MAMBO YA LAZIMA KUFANYA

KAMA UNATAKA DUNIA ITAMBUE UWEPO WAKO KABLA HUJAONDOKA DUNIANI.

https://farm2.staticflickr.com/1028/846890548_d4d8b5c4a8_z.jpg

1. Lazima uwe na muda wa kuongea na Mungu kupitia maombi, walau mara tatu kwa siku.
Zaweza kuwa dakika 30 asubuhi (Ayubu 38:12-13), kuiweka sawa siku yako na kuyageuza mashauri ya waovu juu yako; usikubali kula lunch bila kupata dakika walau 15 na Baba yako wa mbinguni… Jioni siku ikiisha hakikisha unapata muda kurudi mbele za Mungu kwa shukurani na kuomba hekima ya kukusaidia siku zako zijazo.
(Yakobo 1:5-7, Waebrania 4:16, Wafilipi 4:4-7).
Daniel alikuwa waziri mkuu, mtu busy sana Babeli lakini aliweza kuomba majira haya matatu kwa siku (Danieli 6).
Wewe ni waziri mkuu wa nini? Uko busy sio? (BUSY-Be Under Satanic Yoke).
2. Lazima usome kitabu cha kiroho au cha kujenga akili na ufahamu wako (walau sura moja kwa siku) na Biblia.
Vitabu mnavyo kwenye computer zenu, wengine mnazo hata hardcopy lakini HAMSOMI.
Biblia nayo mnasoma kiholela, ovyoovyo.
Ukisoma Biblia lazima uwe na sehemu ya kuandika kila ulichosoma kwa siku hiyo.
Unaandika umesoma wapi, summary iliongelea nini… Je umejifunza nini hapo? Siri zipi umedaka? Maandiko yapi umeyashika na utakuwa ukiyakiri na kuyatumia kwenye maombi?
Kusoma ni lazima (Danieli 9:2, Luka 4:16-19, Mathayo 22:29).

3. Lazima uwe na muda wa kuangalia video walau moja ya mtumishi wa Mungu.
Mnazo kwenye folder za PC zenu lakini hamuangalii… Kama huna download youtube au install tubemate ina download vizuri na angalia!
Hakikisha umelinote down somo zima, umedaka nini? Maandiko mapya uliyopata, kanuni zipi za kuinua maisha yako umepata? Andika vyote chini… Ndani ya wiki utakuwa umeangalia 7, kwa mwezi 30, kwa mwaka 365… Na hauwezi kuwa sawa na wengine!

4. Kila siku andika njozi, maono na ndoto zako.
Zipanue, ziwekee namna na njia ya kuzifikia, ukishaandika kiri kila siku kuwa utakuwa au utafikia hizo ndoto na hautakufa bila kuwa au kufikia hicho kiwango…bandika mikono na kuanza kutabiri na kuamuru zifanye haraka kutimia ndani ya muda na majira ya Mungu (Habakuki 2:2-4), omba watu sahihi na matukio sahihi yatakayokupelekea kwenye ukamilifu wa hizo ndoto.
Haya ni mambo ya kufanya KILA SIKU.
Unapozipitia kila siku UNAJIONA WEWE HALISI inakufanya upuuze yanayoendelea nje na uamini ulichoona ndani yako na hakika ndivyo utakavyokuwa (Mithali 23:7).

5. Kila wiki andaa kisomo kifupi walau kimoja kutokana na yale uliyojifunza wiki nzima, itakusaidia sana kukua kiroho.
Ndani ya mwezi utakuwa na masomo 4, ndani ya mwaka utakuwa na masomo 52, na hakika hautashindwa kuanza kufundisha wengine.
“Kila Mwalimu bora ni mwanafunzi mzuri waziwazi au sirini”
Na wajinga ni asilimia zaidi ya 80 ya watu wote, inahitaji mimi na wewe pamoja tugeuze hili jambo na kugeuza maisha yao.

Mimi nimefanikiwa, sioni sababu ya wewe kutofanikiwa pia.
Hii ratiba kila mtu anaiweza, usisubiri FREE TIME, haipo kwenye maisha.
Mtu hutengeneza muda kwa kitu anachokitaka na kukihitaji mno mno mno.
Kama utaanza kufanya haya, kila siku kwa uaminifu kuna siku utanitafuta na kunipa shuhuda na zawadi kwa kuyafanya maisha yako yawe na maana.

Ni mimi mwana wa Mungu,
Mwl D.C.K
Destined To Reign International Ministries (DETRIM).

Karibu kwenye Tovuti ya Kikristo... hapa utapata mafunzo Mbali mbali ya kukujenga kiimani ,kifahamu,kimazingira na hata kitabia Karibu Tena

Tagged with: , , ,
Posted in Mafunzo

Toa mawazo,maoni

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out / Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out / Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out / Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out / Change )

Connecting to %s

yaliyopita
Ungana nasi kwenye kurasa yetu  ya facebook na like page yetu-kuweza kutangaza neno la bwana na utabalikiwa sana..kwa kazi yako kuu kwani thawabu yako mbinguni ni tele

Andika E-mail kwenye box hapo chini kisha Bonyeza (jiunge Hapa)na uweze kujiunga na tovuti hii kupitia e-mail yako utakayojisajilia,tutaweza kukupa kila taarifa,habari zinazojili kwenye hii blog yetu asanteni

Join 2,217 other followers

Upcoming Events

No upcoming events

%d bloggers like this: