SIKU 30 ZA MIUJIZA NA MAAJABU. (SIKU 30 ZA MFUNGO). [Day26]

 

https://i0.wp.com/www.promisekeepers.org.nz/assets/images/wisechoices/handinrain.jpg

30/01/2016.

“BARAKA YA BWANA (THE BLESSING OF THE LORD)”

Nimekuwa nikisikia watu wakisema “Wahubiri wa kizazi hiki wanawahubiria watu baraka baraka baraka tuuuuu” …. Hii sentensi binafsi inanikera sana sana sana!
Watu kuhubiriwa au kufundishwa kuhusu baraka ni mpango kamili wa Mungu.

Katika somo hili nataka ujue kuwa baraka ni haki ya Muamini.
Na baraka ni kitu cha kutafuta na kung’ang’ania!
Usiiache baraka yako, baraka zinahitaji ufanye kitu ili kuzipata!

i) BARAKA NI NINI?
Baraka ni TAMKO LA MUNGU linaloambatana na nguvu ya kugeuza maisha ya mtu.
Inaweza kubadili kutofanikiwa, kutostawi, kutoongezeka, kuzaa mapooza na kukupa kinyume chake!
Daka hii:
“Kitu cha kwanza Mungu kumpa Mwanadamu bustanini Edeni ni Baraka, hivyo roho ya mtu inaijua baraka na ina kiu ya baraka ambayo huwezi kuizima bila baraka yenyewe”

Mwanzo 1:28 inasema:
“Mungu AKAWABARIKI, akasema zaeni mkaongezeke na kuijaza nchi”
Hii ndilo tukio la kwanza kabisa kwa Mungu kumfanyia mwanadamu alipoumbwa.
Hivyo huwezi kumzuia mtu kutaka na kutafuta baraka.
Baraka ni uwezo wa Mungu unaofanya mambo yawezekane mahali ambapo yalikuwa hayawezekani.
Baraka inaweza kubadili jangwa kuwa mto wa maji.
Baraka inaweza kubadili tumbo la tasa liwe tumbo lizaalo wakuu.
Baraka ni nguvu ya kiungu ya kubadili mambo katika namna chanya ya maongezeko na uzaaji.
Baraka lazima iongeze uzaaji na wingi wa kitu.
Kila palipo na baraka panaambatana na maongezeko na uzalishaji.
Baraka ni kinyume cha laana. Ni kinyume cha kukwama, nuksi, balaa na kuharibikiwa.
Kila palipo na baraka laana haina nguvu ya kufanya kazi kwa sababu sheria ya baraka ina nguvu kuliko sheria ya laana!

ii) BARAKA AU LAANA NI UCHAGUZI.

“Nazishuhudiza mbingu na nchi juu yenu hivi leo, kuwa nimekuwekea mbele yako uzima na mauti, BARAKA NA LAANA; basi chagua uzima, ili uwe hai, wewe na uzao wako”
(Kumbukumbu 30:19).
Kila mmoja wetu amewekewa mbele yake tayari baraka na laana.
Ni maamuzi yako kufanya mambo yatakayokufanya UBARIKIWE au kufanya mambo ambayo yatakupelekea ulaaniwe.
Ukiamua kuchagua LAANA usimsingizie Mungu.
Umewekewa mbele yako ili wewe kwa moyo, akili na maamuzi yako uchague kipi unataka!
BARAKA AU LAANA NI WEWE UNAYEAMUA KIPI UNAPOKEA KUPITIA MATENDO YAKO.
KILA UFANYALO LINAKUWA NA UPANDE WA BARAKA UKITENDA VEMA NA LAANA UKITENDA NJE YA NENO LA MUNGU!

iii) NAMNA YA KUPATA BARAKA YA MUNGU.

1. Ukitenda vema utapata mema.

Kama Mungu alivyomwambia Kaini, “Je ukitenda vema hutapata kibali?” Ndivyo ilivyo leo.
Mungu ataachili baraka kwa kila ALIYEBOFYA KITUFE SAHIHI CHA BARAKA.
Na ataachilia laana kwa ALIYEBOFYA KITUFE CHA UOVU.
(Mwanzo 4:3-7).

2. Ukiishi maisha ya haki, hautatafuta baraka, baraka itakukalia kichwani.
(Mithali 10:6).
Kila anayetembea kwenye haki, Mungu anamuwinda na vifurushi vya baraka.
MAISHA YA HAKI YANALIPA.
AMUA KUWA MTU WA HAKI, SIMAMIA HAKI HALAFU ACHA MUNGU AKUSHANGAZE KWA BARAKA.

3) Kujua kwamba Yesu ALIFUFULIWA NA KUTUMWA KWETU ILI ATUBARIKIE kwa kutuepusha kila mmoja na maovu yake.
(Matendo 3:26).

Kazi mojawapo ya Yesu baada ya kufufuliwa toka wafu ni KUTUBARIKIA SISI TULIO WAKE.
Hakuna sababu ya kukaa nje ya baraka ilhali unasema umeokoka.
Yesu wako amepewa kazi ya kukubarikia na kukusaidia utoke maovuni pia.

4) Yesu alipochinjwa na akashinda. Alipewa vitu saba kwa ajili yake kama kichwa na kwa ajili ya Mwili wake (kanisa). Mojawapo ya hivyo vitu ni BARAKA.
(Ufunuo 5:11-12).
Kama Yesu alikubali KUCHINJWA ili AKUCHUKULIE BARAKA kisheria. Hakuna haja ya kuishi bila baraka maishani mwako ilhali Mwokozi amekwishafanya kila kitu kwa ajili yako.
Mtukuze Yesu kwa kukuletea baraka.

5) Utii kwa Mungu na Neno lake na kulitenda.

“Itakuwa UTAKAPOISIKIA SAUTI YA BWANA, MUNGU WAKO, KWA BIDII, KUTUNZA NA KUFANYA MAAGIZO YAKE YOTE NIKUAGIZAYO LEO, ndipo Bwana, Mungu wako ATAKAPOKUTUKUZA JUU YA MATAIFA YOTE YA DUNIANI; Na BARAKA HIZI ZOTE ZITAKUJIA NA KUKUPATA USIKIAPO SAUTI YA BWANA, MUNGU WAKO. Utabarikiwa…. Utabarikiwa….”
(Kumbukumbu 28:1-14, Kumbukumbu 11:26-28).
Kama ukiliishi Neno la Mungu hautaweza kuiepuka baraka.
Baraka itakutafuta na kukupata.
LIHESHIMU NENO, LIISHI NENO, LITENDE NENO HALAFU BARAKA ZITAKUKALIA KICHWANI.

6) Utoaji wa zaka na sadaka.

“Leteni zaka kamili ghalani, ili kiwemo chakula katika nyumba yangu, MKANIJARIBU KWA NJIA HIYO, asema Bwana wa majeshi; MJUE KAMA SITAWAFUNGULIA MADIRISHA YA MBINGUNI, NA KUWAMWAGIENI BARAKA, hata isiwepo nafasi ya kutosha, au la” (Malaki 3:10).
Uamuzi ni wako kuziheshimu sadaka na hasa ZAKA ili upate kile alichoahidi Mungu kwako.
Baraka zinaisubiri dhabihu na zaka yako unayotoa kwa utiifu wa Neno la Mungu.

7) Heshima na mahusiano mazuri wazazi wako/ walezi.

“Waheshimu baba yako na mama yako; amri hii ndiyo amri ya kwanza yenye ahadi, UPATE HERI (UPATE BARAKA), ukae siku nyingi katika dunia”
(Waefeso 6:2-3).
Kuna baraka ya ajabu inayoambatana na maisha marefu ukiwa mahusiano mazuri na wazazi/ waliokulea.
Hii iko wazi.
Ukitaka kufa mapema cheza na mahusiano yako na wazazi na heshima yao.
Kama huna maelewano mazuri na wazazi/ walezi wako, KAWAANGUKIE. Katengeneze nao ili baraka zianze kukujia na kukupata.
Washirikishe baraka na mema Mungu aliyokupa.
Isaka alimbariki Yakobo kwa sababu ALIMPA CHAKULA AKIPENDACHO.
Tafuta kitu cha kujibarikia kwa mzazi/ mlezi wako.
Hata wakikosea shuka muyamalize kwa amani.

iv). NGUVU YA BARAKA

1) Baraka ya Mungu hutajirisha (Mithali 10:22).

Yakobo aliondoka nyumbani kwa baba yake tajiri sana Isaka (Mwanzo 26:13-14), AKIWA MIKONO MITUPU AKIMKIMBIA ESAU ASIMUUE (Mwanzo 27:41-45).
Akakimbilia nchi ya mbali akiwa na BARAKA ALIYOTAMKIWA NA BABA YAKE ISAKA (Mwanzo 27:27-33).
Matokeo: YAKOBO ALIRUDI AKIWA TAJIRI SANA.
HUWEZI KUWA NA BARAKA NA UKAWA MASIKINI.
UNAWEZA USIWE NA VITU VINAVYOONEKANA LAKINI KAMA UNA BARAKA NI SUALA LA MUDA DUNIA ITAJUA KWAMBA UPO!
“Baraka ya Mungu hutajirisha”

2) Baraka ya Mungu huleta utiisho (Mwanzo 26:12-14, 24-29).

Isaka akiwa na baraka ya Mungu alikuwa tajiri mkubwa kule Gerari.
Akiwa huko Mfalme Abimeleki na watu wa nchi ile walimuomba WASAINISHANE MKATABA asije akawapiga. Walimuogopa na kuona utiisho juu yake.
Baraka ya Mungu huleta utiisho.
Hauwezi kuwa umebeba baraka ya Mungu na watu wakakuchukulia poa.
Utiisho wa Mungu huambatana na waliobarikiwa (Kutoka 23:25,27).
Nakuombea ubarikiwe mpaka ifike mahali utisho uwe juu yako.

3) Baraka inazuia laana yoyote ikuguse (Hesabu 23:20).

Mchawi, mganga na hata mwanadamu anayejaribu “kumlaani aliyebarikiwa” anaishia kusema: “NIMLAANIJE YEYE AMBAYE MUNGU HAKUMLAANI?” (Hesabu 23:8).
Mungu mwenyewe anawafuata wanaojaribu “kuwalaani waliobarikiwa” na kuwaambia, “Usijaribu kumlaani huyu, tayari nimembariki”
MUNGU AKIKUBARIKI, HAKUNA WA KUKULAANI!

Kwa leo niishie hapa,
Umebarikiwa.
WEWE NI MTU MKUU NA ULIYEBEBA MAJIBU YA ULIMWENGU WAKO!

Advertisements

Karibu kwenye Tovuti ya Kikristo... hapa utapata mafunzo Mbali mbali ya kukujenga kiimani ,kifahamu,kimazingira na hata kitabia Karibu Tena

Tagged with: , , ,
Posted in Mafunzo

Toa mawazo,maoni

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out / Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out / Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out / Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out / Change )

Connecting to %s

yaliyopita
Ungana nasi kwenye kurasa yetu  ya facebook na like page yetu-kuweza kutangaza neno la bwana na utabalikiwa sana..kwa kazi yako kuu kwani thawabu yako mbinguni ni tele

Andika E-mail kwenye box hapo chini kisha Bonyeza (jiunge Hapa)na uweze kujiunga na tovuti hii kupitia e-mail yako utakayojisajilia,tutaweza kukupa kila taarifa,habari zinazojili kwenye hii blog yetu asanteni

Join 2,215 other followers

Upcoming Events

No upcoming events

%d bloggers like this: