BABA WA KIROHO

(UKWELI KUHUSU BABA WA KIROHO)

1. Si kila aliyekuongoza “sala ya toba” ni baba wa kiroho.
Baba wa kiroho ni yule anayekulisha (anayekufanya ukue na usife kiroho), anakufanya umjue Mungu, ujue siri za Ufalme wa Mungu, na utembee ndani yake!
“Na kondoo zangu wanaijua sauti yangu”
(Yesu katika Yohana 10).
Ni mtu ambaye “sauti yake” inaeleweka kwako, na ina nguvu moyoni na maishani mwako!
Hata ukiwa mahali pa kukosea au kutenda yasiyo sawa, akilini mwako ukikumbuka somo lake au maonyo yake, unaghairi na kuahirisha, hata kama hayupo.
Sauti yake iko hai ndani yako hata asipokuwa nawe.
Mafundisho yake yako hai hata kama hayupo ulipo.

2. Mtu hawi baba wa kiroho kwa kukuombea ukaponywa au kufunguliwa.
“Waliponywa wengi wakati wa Yesu, walifunguliwa na kutendewa miujiza wengi… Lakini alipofufuka alikuwa na watoto wa kiroho 120 waliobaki CHUMBA CHA JUU hadi siku ya pentekoste… Japo alilisha wanaume zaidi ya 5000, bila kuhesabu wanawake na watoto, na makundi ya maelfu yalimfuata… Lakini alikuwa na watoto 120 tu waliokuwa wakitii MAELEKEZO YAKE NA KUFANYA ALICHOWAAGIZA (kukaa ghorofani mpaka wavikwe uweza)”
Idadi kubwa ya wanaokufuata, wanaofurahia mafundisho yako, walioponywa, waliotendewa miujiza na wewe, isikupotoshe ukadhani ni wanao wa kiroho!

3. Baba wa kiroho ni yule mtu ambaye “hachoshwi” na mapungufu, makosa, na matatizo yako, bali anaamini “UNA HAZINA KUBWA (He believes in you and your God given potentials)”
Petro ni mfano halisi wa Ubaba unavyotakiwa kuwa.
Ali-mess up mara nyingi sana, lakini Yesu alimwambia, “NINAKUOMBEA UKISHAVUKA UTAWAIMARISHA WENZAKO” … Badala ya kumtenga alimwambia, “JUU YAKO NA UFUNUO HUU ULIOTOA NITALIJENGA KANISA LANGU WALA MALANGO YA KUZIMU HAYATALISHINDA”
(Mathayo 16).
Bado alipokamatwa “ALIMKANA MARA TATU” lakini alipofufuka, mtu wa kwanza kumtaja alikuwa Petro… Alisema, “Enenda ukawaambie wote pamoja na PETRO kuwa nawatangulia Galilaya”
Baba hamchoki mwana… Kama umechokwa, jua hakika hapo ulipo umekosea, huyo si baba yako!
Si mnakumbuka HABARI YA MWANAMPOTEVU (Luka 15)?
Baba hakumchoka mwanae mbali ya kukiuka utaratibu na kutoka nje ya “mfumo wa familia”… Aliporudi, BABA ALIKUWA WA KWANZA KUKIMBIA KUMLAKI MWANA MPOTEVU… Ikiwa na maana Baba wa kiroho hawezi kutulia na kukaa na amani ilhali hamuoni mwanae… Je, wewe huyo Baba yako anajali asipokuona? Anajali akiona kiroho chako kimeyumba na unapotea nje ya imani?
Anakutenga au usingizi unamuisha mpaka aone umerudi?
Baba wa kiroho huamini katika wewe no matter what happens!
“Yesu alikaa na Yuda na alijua anamuibia na ajenda mbaya dhidi yake lakini hakumfukuza… Aliamini ana kitu… Aliamini atazaa matunda… Japo haikuwa hivyo”

4. Baba wa kiroho ana muda (hutengeneza muda kwa ajili ya wanae hata kama unabana kiasi gani);
“Asiyewatunza wa kwake hasa wale wa nyumbani kwake ni mbaya kuliko asiyeamini na ameikana imani”
(1Timotheo 5:8).
Makusanyiko ya kiroho ni FAMILIA ZA KIROHO.
Baba yeyote anakuwa na muda na wale wa nyumbani kwake.
Hauwezi kumwambia kitu au jambo halafu akasema yuko “busy” anajua wewe ni sehemu ya familia yake, ni sehemu ya utumishi wake, anawajibika kwako na atakutolea hesabu mbele za Mungu.
Kama hana muda kwa ajili yako ni baba wa namna gani huyu?
Biblia inasema Yesu alikuwa na “general message” (mahubiri ya jumla) kwa ajili ya makutano, lakini alikuwa na “private time” ya kuchanganua message kwa wanafunzi wake.
A father must have time for His children.

5. Baba wa kiroho lazima awe na kile unachokitaka ili ufanikiwe.
Ni makosa ya aina yake kwa kinda la mwewe kujichanganya na vifaranga vya kuku.
Sikia hii:
Siku moja Yesu alipiga injili ngumu kidogo na watu wakatawanyika na kuondoka/ wakasusia huduma yake… Wakawa wamebaki wanafunzi wake tu, akawageukia na kuwauliza, “Na ninyi mnataka kuondoka kama hawa?”
Petro akajibu kwa niaba ya wengine:
“Twende wapi? Kwako kuna maneno ya uzima”
Akiwa na maana:
“Tumekuchunguza sana, tumekuelewa sana… Tunajua tunachokihitaji kutupeleka NEXT LEVEL kiko kwako, twende wapi tuache PACKAGE zetu?”
Nisikilize:
Kama hana kile unachohitaji kukupeleka unakotaka kufika kiroho, achana naye.
“Wanafunzi wa Yohana walipomuona Yesu, na wakajua ana kile ambacho wanakitafuta, walimuacha wakamfuata Yesu”
(Yohana 1:35-39).
Usikae mahali ambapo ukiangalia kile unachokitafuta hakiko pale.
Mfano:
Unataka kuwa tajiri halafu mtumishi uliye naye anapinga masuala ya utajiri na mafanikio… Unapoteza muda hapo!
Unataka kuwa kiongozi mkubwa na mleta mageuzi; Halafu huyo mtumishi uliye chini yake hana hata team ya uongozi anayoiongoza (hana leadership structure)… Yeye ni kila kitu na anafanya yote… Hapa hapakufai!
Unaamini katika ishara, maajabu na miujiza na unataka Mungu akutumie kwa viwango vya ajabu… Lakini huyo uliye chini yake anapinga masuala ya miujiza, ishara na maajabu kiasi cha kusimama madhabahuni kupinga au kuwasema watumishi wanaotenda miujiza, ishara na maajabu, hakika hapo si kwako… Umechanganya!
Mfano unaamini kwenye utajiri:

Hakikisha baba yako wa kiroho naye ni mtu anayeamini katika utajiri.

Note:
Anaweza asiwe tajiri wa vitu bado, LAKINI anaamini katika utajiri, anafundisha kuhusu utajiri, anauzungumza utajiri na kuukataa umasikini, anaamini kwenye utele, mafanikio na anatarajia hayo tu na si upande wa pili.
Huyu ni mtu sahihi… Ni tajiri ambaye anasubiri muda tu utajiri uonekane nje!
Baba lazima awe na unachokitaka… Kwenye lugha yake… Kwenye mafundisho yake… Kwenye matarajio yake nakadhalika!

Nitaendelea….

Karibu kwenye Tovuti ya Kikristo... hapa utapata mafunzo Mbali mbali ya kukujenga kiimani ,kifahamu,kimazingira na hata kitabia Karibu Tena

Tagged with: , ,
Posted in Mafunzo

Toa mawazo,maoni

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out / Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out / Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out / Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out / Change )

Connecting to %s

yaliyopita
Ungana nasi kwenye kurasa yetu  ya facebook na like page yetu-kuweza kutangaza neno la bwana na utabalikiwa sana..kwa kazi yako kuu kwani thawabu yako mbinguni ni tele

Andika E-mail kwenye box hapo chini kisha Bonyeza (jiunge Hapa)na uweze kujiunga na tovuti hii kupitia e-mail yako utakayojisajilia,tutaweza kukupa kila taarifa,habari zinazojili kwenye hii blog yetu asanteni

Join 2,217 other followers

Upcoming Events

No upcoming events

%d bloggers like this: