SIKU 30 ZA MIUJIZA NA MAAJABU. (SIKU 30 ZA MFUNGO). [DAY29]

https://i0.wp.com/authorjimlynch.com/wp-content/uploads/2012/04/Walk-on-the-Beach.jpg

02/02/2016.

“HEKIMA YA KIMUNGU (DIVINE WISDOM)”

Hakuna mtu asiyetaka kuishi kwa urahisi hapa duniani.
Naamini kila mtu akipata dawa ya kula kwa jasho atamtukuza Mungu.
Na dawa hiyo ni HEKIMA YA KIUNGU.
Naomba usome hili somo kwa makini na umsihi BWANA mpaka upate matokeo.
Karibu tujifunze siri hii ya muhimu mno zaidi ya mno yenyewe.

Hekima hii inapatikana kwa njia zifuatazo:

1. Kwa kuiomba
(Yakobo 1:5-7).
Suleimani aliomba hekima na akapewa.
Usisahau Mungu hana upendeleo na hajabadilika.
Kikubwa uombe kwa imani.

2. Yesu Kristo tuliyenaye ndani yetu ni Hekima ya Mungu.
(1Kor 1:30).
Kama umeokoka tayari umekaa kwenye chanzo cha hekima hii ya ajabu ambacho ni YESU MWENYEWE.

3. Biblia inasema tukiokoka tunakuwa NDANI YA YESU (2Kor 5:17, Mdo 17:28), na humo ndani yake tulimo kuna HAZINA ZA HEKIMA NA MAARIFA (Kolosai 2:3).
Zidai leo maana unakaa katikati ya hizo hekima na maarifa zilizositirika ndani ya Kristo.

4. Muombe Mungu akuletee WENYE HEKIMA MAISHANI MWAKO watakaokufanya kuwa mwenye hekima (Mithali 13:20).
Lakini tayari tunao watumishi wa Mungu waliofanikiwa katika mambo mbalimbali ambao wana VITABU, VIDEO, YOUTUBE CHANNEL, WEBSITES nakadhalika, fuatilia mafundisho yao, UNAPOJILISHA MAFUNDISHO YAO, UNAJINOA KUWA KAMA WAO… Chuma hunoa chuma (Mithali 27:17).
Tenga muda kusoma mafundisho, biography za waliofanikiwa, website zao, vitabu, video na audio zao.
Halafu omba hicho ulichokisoma na kukiona kiwe halisi kwako, na kitakuwa.
You have something to do too to be wise!

5. Amua kumuomba Mungu akupe “ROHO YA HEKIMA, UFAHAMU NA MAARIFA” (Isaya 11:2).
Ukishakuwa MCHA MUNGU tu na ukatembea kwenye UCHA MUNGU KWA UAMINIFU WOTE bila hata kuomba HEKIMA YA MUNGU itaanza kuonekana waziwazi pamoja na AKILI ISIYOKUWA YA KIWANGO CHA KAWAIDA (Zaburi 111:10).

6. Tenga muda wa kutosha kukaa na MAANDIKO MATAKATIFU maana hayo yana uwezo wa KUKUPA HEKIMA NA KUKUFANYA MWENYE HEKIMA (2Timotheo 3:15).
Hakuna mtu aliyeamua kujichimbia na Biblia atakayekosa HEKIMA ITOKAYO JUU.
You can’t rub your mind with God’s mind and remain the same!

Kwanini leo tunaikazania HEKIMA YA MUNGU??

1. Inamfanya mtu AFANIKIWE KWA URAHISI katika kila eneo la maisha.
(Mhubiri 10:10).

2. Ukiwa na HEKIMA YA MUNGU utaumba chochote maishani mwako.
Maana hata Mungu hakutumia upako au mifungo na maombi kuumba vitu, bali alitumia HEKIMA.
Hekima inaweza kuumba chochote.
Ukiipata HEKIMA YA MUNGU tu umetoka jumla.
(Mithali 3:19).

3. Ukiwa na HEKIMA hii ya Mungu utakuwa TAJIRI.
(Zaburi 104:24, Mithali 3:13-16).

4. Hekima hii ya ajabu itakupa uhakika wa kushinda kila mshindani na kila vita mbele yako.
( Matendo 6:9-10, Luka 21:15).

5. Hekima ya Mungu itakuhamisha daraja na kiwango cha maisha ulichopo kukupeleka mahali ambapo waliokujua wataishia kujiuliza NINI KIMEKUPATA!
(Marko 6:2, Matendo 4:13).

6. Hekima ya Mungu ni ULINZI KWAKE aliye nayo (Mhubiri 7:12).

7. Hekima humfanya aliyonayo awe na NGUVU YA ZIADA kuliko wanadamu wasio nayo.
(Mithali 24:5).

8. Ukiwa na hekima ya Kimungu utakuwa kama sumaku.
Utawavuta watu kuja kukusikia na kuona kazi uzifanyazo na yale Mungu aliyotia moyoni mwako.
(1Wafalme 10:24).

Nadhani umeona ni kwa kiasi gani HEKIMA YA MUNGU ni kila kitu.

Ni prayer point ya leo, LAKINI OMBA MPAKA UTAKAPOONA UMEANZA kutembea katika HEKIMA hii ya ajabu.
Usiishie leo tu.
Tumia njia zote za kupata hekima nilizokupa.

Tuishie hapa kwa leo,
WEWE NI MWENYE HEKIMA ILIYOPITILIZA, NA MTU WA AJABU KWA DUNIA YAKO.

Advertisements

Karibu kwenye Tovuti ya Kikristo... hapa utapata mafunzo Mbali mbali ya kukujenga kiimani ,kifahamu,kimazingira na hata kitabia Karibu Tena

Tagged with: , ,
Posted in Mafunzo

Toa mawazo,maoni

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out / Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out / Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out / Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out / Change )

Connecting to %s

yaliyopita
Habari iliyotazamwa sana
Ungana nasi kwenye kurasa yetu  ya facebook na like page yetu-kuweza kutangaza neno la bwana na utabalikiwa sana..kwa kazi yako kuu kwani thawabu yako mbinguni ni tele

Andika E-mail kwenye box hapo chini kisha Bonyeza (jiunge Hapa)na uweze kujiunga na tovuti hii kupitia e-mail yako utakayojisajilia,tutaweza kukupa kila taarifa,habari zinazojili kwenye hii blog yetu asanteni

Join 2,215 other followers

Upcoming Events

No upcoming events

%d bloggers like this: