SIKU 30 ZA MIUJIZA NA MAAJABU. (SIKU 30 ZA MFUNGO)[Day 30]

https://i2.wp.com/www.youthvillage.co.za/wp-content/uploads/2015/04/Youth-Oppotunities-400x230.png

03/02/2016.

“KIWANGO HALISI CHA MUNGU ANACHOTAKA UISHI (THE REAL LIFE GOD DESIRES FOR YOU)”

NENO KUU:

** MATHAYO 6:25-30.

25 Kwa sababu hiyo nawaambieni, Msisumbukie maisha yenu, mle nini au mnywe nini; wala miili yenu, mvae nini. Maisha je! Si zaidi ya chakula, na mwili zaidi ya mavazi?

26 Waangalieni ndege wa angani, ya kwamba hawapandi, wala hawavuni, wala hawakusanyi ghalani; na Baba yenu wa mbinguni huwalisha hao. Ninyi je! Si bora kupita hao?

27 Ni yupi kwenu ambaye akijisumbua aweza kujiongeza kimo chake hata mkono mmoja?

28 Na mavazi, ya nini kuyasumbukia? Fikirini maua ya mashamba, jinsi yameavyo; hayafanyi kazi, wala hayasokoti

29 nami nawaambia, ya kwamba hata Sulemani katika fahari yake yote hakuvikwa vizuri kama mojawapo la hayo.

30 Basi, ikiwa Mungu huyavika hivi majani ya kondeni, yaliyopo leo, na kesho hutupwa kalibuni, je! Hatazidi sana kuwavika ninyi, enyi wa imani haba?

:UTANGULIZI:

Kuna watu wanaishi maisha yasiyokuwa yao maana Mungu hakuwapangia waishi hivyo. Hii husababishwa na Kuonewa na shetani au kukosa maarifa.

Shetani huharibu maisha ya mtu kwa kumuibia, kumharibia na kuchinja/ kuua mambo katika maisha ya mtu (Yohana 10:10).

Lakini kuna walio na maisha duni na ya ovyo ambayo Mungu hakuwakusudia kwa vile tu hawana maarifa.
Bila maarifa sahihi katika maeneo yote huwezi kutoka hata kama Shetani atakuacha bila kukusumbua.
“Kwa maarifa nyumba hujaa vitu vya thamani na vya kupendeza”
(Mithali 24:3-4).
Bila maarifa huwezi kuishu maisha ya kupendeza na bora.
Maarifa ni taarifa sahihi toka kwenye Neno la Mungu.
Kama hauna taarifa sahihi/ kanuni za Ufalme utaishi colourless life!

*Yoh 10:10.. “Yesu alikuja ili tuwe na Uzima tena Uzima tele”
Kiingereza inasema;

“He came so that we can have life and life in its abundance ”

Yaani “Yesu alikuja ili tuwe na maisha katika ubora wake”

UFANYEJE ILI KUFANIKIWA KUISHI MAISHA MUNGU ANAYOTAKA UISHI SAWASAWA NA NENO KUU KUTOKA MATHAYO 6:25-30?

KANUNI SABA ZA KUJIFUÑZA:

1. “Usiyasumbukie maisha.”

Katika mstari wa 25, tunaona kauli hii;

“Msiyasumbukie maisha yenu”

Hiii ni kauli ya Yesu, si ya Paulo, Petro au Yohana au DCK.
Ni kauli ya aliyesema “maneno yake hayatapita kamwe” maana yake “maneno yake ni eternal principle” na ni kanuni isiyopitwa na wakati wala haibadiliki kwa sababu ya teknolojia wala maendeleo.
Yesu anaposema tusisumbukie maisha, anatuambia si mapenzi ya Mungu kwa wanafunzi wake, watoto wa Mungu kusumbuka katika maisha.
Yesu anasema kuna uwezekano wa kuishi “friction free life”
Kama Yesu kasema kwanini usiamini?
Kwanini usiipokee hii kanuni?

Angalia hii:

Kusumbukia maisha sio sawa na kujishughulisha na maisha.
Kusumbuka ni kutumia akili na nguvu zako zote na kutegemea hizo kufanikiwa, na kujishughulisha ni kufanya unachotakiwa kufanya na kumuachia Mungu nafasi ya kukusaidia kupata matokeo makubwa na bora.
You are not a hustler but a worker.
Mungu hataki u-hustle bali anataka ufanye kazi.

Usisumbukie maisha maana duniani sio mahali pako ila mbinguni, uko duniani kwa kusudi maalumu kwa muda maalumu.

Kuishi kwako duniani kusikufanye utende kama watu wa duniani, kama wanasumbuka acha wasumbuke wao (walio nje ya Ufalme wa Mungu) ila kusumbuka si fungu lako.
Ingawa Kuku na tai wote ni ndege lakini wana tofauti , tai anaruka na kuku haruki, you are an eagle not a chicken!

**Mungu anasemaje kuhusu kusumbuka?**

*1Peter 5:7
Huku mkimtwika yeye fadhaa zenu zote, kwa maana yeye hujishughulisha sana kwa mambo yenu.

Kama Mungu anajishughulisha sana na mambo yako huna haja ya kusumbuka

*1Yoh 4:4.
Aliye Ndani yako ni mkuu kuliko aliye katika dunia hii.
Mpe nafasi akupe ushindi.

*Math 11:28
Yesu anataka akupumzishe na mizigo yote inayokusumbua.
Yesu anataka upumzike, yeye afanye kila jambo “nyuma ya pazia” kwa niaba yako.

* Filipi 4:6-7
Usisumbukie neno lolote bali katika kusali,kuomba pamoja na kushukuru.

Kinachotakiwa ni kutunza uwepo wa Mungu kwako tu maana ufalme wa Mungu uko Ndani yako kama umeokoka (Luka 17:20-21, Mdo 17:28).

Roho Mtakatifu aliletwa kwako kama msaidizi (Yohana 14:16), version nyingine ya Biblia ya kiingereza (KJV) inamuita comforter ,kazi ya comforter ni kufanya uishi comfortable life and not otherwise.
Holy spirit is a maker of a comfortable life.

Unapotumia na kuamini nguvu zako huthamini nguvu za Mungu Ndani yako yani Roho Mtakatifu.
Be smart, let Him work for you and through you!

**Smartness is more important than hard work , work smart not hard.

2. “Omba hekima ya kukusaidia kuweka vipaumbele katika maisha yako”

Usifanye vitu visivyo na umuhimu kuwa na umuhimu ..mstari wa 26 Mungu anaonesha vipaumbele:
“kwamba maisha ni bora kuliko chakula”;
“na mwili ni bora kuliko mavazi”

Kwenye dunia yetu ya sasa watu wanafeli maisha kwakuwa hawana vipaumbele.
Wengi wako tayari kuhatarisha maisha ili wapate chakula.
Wengine wanauza miili ili wapate mavazi.
Huku ni kutokuwa na vipaumbele.
Na kama huna vipaumbele, huwezi kufanya kazi na Mungu.
God is God of priorities!
Aliumba resources kabla ya kuumba mtu.
Aliumba maji kabla ya samaki.
Aliumba miche na mimea kwanza kabla ya wanyama.
Aliumba kwanza nchi kabla ya mimea.
Hii ndiyo uwekaji wa vipaumbele kwa usahihi.
Si kila kitu sahihi au bora ni lazima ukifanye kwanza, vitu vinazidiana umuhimu na ulazima.

Kwenye maisha utafika mahali pa kulazimika kuwa na vipaumbele kama unataka mafanikio na ustawi.

Fikiri unapata kazi ambayo inakulazimu kuwa kazini hadi siku ya ibada/ muda wa ibada… Hapa itabidi uamue kàti ya kazi na Uhusiano wako na Mungu!
Kama ni “pesa mbele” utachagua kazi… Kama ni “kingdom minded” utakuwa radhi kuipoteza hiyo kazi ili ubaki na muda wako na Mungu.
Hapa lazima tuone kipaumbele chako.

Daniel katika Daniel 6 , walikosa cha kumshtaki wakaamua kutumia mambo yake na Mungu wake,ndo maana wakapanga kumkataza kumuabudu Mungu wake lakini Daniel alijua kipaumbele chake ndo maana bado alizidi kumuabudu Mungu tena huku madirisha yakiwa wazi Mara tatu kwa siku ( kuanzia leo anza utaratibu wa maombi ya Mara tatu kwa siku hata kama uko kazini tenga muda kidogo wa lunch nk. Na maisha yako yatabadilika )

*Mtu wa Mungu unaweza kutegwa na kazi unayofanya inakufanya kukosa muda na Mungu wako..kwa mfano kazi hadi jumapili, au siku za wiki baada ya kazi muda unaotakiwa kwenda kwenye ibada au Huduma unakuwa offered over time payment ubaki ufanye kazi. Omba hekima ya Mungu ikusaidie kutambua kipaumbele kama ni Mungu kukubadilishia kazi nk.

3. “Sio kila kitu ambacho unakivuna katika maisha yako umekipanda/ unaweza kuvuna usipopanda”

*Katika maisha kuna kanuni mbili: “moja ya kupanda na kuvuna”
(Wagalatia 6:7-8, Luka 6:38), nyingine ni kanuni ya “kuvuna bila kupanda” (Mathayo 25:24, 26).
Mstari wa 26, Mungu asingetoa mfano wa ndege kama hakuna kuvuna bila kupanda.
(Ndege huvuna wasipopanda… Yesu alitaka tujue kuwa anaweza kukupa vitu ambavyo hujavipanda kama afanyavyo kwa ndege!

Inategemea tu ushirika wako mzuri na Mungu.
(Ndege wanaji-position kwenye namna ya maisha aliyowaumbia, na wanavuna bila kupanda)!

Kwa msaada wa Mungu tunatenda mambo makuu (Zab.60:12).

4. “Thamani yako mbele za Mungu tangu ulipompokea Yesu ni kigezo tosha cha kukufanya upokee mambo makuu na mazuri toka kwa Mungu”

Tumeona kuwa “Baba yetu wa mbinguni” ndiye alishaye ndege wa angani (mstari wa 26).
Halafu Yesu anauliza, “kama Mungu ambaye ni Baba yenu anatunza ndege ambao si wanae kisheria, Je si zaidi ninyi?”

Baba yako wa mbinguni (Mungu) yuko tayari kukupa wewe chochote maana thamano yako ni kubwa na bora kuliko ya chochote.
Aligharamika kutoa damu ya mwanae wa pekee, iliyo ya thamani mno kuliko fedha na kuliko dhahabu (1Petro 1:18-19); Kama alitumia vilivyo bora zaidi ya fedha na zaidi ya dhahabu kukununua, ataachaje kukupa na hayo (fedha na dhahabu) pia? (Warumi 8:32).
Ataachaje kukupa mavazi na chakula?
Ataachaje kukupa mme/ mke bora?
Ataachaje kukufanya mtu mkuu?
*Wewe ni bora kuliko ndege*

*Watu wote ni wa Mungu lakini wachache ni wana wa Mungu.
* Ndo maana tunaita Abba yani baba (Yoh 1:12).

*Math 7:7-10

“Aombaye hupokea”
(Mathayo 7:8), hivyo baada ya maombi kuwa na furaha na mshukuru Mungu maana umepokea ulichoomba (Marko 11:24).
Baba yetu wa mbinguni yuko tàyari kutupa chochote kuliko baba zetu wa mwilini (Mathayo 7:10).
Omba Mungu alete Mvua unapoona Neno lake ambalo ndilo wingu lako.
(Eliya alipoona wingu kama mkono alijua inafuata mvua kubwa. Unapoliona Neno la Mungu kuhusu jambo lolote, hilo ndilo wingu lako, ingia nalo kwenye maombi kudai mvua kubwa)!

5. “Kuna Mungu anayeshughulika sana na mambo ya mtu mmoja mmoja”

Mstari wa 27, “Ni yupi kati yenu akijisumbua aweza kuongeza kimo chake hata kwa mkono?”…
Mungu anashughulikaga na mtu mmoja mmoja, ndio maana Mungu akasema “kimo chake” sio “vimo vyenu”.

* Hab 2:4 mwenye haki huishi kwa imani yake.
(Imani yake na si imani zenu).
Unahitaji kutengeneza imani “yako binafsi” kwa kila jambo la maisha yako!

*Zab 91:7-8 Mungu husema na mtu mmoja.
Wataanguka “mkono wako” (si mikono yenu)… Ni ahadi kwa mtu mmoja binafsi.
Kuna Mungu anayekutazama wewe kama wewe… Aliyekuumba na kukuza mwili wako kivyako… Alijishughulisha na wewe ukiwa peke yako.
* Mungu alikuumba
* Alikuza viungo vyako bila hata maombi
* Anakupa hewa wewe kama wewe
(Kwa ufupi Mungu anajishughulisha na maisha yako wewe kama wewe… Usijaribu kuyafanya maisha yako kuwa general… Mungu hufanya kazi na mtu mmoja mmoja kati ya wote walioko… Kama unataka kuona matokeo: Yatazame maisha kama vile ni wewe tu uliyeko na Mungu anakupa attention ya 24/7).
“Personalize your life”

6. “Sio kila kitu unachokipata kwenye maisha ni kwa sababu umekifanyia kazi”

.Usimuwekee Mungu mpaka wa kukupa usivyofanyia kazi, iko hiyo fursa.
.Mungu yuko tayari kukupa yale usiyofanyia kazi.
. Yesu asingetoa mfano wa maua na yanavyopata benefit bila kufanya kazi kama hana system ya kumfanya mtoto wake naye apate bila kufanya kazi (mstari28).

Yoshua 24:11-13.

13 Nami nimewapa ninyi nchi msiyoitendea kazi, na miji msiyoijenga, nanyi mmekaa humo; mnakula matunda ya mashamba ya mizabibu na mizeituni msiyoipanda.
Mungu yuko tayari “kutia yote uyatakayo mikononi mwako” bila wewe kupigana kwa mshale wala upanga wako (Yoshua 24:11-12).

7. “Mungu anahitaji imani yoyote toka kwako ili apate kufanya mambo makuu”
“Je si zaidi ninyi enyi WA IMANI HABA?”
(Math 6:30).
Haijalishi kiwango cha imani uliyonayo mbele za Mungu.
Ukiwa na imani ndogo sana unaweza kupata matokeo yoyote makubwa na ya kushangaza (Mathayo 17:20).
Itunze imani yako, ni kiwanda chako cha miujiza.
Yuda 1:3
“Ishindanie Imani yako”
Warumi 12:3
“Mungu amemgawia kila mmoja kiasi cha imani”
Itumie hiyo imani, usiiache tu mfukoni.
1 Petro 1:23.
“Neno la Mungu ulilopewa, litumie ni mbegu ya kuzaa miujiza isiyoharibika”

PROPHETIC DECLARATION FOR FEBRUARY.
(TAMKO LA KINABII KWA MWEZI FEBRUARI)!

“THE MONTH OF POWER”

*Everything you want shall answer to God’s power in you (Ephesians 3:20).
“The power of God in you shall work wonders for you”

* The prosperity power shall dominate your life from now on (Deutronomy 8:18).
“I prophecy, you shall not lack grace and power to be prosperous and great”

Luke 10:19.
*The Lord has given you power over each and every demonic and satanic forces.
No power of darkness shall be able to stop you.
By His power you are going to arrest and torment darkness!

John 1:12
*The Lord has given you power to become greater.
*Jesus is giving you power to become greater !
* Mbali na unyanyasaji wa shetani.
“Receive His Power to become successful like your heavenly father”

* Nguvu ya kukutangaza kila mahali (Luke 4:14).

Habari za Yesu zilienea kwa sababu ya nguvu.
Nguvu ya Mungu imeachiliwa ili kusambaza habari zako na taarifa zako.
Mungu mwenyewe atakufanyia promotion.

Nguvu za Mungu zitadhihirika kwenye kila jambo lako mwezi huu wa February.
Huu ni MWEZI WA NGUVU.

Utukufu umrudie Bwana Yesu aliyetusaidia na kutuwezesha.
Hatmaye tumemaliza leo siku 30 za Mfungo.

KILA ULIYESHIRIKI KUOMBA NA KUFUNGA SIKU HIZI 30, MAISHA YAKO HAYATAKUWA YALIVYOKUWA!

Advertisements

Karibu kwenye Tovuti ya Kikristo... hapa utapata mafunzo Mbali mbali ya kukujenga kiimani ,kifahamu,kimazingira na hata kitabia Karibu Tena

Tagged with: , ,
Posted in Mafunzo
One comment on “SIKU 30 ZA MIUJIZA NA MAAJABU. (SIKU 30 ZA MFUNGO)[Day 30]
  1. emanuel bike says:

    Somo zuri sana mtumishi Mungu akubariki,akuongezee hekima na maarifa ili uzid kufanya meng mazuri ya kumpendeza yeye

Toa mawazo,maoni

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out / Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out / Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out / Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out / Change )

Connecting to %s

yaliyopita
Habari iliyotazamwa sana
  • None
Ungana nasi kwenye kurasa yetu  ya facebook na like page yetu-kuweza kutangaza neno la bwana na utabalikiwa sana..kwa kazi yako kuu kwani thawabu yako mbinguni ni tele

Andika E-mail kwenye box hapo chini kisha Bonyeza (jiunge Hapa)na uweze kujiunga na tovuti hii kupitia e-mail yako utakayojisajilia,tutaweza kukupa kila taarifa,habari zinazojili kwenye hii blog yetu asanteni

Join 2,219 other followers

Upcoming Events

No upcoming events

%d bloggers like this: