SIKU 30 ZA MIUJIZA NA MAAJABU. (SIKU 30 ZA MFUNGO). [Day 24]

28/01/2016.https://i0.wp.com/static.wixstatic.com/media/837e29_3a9b1f58fbd34c00aa7904f4a75adf22.jpg

“UTENDAJI WA MALAIKA MAISHANI MWAKO (FUNCTIONALITY OF ANGELS IN YOUR LIFE)”

Kila mtu duniani amewahi kusikia kuhusu malaika.
Na karibu kila mtu anaamini kuhusu uwepo wa malaika.
Na kila anayeamini katika Mungu kwa dhati au kwa kubeep anaamini kuna malaika.

Somo hili limekujia kukusaidia kujua yafautayo;
i) Malaika ni nani?
ii)Malaika wa nuru na wa giza
iii) Kazi za malaika
iv) Mambo yatakayofanya malaika wawe upande wako
v)Namna ya kuwatumia malaika kukusaidia katika maisha

i)MALAIKA NI NANI?
Malaika ni ASKARI WATENDA KAZI wa Ufalme wa Mungu.
Mungu amewaamini na kuwapa uhalali wa kubeba jina lake, yaani kusimama kwa niaba ya Ufalme wa mbinguni (Kutoka 23:21).
Hawa ni Watenda kazi ambao hutenda na kutimiza kazi za Ufalme wa Mungu duniani.
Hawa hawaoi wala hawaolewi ( Mathayo 22:30).
Wanakaa uweponi mwa Mungu wakitenda kazi anazowatuma kuzifanya duniani.

ii) MALAIKA WA NURU NA MALAIKA WA GIZA

Biblia inatuambia kuna aina mbili za malaika, malaika wa nuru (Malaika walio chini ya Ufalme wa mbinguni), na malaika wa giza (ambao wako chini ya Ufalme wa giza)!

Wote hawa mwanzo walikuwa wamoja kwa mujibu wa Neno la Mungu.
Lakini kulitokea mkang’anyiko Shetani aliyekuwa mmoja kati ya MALAIKA WAKUU WATATU (wengine ni Mikaeli na Gabrieli), alipoanzisha mpango wa kumpindua Mungu na kuweza kuwashawishi THELUTHI (1/3) YA MALAIKA WA MUNGU kujiunga naye ili waweze kumpindua Mungu.
“Ikaonekana Ishara nyngine mbinguni; na tazama, joka kubwa jekundu, alikuwa na vichwa saba na pembe kumi, na juu ya vichwa vyake vilemba saba.
Na mkia wake WAKOKOTA THELUTHI YA NYOTA ZA MBINGUNI, na kuziangusha katika nchi (na kuwafanya watupwe duniani kwa kukubali kuasi naye)…” (Ufunuo 12:3-4).
Alipomaliza kuwapata THELUTHI YA MALAIKA waliunda jeshi ili wapigane na JESHI LA MALAIKA WATII WA MUNGU WALIOKUWA WAKIONGOZWA NA MIKAELI… Atukuzwe Mungu ya kwamba IBILISI NA MALAIKA ZAKE WA GIZA/ WAASI WALIPIGWA NA KUTUPWA TOKA MBINGUNI (Ufunuo 12:7-9).

Hawa Malaika wa giza walipofika huku “juu ya nchi” (duniani) walianza vita na mwanamke na uzao wake (Ufunuo 12:4).
Kazi ya hawa Malaika wa giza ni KUPAMBANA NA UZAO WA MWANAMKE (WANADAMU)!
Wanafanya kazi kubwa ya KUWADANGANYA WATU (Ufunuo 12:9).
Na ndio maana alipotupwa Ibilisi breki ya kwanza ilikuwa Edeni ili afanye KAZI YAKE YA KUDANGANYA. Na alifanikiwa.
Alipofanikiwa kumdanganya Adamu na mkewe, alifanikiwa kuudanganya na uzao wake!

Kazi yao nyingine ni “KUULA UZAO WA MWANAMKE” (Ufunuo 12:4).
Hawa malaika wa giza, hawana huruma na wewe mwanadamu.
Wana kazi ya kuhakikisha wanakula kila kilichozaliwa na uzao wa mwanamke.

Wanakaa wapi hawa malaika wa giza?
Wanakaa JUU YA NCHI NA WENGINE BAHARINI.
“Ole wa BAHARI NA NCHI maana yule Ibilisi ameshuka kwenu mwenye gadhabu nyingi, akijua ya kuwa ana wakati mchache tu”
(Ufunuo 12:12).
Wale wa NCHI KAVU tuna makundi kama; Mapepo (roho chafu zinazozurura zisizo na makazi maalum), mizimu (malaika wa giza wanaofanyiwa ibada za mila na desturi na wanadamu)… Wale wa BAHARINI wanaitwa MAJINI (wa majini)!
Hawa wana kazi kuu tatu;
Kuiba, kuchinja na kuharibu (Yohana 10:10)!
Na wanafanya kila wawezalo kuhakikisha wanaharibu maisha ya UZAO WA MWANAMKE!
Machafuko na uovu unaoendelea hapa duniani ni matokeo ya UTENDAJI KAZI WA JOKA NA MALAIKA ZAKE WA GIZA!

Lakini habari njema ni kwamba KUNA MALAIKA WA NURU WALIOBAKI WANAOMTII MUNGU ambao ni THELUTHI MBILI (kumbuka theluthi aliondoka nayo Ibilisi)!
Hivyo basi kimahesabu, “THELUTHI MBILI YA MALAIKA WA NURU” ni MARA MBILI YA “THELUTHI MOJA YA MALAIKA WA GIZA”
Hii ni kwamba, “Kwa kila malaika mmoja wa giza aliye kinyume chetu tuna malaika wawili wa nuru wa kumthibiti”
Hii ndiyo sababu mojawapo ya kutaka uwajue malaika wa nuru ili uwatumie KUDHIBITI NA KUHARIBU KAZI YA IBILISI NA MALAIKA ZAKE WA GIZA!

Namna ya kutofautisha Malaika wa nuru na malaika wa giza (pepo);
“MALAIKA WA GIZA WANAPENDA KUABUDIWA NA KUPEWA IBADA NA WATU BALI MALAIKA WA NURU HAWAKUBALI KAMWE KUABUDIWA, SIKU ZOTE WATAKUSISITIZA USIWASUJUDIE AU KUWAABUDU”
Ukiona malaika kaja kwako na anakwambia au anakubali kuabudiwa ujue una deal na pepo na si malaika!
Shetani alitaka Yesu amuabudu, na anaendelea kutafuta ibada toka kwa wanadamu (Luka 4:6-8).
Na hasa wanakuja na hilo kwa watafutao mali na utajiri.
Malaika wa nuru wanakukataza kuwaabudu (Ufunuo 19:10).
SHIKA SANA HII SIRI MAANA MALAIKA WANAWEZA KUKUTOKEA HATA WEWE UNAYESOMA UJUMBE HUU.

iii) KAZI ZA MALAIKA WA NURU.

1. Kuwaongoza watakatifu, kuwalinda na kuwapeleka mahali pa HATMA YAO MUNGU ALIPOWATENGENEZEA (Kutoka 23:20).

Ni vizuri ujue Mungu ana MIPANGO MAALUMU KWA AJILI YAKO (Yeremia 29:11 Biblia ya RSV).
Na hiyo mipango yake ina kila kitu bora Mungu alichokukusudia.
TAYARI MUNGU AMESHAKUTENGENEZEA.
Wewe hupajui lakini kuna MALAIKA MAALUM unao ambao ukikaa nao vizuri watahakikisha wanakufikisha kwenye KILA MUUJIZA WAKO MUNGU ALIOKUTENGENEZEA.
Hakuna sababu ya kukosa chochote ambacho Mungu alikutengenezea kabla ya misingi ya ulimwengu kuwepo maana kuna malaika wa kukupeleka huko miujiza yako na majibu yako yalipo.

2. Kuwalinda wacha Mungu na kuwaokoa na hatari na mabaya yote ambayo Ibilisi na watu waovu wamewakusudia.
(Zaburi 34:7, Zaburi 91:11-12).
*Wanahakikisha ulinzi wako kwenye kila jambo lako.
*Wanakuepusha na madhara yanayowapata wengine.
Kwenye Biblia waliwaokoa watakatifu wafuatao;
-Lutu kwa maombi ya Ibrahimu (Mwanzo 19).

-Danieli kwenye tundu la simba (Danieli 6).

-Petro gerezani (Matendo 12).
Hata wewe ukijielewa na kuwatumia watakusaidia.

3. Kuleta taarifa kwa watu wa Mungu.
Malaika huleta taarifa kwa watu wa Mungu kwa njia mbili;
Watu wakiwa macho (ukiwa macho unaona) na pili, ukiwa kwenye maono (kwa ndoto na maono ya wazi)!
Wafuatao kwenye Biblia waliletewa taarifa na malaika toka kwa BWANA;
-Yohana (Ufunuo 22:6).
-Manoa na mkewe (Waamuzi 13:1-22).
-Ibrahimu (Mwanzo 18).
-Yusufu (Mathayo 1).
-Kolnerio (Matendo 10).
Wako wengine wengi waliopewa taarifa na malaika kwenye Biblia.
Na wewe utaanza kupata taarifa toka kwa malaika kuanzia sasa katika jina la Yesu!

4. Kuwatumikia watakatifu.
(Waebrania 1:14, Ufunuo 19:10).
Ni haki yako kabisa wewe ULIYEOKOKA KUTUMIKIWA NA MALAIKA.
Malaika wanasubiri watakatifu muwatumie wawasaidie.

5. Kupeleka mapigo kwa watenda dhambi.
(Mwanzo 19, 2Wafalme 19:35, Isaya 37:36).
Mungu akitaka kushusha kipigo kwenye nyumba ya waovu, malaika ndio hutimiza hiyo kazi!
Epuka dhambi na uovu maana malaika watasimama kinyume chako na kukuadhibu badala ya kubeba baraka kukuletea.

iv) MAMBO YATAKAYOFANYA MALAIKA WA NURU WAWE UPANDE WAKO.

1. Lazima uwe umeokoka, lakini si kuokoka tu bali UNAUTUNZA USHUHUDA WA YESU (Ufunuo 19:10).
Lazima uwe barua bora inayomwakilisha Yesu (2Wakorintho 3:2-3).
Lazima uwe chumvi na nuru ya ulimwengu na watu wanamtukuza Mungu kupitia maisha yako (Mathayo 5:13-16).

2. Uwe unaliheshimu Neno la Mungu; Unalisikia, kulielewa na kulitunza.
Malaika hufanya kazi na washikao maelezo ya Neno la Mungu (Kutoka 23:20-23).

3. Jizoeze kulikiri Neno la Mungu kwa sauti; MALAIKA WA MUNGU HUPATA NGUVU YA KUTUSAIDIA PALE WAKISIKIA SAUTI YA NENO LA MUNGU TUNALOLITAMKA.
(Zaburi 103:20).
“Mhimidini Bwana, enyi malaika zake, ninyi mlio hodari, mtendao Neno lake, Mkiisikiza sauti ya Neno lake”
Angalia hilo andiko hapo juu na utajifunza yafuatayo;
-Malaika wanatenda NENO LA MUNGU
Hawatafanya na hawafanyi chochote nje ya Neno la Mungu.
Kadri unavyokuwa mtu wa Neno, unakuwa mtu wa kufaidi utendaji wa malaika.
-Malaika wanakuwa hodari WAKIISIKIA SAUTI YA NENO LAKE.
Jizoeze kulitamka Neno.
Sema unachokijua ili malaika wakutetee.
Usipojizoeza kutamka Neno ili malaika wasikie sauti ya Neno, utakosa utendaji wao.

Kwa leo tuishie hapa,
Umebarikiwa,
WEWE NI MTU MKUU, NI SHUJAA MKUBWA ULIYEBEBA URITHI WA VIZAZI VINGI!

Advertisements

Karibu kwenye Tovuti ya Kikristo... hapa utapata mafunzo Mbali mbali ya kukujenga kiimani ,kifahamu,kimazingira na hata kitabia Karibu Tena

Tagged with: , , ,
Posted in Mafunzo
One comment on “SIKU 30 ZA MIUJIZA NA MAAJABU. (SIKU 30 ZA MFUNGO). [Day 24]

Toa mawazo,maoni

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out / Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out / Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out / Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out / Change )

Connecting to %s

yaliyopita
Habari iliyotazamwa sana
Ungana nasi kwenye kurasa yetu  ya facebook na like page yetu-kuweza kutangaza neno la bwana na utabalikiwa sana..kwa kazi yako kuu kwani thawabu yako mbinguni ni tele

Andika E-mail kwenye box hapo chini kisha Bonyeza (jiunge Hapa)na uweze kujiunga na tovuti hii kupitia e-mail yako utakayojisajilia,tutaweza kukupa kila taarifa,habari zinazojili kwenye hii blog yetu asanteni

Join 2,215 other followers

Upcoming Events

No upcoming events

%d bloggers like this: