SIKU 30 ZA MIUJIZA NA MAAJABU. (SIKU 30 ZA MFUNGO).[Day 25]

29/01/2016.

“MKRISTO NI MTU WA KIWANGO CHA DUNIA (A CHRISTIAN IS A GLOBAL PERSONALITY)”

1. WATOTO WA MUUMBA NA MMILKI WA DUNIA NA ULIMWENGU.

“Nchi na vyote viijazavyo ni mali ya Bwana; DUNIA NA WOTE WAKAAO NDANI YAKE”
(Zaburi 24:1).

“Mbingu ni mali yako, nchi nayo ni mali yako, ULIMWENGU NA VYOTE VIUJAZAVYO, Ndiwe uliyeupiga msingi wake”
(Zaburi 89:11).

“Kama ningekuwa na njaa nisingekuambia? Maana ULIMWENGU NI WANGU, NAVYO VIUJAZAVYO”
(Zaburi 50:12).

Mungu aliye hai, Baba wa Bwana wetu Yesu Kristo ndiye anayemilki DUNIA na ULIMWENGU KWA UJUMLA WAKE.

Yesu alipotuokoa ametupa UWEZO WA KUWA WANA WA MUNGU.
(Yohana 1:12-13).

Pia Neno la Mungu limeeleza wazi ya kuwa sisi tu WARITHI, WARITHI WA MUNGU TUNAORITHI KILA ALICHONACHO TUKIWA PAMOJA NA KRISTO YESU (Warumi 8:16-17).

Mtume Yohana kipenzi cha Yesu naye alieleza kuhusu UTAMBULISHO WETU hata kama mazingira na wanadamu hawataki kukubali kuwa sisi NI WANA WA MUNGU, HAIBADILI CHOCHOTE MAANA NDIVYO TULIVYO.
(1Yohana 3:1-2).

Kwa maandiko haya machache umeona ya kuwa Baba yako wa mbinguni ndiye muumbaji na mmilki wa Ulimwengu na kupitia Wokovu tumefanyika watoto wa Baba ambaye NI MMILKI WA DUNIA NA ULIMWENGU.
Haiwezekani BABA AWE MMILKI WA ULIMWENGU halafu mwanae awe MMILKI WA FAMILIA AU MTAA.
Maana “Kama Yeye alivyo ndivyo tulivyo sisi ulimwenguni humu” (1Yohana 4:17).

Wewe ni mtoto wa muumba na mmilki wa Ulimwengu na dunia. Lazima dunia na ulimwengu ujue kwamba upo na umtambulishe Baba yako uliyembeba ndani yako (1Yohana 4:4).
Naamini ukidaka Ufunuo huu, UTAVUKA BORDER NA BORDER MPAKA YESU ANARUDI.
Utafika wasikofika wazazi wako, utakuwa na vitega uchumi nchi mbalimbali duniani kwa Utukufu wa Mungu.
NAKUSALIMU MTOTO WA MUUMBA NA MMILKI WA ULIMWENGU NA DUNIA!

2. CHUMVI YA DUNIA, NURU YA ULIMWENGU.

“Ninyi ni CHUMVI YA DUNIA…Ninyi ni NURU YA ULIMWENGU…”
(Mathayo 5:13-14).
Daka siri zifuatazo:
i) ..Ya dunia…ya ulimwengu
Yesu hakusema “ya kijiji” au “ya mji” au “ya wilaya au mkoa” au “ya taifa au bara moja” bali alisema NI YA DUNIA NA ULIMWENGU.
Yesu akisema wewe mwanafunzi wake ni wa kiwango cha DUNIA na kiwango cha ULIMWENGU hakuna wa kuzuia au kupinga, iko hivyo ni suala la wewe kuamini!

ii) CHUMVI NA NURU

Chumvi na nuru ni bidhaa zinazojulikana kote DUNIANI NA ULIMWENGUNI.
Hakuna mahali wasipoikubali chumvi au nuru.
Hakuna mahali ambapo chumvi na nuru havihitajiki.
Hakuna mahali ambapo chumvi na nuru vinakosa heshima.
Kokote kule, nchi yoyote ile, bara lolote lile, LINAHITAJI CHUMVI NA NURU.
Nuru na chumvi vinafanya ULIMWENGU uwe maana!
Ndiyo mapenzi ya Yesu kwako na kwangu; ANATAKA TUJITAMBUE KUWA SISI NI WA KIWANGO CHA DUNIA NA ULIMWENGU NA SI VINGINEVYO.
Usikubali kufia mkoani kwako, usikubali kuishia Tanzania, Afrika pekee haitoshi, DUNIA INAKUSUBIRI. Ulimwengu unakuulizia.
AMINI HILI NENO, USIKUBALI KUISHI CHINI YA HUU UNABII YESU ALIOTAMKA JUU YAKO.
“Wewe ni mtu wa kiwango cha dunia. Wewe ni mtu wa kiwango cha ulimwengu”
Dunia inasubiri ladha yako. Ulimwengu unangojea nuru yako.

3. HATA MIISHO YA NCHI.
“Nanyi mtakuwa MASHAHIDI WANGU….HATA MIISHO YA NCHI”
(Matendo 1:8).
Yesu amekuokoa tayari. Amekupa Roho wake mtakatifu. Amekupa Neno lake.
Amekujalia kuzijua siri za Ufalme wa mbinguni kuhusu kila eneo la maisha.
Hajakuokoa uishie kwenye Familia yako, kanisa lenu la mahali pamoja, dhehebu lenu, Tanzani na Afrika tu.
Hapana! Umeokolewa UWE SHAHIDI WA YESU KWENYE ENEO LA WITO WAKO KWA KIWANGO CHA MWISHO NCHI (The end Of the Earth)!
Usikubali kuwa mahali pamoja.
Hiyo huduma unayotoa Tanzania inahitajika nchi yoyote duniani.
Hiyo biashara unayofanya Tanzania inaweza kufanyika kokote ulimwengu.
Wanakusubiria wewe uwafikie. Wanakusubiria UWAPE USHAHIDI WA YALE MUNGU AMEWEKA NDANI YAKO.
Mipaka yako si Tanzania bali MIISHO YA NCHI.

4. WALE WALIOPINDUA ULIMWENGU WAMEFIKA NA HUKU.

“WATU HAWA WALIOUPINDUA ULIMWENGU wamefika huku nako”
(Matendo 17:6).
Hiki ndicho ninachokisikia kuhusu wewe ULIYEOKOKA.
Kuna nyakati zinakuja ambako WATU WA MATAIFA MBALIMBALI wataangalia makanisa uliyojenga, makampuni yako ulimwenguni kote, majengo uliyonunua au kujenga kila kona ya dunia, kisha watasema, “MTU HUYU ALIYEUPINDUA ULIMWENGU AMEFIKA NA HUKU NAKO”
Mimi sitakufa bila kuongelewa namna hiyo kila kona ya dunia.
Naamini hata wewe hutakubali unabii huu usiwe wa kwako.
“Wale tuliopindua si TANZANIA AU AFRIKA TU BALI ULIMWENGU tutafika kila mahali katika jina kuu la Yesu”
TUTAWEKA REKODI ZETU MPYA NA KUFUTA ZILIZOKUWEPO KATIKA JINA LA YESU.
SISI NI WAPINDUA ULIMWENGU; HUO UPAKO TUNAO NDANI YETU.
JIANDAE FURSA ZINAANZA KUJA BAADA YA KUDAKA UFUNUO HUU.
“You shall go places in Jesus’ name”

5. ULIMWENGU UTAKUTAFUTA UKIPATA HEKIMA YA MBINGUNI.

“ULIMWENGU WOTE UKAMTAFUTA SULEIMANI uso wake (umuone), ili WAISIKIE HEKIMA, MUNGU ALIYOTIA MOYONI MWAKE”
(1Wafalme 10:24).
Suleimani alitafutwa, Yesu alitafutwa, akina Paulo walitafutwa.
Na wewe utatafutwa na watu wa kila eneo kuona uso wako na kupokea vitu Mungu amekuwekea moyoni mwako.
Moyo wako una vitu umebeba vitakavyokufanya ULIMWENGU UKUTAFUTE.
Linda sana moyo wako na usafishe usichafuliwe na chochote kama unataka dunia ikutafute.
MUDA SI MREFU ULIMWENGU UTANITAFUTA.
Naamini nawe ukitendea kazi haya, Utatafutwa na WAFALME WA ULIMWENGU kama Sulemani (1Wafalme 4:34).
UTATAFUTWA ENDAPO UTATUNZA KILA HAZINA MUNGU AMEKUWEKEA MOYONI.

6. MALI ZAKO ZIKO ZAIDI YA TAIFA LAKO.

“Nitaihubiri amri; Bwana aliniambia, NDIWE MWANANGU, MIMI LEO NIMEKUZAA. Uniombe nami nitakupa MATAIFA KUWA URITHI WAKO, NA MIISHO YA DUNIA KUWA MILKI YAKO”
(Zaburi 2:7-8).
Hili andiko si la kila mtu. Ni andiko maalum kwa wale ambao MUNGU AMEWAZAA (WATOTO WA MUNGU: Yohana 1:12-13).
Hawa ndio ambao UTAJIRI WAO UKO KWENYE MATAIFA MBALIMBALI NA MILKI YAO NI MPAKA MIISHO YA NCHI.
Hii ni sababu tosha ya kumfanya Mtenda dhambi aokoke na kuzaliwa mara ya pili aingie kwenye kiwango hiki cha UTAJIRI WAKO KUWA KILA TAIFA NA KILA PEMBE YA DUNIA.

Tafakaria na hii:
“Na malango yako nayo yatakuwa wazi daima, hayatafungwa mchana na usiku; ILI WATU WAKULETEE UTAJIRI WA MATAIFA”
(Isaya 60:11).
Rafiki yangu ULIYEOKOKA hizi ahadi si kwa wasomi tu.
Si kwa wanaojua kiingereza tu.
Ni kwa wote waliookoka.
Ukishaokoka na ukaliamini NENO LA MUNGU….UTAKWENDA KILA MAHALI DUNIANI… UTAKUWA NA MALI KILA SEHEMU YA DUNIA!
Uhitaji kuwa fisadi ili uwekeze kila pembe ya dunia, unahitaji kuokoka na kuamini hizi siri nimekumegea!

WEWE NI MTU MKUU MWENYE MAJIBU YA DUNIA NZIMA!

Advertisements

Karibu kwenye Tovuti ya Kikristo... hapa utapata mafunzo Mbali mbali ya kukujenga kiimani ,kifahamu,kimazingira na hata kitabia Karibu Tena

Tagged with: , ,
Posted in Mafunzo
One comment on “SIKU 30 ZA MIUJIZA NA MAAJABU. (SIKU 30 ZA MFUNGO).[Day 25]
  1. EZEKIA Chuvaka says:

    Nashukuru,

Toa mawazo,maoni

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out / Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out / Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out / Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out / Change )

Connecting to %s

yaliyopita
Habari iliyotazamwa sana
  • None
Ungana nasi kwenye kurasa yetu  ya facebook na like page yetu-kuweza kutangaza neno la bwana na utabalikiwa sana..kwa kazi yako kuu kwani thawabu yako mbinguni ni tele

Andika E-mail kwenye box hapo chini kisha Bonyeza (jiunge Hapa)na uweze kujiunga na tovuti hii kupitia e-mail yako utakayojisajilia,tutaweza kukupa kila taarifa,habari zinazojili kwenye hii blog yetu asanteni

Join 2,219 other followers

Upcoming Events

No upcoming events

%d bloggers like this: