KULA KWA JASHO

https://scontent.xx.fbcdn.net/v/t1.0-9/12994488_1002043333165168_3089602848912551744_n.jpg?_nc_eui2=v1%3AAeFsl-V5P3KAQwYBctSNpvqlpQWIQMTCZFI78pvHTNGDMoyCpnUS8ANE2htBLRWQV1XEA0jHfW8Xm9Ykrh4Xm6tuBpTHVmi7SrZPcsmTnpzxbA&oh=dd6540fcd12607b10064608364aae515&oe=58628271

1. Haukuwa Mfumo wa kwanza wa Maisha, ni mfumo uliokuja KAMA LAANA, na haukuwa option ya kwanza ya Mungu!

2. Kula kwa jasho ni Mfumo wa kiwango cha chini mno, ambao haufikii hata nusu ya mfumo wa kwanza ambao Mungu alituumba kuuishi.

3. Mfumo wa kwanza wa KUTOKULA KWA JASHO tuliupoteza kwa anguko la mwanadamu bustanini (dhambi), Lakini UMEREJEA KUPITIA KRISTO YESU NA WOKOVU.

4. Mfumo wa kula kwa jasho ni mfumo ulioko kwenye SEKTA YA AJIRA, Unatoa jasho ili ule na kumudu maisha.
Ukikubali kuajiriwa umeukubali mfumo wa kula kwa jasho, maana unafanya kazi si kwa ajili yako bali kwa ajili ya Boss wako.
Huu ni mfumo wa kinyonyaji, kula yako inategemea huruma za mwajiri.

5. Waajiri wote wamejitoa kwenye Mfumo wa kula kwa jasho, ila wamewaweka watu chini yao wanaotoa jasho badala yao, huku wao wakivuna jasho la wanaopenda kutoa jasho.

6. Mungu alituumba na kutuagiza tufanye kazi, ila hakutuagiza tutoe jasho. Jasho limekuja kama laana, na hatuwezi kukubali kuendelea kuwa chini ya laana baada ya Yesu kufanya kila kitu msalabani.

7. Ili utoke katika Mfumo huu kandamizi wa kula kwa jasho, unalazimika KUANZISHA VYAKO, na kuwaza kuwapa ajira wanaopenda kutoa jasho wafanye kazi kwa niaba yako kwenye wazo uliloanzisha huku wewe unahesabu faida kwa jasho lao.

8. Kila anayeanzisha kitu chake, na kuweka watu wafanye kazi badala yake (waajiriwa), mtu huyo ameishinda laana ya kula kwa jasho.

9. Ni muhimu ujue, kula kwa jasho si baraka bali ni laana, si ujanja bali ni adhabu na hukumu dhidi ya dhambi.
Kula kwa jasho si njia pekee ya kuishi, unaweza kurudi tena Edeni pale utakapoamua KUISHI KWA KILA NENO LITOKALO KINYWANI MWA BWANA.

Tangu nilipojua haya, nilijitoa kwenye orodha ya wanaokula kwa jasho.
Maisha yangu yanakwenda kwa wepesi mno na kwa spidi kubwa, naishi kwa Kanuni tofauti na wanayoishi nayo karibu watu wengine wote duniani.

Advertisements

Karibu kwenye Tovuti ya Kikristo... hapa utapata mafunzo Mbali mbali ya kukujenga kiimani ,kifahamu,kimazingira na hata kitabia Karibu Tena

Tagged with: ,
Posted in Mafunzo

Toa mawazo,maoni

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out / Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out / Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out / Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out / Change )

Connecting to %s

yaliyopita
Habari iliyotazamwa sana
Ungana nasi kwenye kurasa yetu  ya facebook na like page yetu-kuweza kutangaza neno la bwana na utabalikiwa sana..kwa kazi yako kuu kwani thawabu yako mbinguni ni tele

Andika E-mail kwenye box hapo chini kisha Bonyeza (jiunge Hapa)na uweze kujiunga na tovuti hii kupitia e-mail yako utakayojisajilia,tutaweza kukupa kila taarifa,habari zinazojili kwenye hii blog yetu asanteni

Join 2,212 other followers

Upcoming Events

No upcoming events

%d bloggers like this: