SIKU 30 ZA MAAJABU NA MIUJIZA. (SIKU 30 ZA MFUNGO)[Day 23 ].

27/01/2016.

“NGUVU YA SHUHUDA (THE POWER OF TESTIMONS)”

“Nao wakamshinda kwa damu ya Mwanakondoo, na kwa NENO LA USHUHUDA WAO…”
(Ufunuo 12:11).

Watu wengi hawajui ni kwanini shuhuda ni za muhimu katika maisha ya imani. Na hawajui pia namna ya kuzitumia shuhuda kwa namna chanya ili zizae miujiza na mambo makubwa kwenye maisha yao.
Katika somo hili nataka upate siri kutoka katika Neno la Mungu kuhusu NGUVU YA SHUHUDA katika maisha ya imani.
Biblia inataja NENO LA USHUHUDA kama silaha moja wapo ambayo walionunuliwa kwa damu ya Mwanakondoo wanaweza kuitumia na kumshinda adui na hila zake!
Nataka uweke moyo na akili yako kwenye kinachofuata hapa chini, na Mungu akupe neema udake siri hizi za Ufalme wa Mungu!

NGUVU ZILIZOMO NDANI YA SHUHUDA;

1. NDANI YA SHUHUDA KUNA NGUVU YA KUINUA IMANI YA MTENDEWA MUUJIZA KWA PAMBANO LA KIROHO LILILOKO MBELE YAKE AU ANALOPITIA.

Ukisoma kitabu cha 1Samweli 17, utamuona kijana mdogo, mchunga kondoo aitwaye Daudi.
Huyu kijana alikuja kwenye kambi ya majeshi ya Israeli na kuyakuta yanahangaishwa na adui kwa muda wa siku 40 (Mwezi mmoja na siku 10).
Na walishakosa suluhu ya kutatua tatizo hilo liitwalo GOLIATI.
Lakini huyu kijana alikuja na akaanza kutangaza kuwa anaweza kuliondoa hilo tatizo.
Walipomuuliza atawezaje kushinda na hana uzoefu na vita na anapigana na shujaa wa vita wa tangu ujanani, ALIWAPA SHUHUDA ZA MAMBO AMBAYO MUNGU AMETENDA KUPITIA YEYE.
Aliwaambia, “MTUMISHI WAKO ALIKUWA AKICHUNGA KONDOO ZA BABA YAKE, NA ALIPOKUJA SIMBA, AU DUBU, AKAMKAMATA MWANAKONDOO WA LILE KUNDI, MIMI HUTOKA NIKAMFUATA, NIKAMPIGA, NIKAMPOKONYA KINYWANI MWAKE; NA AKINIRUKIA HUMSHIKA NDEVU ZAKE, NIKAMPIGA, NIKAMUUA. MTUMISHI WAKO ALIMUUA SIMBA NA DUBU PIA, NA HUYU MFILISTI ASIYETAHIRIWA ATAKUWA KAMA MMOJA WAO, KWA SABABU AMEWATUKANA MAJESHI YA MUNGU ALIYE HAI. DAUDI AKASEMA, BWANA ALIYENIOKOA NA MAKUCHA YA SIMBA, NA MAKUCHA YA DUBU, ATANIOKOA MA MKONO WA MFILISTI HUYU…”
(1Samweli 17:34-37).
Biblia inasema “IMANI UHAKIKA WA MAMBO YATARAJIWAYO…” (Waebrania 11:1).
Daudi anasema kwa UHAKIKA KUHUSU ANACHOTARAJIA KUPATA DHIDI YA GOLIATI;
“Bwana aliyeniokoa na makucha ya simba, na makucha ya dubu, ataniokoa na mkono wa Mfilisti huyu”
“…BWANA ALIYENIOKOA…ATANIOKOA…”
Hii ni imani!
Imani iliyokuwa ndani ya Daudi kwa sababu ya SHUHUDA MBILI ALIZOKUWA NAZO kuhusu dubu na kuhusu simba aliowaua kwa MSAADA WA BWANA!
Mungu akishakutendea jambo ambalo linakuonesha ni mkono wa Mungu si kibinadamu, linakufanya UMUAMINI KWA MAMBO MENGINE.
Inakujengea uhakika kuwa Mungu yuko upande wako na akiwa upande wako hakuna wa kuwa juu yako (Warumi 8:31)!
Kumbuka hii:
“TUMIA MUDA WAKO KUJIKUMBUSHA YALE AMBAYO MUNGU AMEKUTENDEA TANGU UPATE UFAHAMU, NA IMANI YAKO ITAKUA KULIKO JITU LILILOKO MBELE YAKO”

2. SHUHUDA UWAFANYA WANAOKUPINGA KWAMBA HUWEZI KUPATA USHINDI KUUNGANA NA WEWE.

Daudi aliposema anaweza kumshinda Goliati na kukikata kichwa chake hakuna aliyemuamini.
Alipojieleza kwa askari wa Sauli wakamuelewa wakaacha kumpinga na wakamleta kwa Mfalme Sauli.
Alipofika kwa Sauli, ndipo alipoanza KUKATISHWA TAMAA NA KUAMBIWA HAWEZI KUSHINDA.
Lakini alipoanza kushuhudia kile ambacho Mungu amefanya kwa mikono yake, Sauli aliungana naye kiasi cha kumpa si ruhusa ya kupambana na Goliati bali hata silaha zake na mavazi yake ya vita.
Sauli alimwambia Daudi, “HUWEZI WEWE KUMWENDEA MFILISTI HUYO NA KUMPIGA, MAANA WEWE U KIJANA MDOGO TU; NA HUYU NI MTU WA VITA TANGU UJANA WAKE”
(1Samweli 17:33).
Lakini alipojieleza na kushuhudia NINI MUNGU AMEFANYA KUPITIA MAISHA YAKE (1Samweli 17:34-37).
Sauli aliposikia SHUHUDA ZA DAUDI AKAACHA KUMPINGA AKAUNGANA NAYE.
“Sauli akamwambia Daudi, ENENDA, NA BWANA ATAKUWA PAMOJA NAWE”
Ukikutana na watu wanaokuambia HUWEZI usijibu kwa maneno matupu, wape shuhuda za nini Mungu amekufanyia.
Wakiyasikia matendo makuu ya Mungu wako, WATAKUUNGA MKONO NA HATA KUKUPA SILAHA ZAO UZITUMIE KUELEKEA USHINDI WAKO kama alivyofanya Sauli kwa Daudi!

3. SHUHUDA NI ROHO YA UNABII AMBAYO INAWEZA KUZAA MATOKE KAMA HAYOHAYO.

“Kwa maana USHUHUDA WA YESU NDIO ROHO YA UNABII”
(Ufunuo 19:10).
Shuhuda NI NENO LA MUNGU LILILOCHUKUA MWILI.
Shuhuda ni MANENO YA MUNGU YALIYOTHIBITIKA KATIKA MWILI WA NYAMA.
Watu wanaposhuhudia, na ukadaka huo ushuhuda, na ukaung’ang’ania bila kugeuka kulia wala kushoto, UTAPATA MATOKEO HAYOHAYO ALIYOPATA MSHUHUDIAJI MWINGINE ALIYETANGULIA.

Uzoefu wangu kuhusu hili;
Nilisoma ushuhuda wa Bishop David Oyedepo kuhusu binti mmoja aliyekwenda kwenye mtihani wake wa mwisho wa kumaliza chuo na alipopewa karatasi akakosa swali hata moja la kujibu.
Akachukua karatasi ya kujibia akaandika jina lake na kukusanya bila kuandika chochote.
Alipotoka akamfuata Bishop Oyedepo akiwa analia na kumwambia, “Baba, nimetoka chumba cha mtihani muda huu, nimeandika jina tu na sikujibu swali hata moja. LAKINI siko tayari kurudia mwaka, NATAKA UOMBE MATOKEO YA HUU MTIHANI NIFAULU YAKITOKA”
Bishop Oyedepo akasema hakuna tatizo, “Mungu amewahi kuandika AMRI KUMI KWA KIDOLE CHAKE/ CHANDA CHAKE” (Kutoka 31:18), hivyo nitakuombea na ATAANDIKA MAJIBU KWENYE KARATASI TUPU AMBAYO UMEKUSANYA maana Mungu anajua kila somo na ana majibu ya kila swali!
Akamwambia apige magoti, akaomba!
Matokeo yalipotoka, YULE BINTI ALIONGOZA KWA 98%… Kidole cha Mungu kiliandika kwenye karatasi tupu sawa na Ufunuo wa Neno aliotumia Bishop Oyedepo!

Siku moja binti yangu wa kiroho, S.K aliyehitimu degree yake ya sheria majuzi pale TUMAINI UNIVERSITY. Alinifuata akaniambia tangu aanze chuo hajawahi kumaliza semister bila supplimentary. Na kwenye mitihani yake ya mwisho ya kumaliza degree alikuwa na supplimentary mbili ambazo HAKUTAKA KWENDA KUZIFANYA. Alitaka niamini naye APATE DEGREE BILA KUFANYA SUPPLIMENTARY MBILI.

Nikakumbuka Ushuhuda wa Bishop Oyedepo na yule binti ambaye aliongoza kwa 98% bila kufanya mtihani kwa sababu Bishop aliomba “KIDOLE CHA MUNGU KIANDIKE KWENYE KARATASI TUPU” na mimi nikasema, “NITATUMIA ROHO YA UNABII ILIYOMO KWENYE USHUHUDA WA YULE BINTI NA LILE NENO LA KUTOKA 31:18, NA HUYU BINTI ATAHITIMU BILA KUFANYA SUPPLIMENTARY”
Tuliomba na ndicho kilichotokea!
Ana degree yake ya sheria sasa kwa utukufu wa Mungu!

Kwa leo tuishie hapa,
Umebarikiwa,
WEWE NI MTU MKUU, UMEBEBA MAJIBU YA WENGI NA VIZAZI VINGI!
Mwl D.C.K

Advertisements

Karibu kwenye Tovuti ya Kikristo... hapa utapata mafunzo Mbali mbali ya kukujenga kiimani ,kifahamu,kimazingira na hata kitabia Karibu Tena

Tagged with: , , ,
Posted in Mafunzo

Toa mawazo,maoni

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out / Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out / Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out / Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out / Change )

Connecting to %s

yaliyopita
Ungana nasi kwenye kurasa yetu  ya facebook na like page yetu-kuweza kutangaza neno la bwana na utabalikiwa sana..kwa kazi yako kuu kwani thawabu yako mbinguni ni tele

Andika E-mail kwenye box hapo chini kisha Bonyeza (jiunge Hapa)na uweze kujiunga na tovuti hii kupitia e-mail yako utakayojisajilia,tutaweza kukupa kila taarifa,habari zinazojili kwenye hii blog yetu asanteni

Join 2,215 other followers

Error: Twitter did not respond. Please wait a few minutes and refresh this page.

Upcoming Events

No upcoming events

%d bloggers like this: