TULILOPEWA.
UMEPEWA, NIMEPEWA, TUMEPEWA!
Linaweza kufanya chochote lakini lina vizuizi vyake;
*Kutookoka
Hili ni jina walilopewa wanaookolewa (Matendo 4:12).
*Kukosa utii MAPENZI YA MUNGU KWAKO; Yesu alinyenyekea na kutii MAPENZI YA MUNGU KWAKE na ndipo alipopewa UFUNGUO HUU NA NGUVU YAKE (Wafilipi 2:5-11).
Huwezi kutumia ufunguo huu wa Ufalme wa Mbinguni kama wewe si mnyenyekevu na mtiifu kwa Mungu na mapenzi yake ambayo tunayapata kwenye Neno lake!
*Kukosa imani maalum juu ya JINA LA YESU; Watu wengi wanamwamini Yesu bila wasiwasi lakini hawana kiwango hichohicho cha Imani kwa jina lake, na hiyo inazuia jina la Yesu lisitoe matokeo makubwa.
“NDIO WALE WALIAMINIO JINA LAKE (Wenye imani katika jina la Yesu kama wanavyomuamini Yesu mwenyewe): (Yohana 1:12).
“Na KWA IMANI KATIKA JINA LAKE (JINA LA YESU)…” (Matendo 3:16).
Biblia inasisitiza sana kuhusu KUJENGA IMANI KWENYE JINA LA YESU kama tunavyomuamini Yesu mwenyewe (Yohana 2:23, Yohana 3:18, 1Yohana 3:23, 1Yohana 5:13).
Kwa faida yako mwenyewe JENGA IMANI KUHUSU UWEZA NA NGUVU ZA JINA LA YESU!

Kwa leo tuishie hapa,
Umebarikiwa,
WEWE NI MTU MKUU, SHUJAA NA SULUHU YA MAISHA YA WENGI!

Advertisements

Karibu kwenye Tovuti ya Kikristo... hapa utapata mafunzo Mbali mbali ya kukujenga kiimani ,kifahamu,kimazingira na hata kitabia Karibu Tena

Tagged with: , ,
Posted in Mafunzo

Toa mawazo,maoni

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out / Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out / Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out / Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out / Change )

Connecting to %s

yaliyopita
Ungana nasi kwenye kurasa yetu  ya facebook na like page yetu-kuweza kutangaza neno la bwana na utabalikiwa sana..kwa kazi yako kuu kwani thawabu yako mbinguni ni tele

Andika E-mail kwenye box hapo chini kisha Bonyeza (jiunge Hapa)na uweze kujiunga na tovuti hii kupitia e-mail yako utakayojisajilia,tutaweza kukupa kila taarifa,habari zinazojili kwenye hii blog yetu asanteni

Join 2,219 other followers

Upcoming Events

No upcoming events

%d bloggers like this: