MVIVU

https://scontent.xx.fbcdn.net/v/t1.0-9/12472598_1001550493214452_6746639582333585050_n.jpg?_nc_eui2=v1%3AAeHB0cFRyXe6tFmeDS1Nc5wQNoRc_Mg0i_mkUT5I7LsSNc9cVoooUyiQpu34sI-uFZzUVhj4CTWdHbgcHvUXF-FjBJYu0rkgtMn4jD0VaG4WiA&oh=33ed34e28d623d55bf5700b6f4cfe3c6&oe=585F7B95

“Mtu yeyote anayekuambia juu ya hatari zilizoko kwenye njia yake kuelekea mafanikio anayoyataka, na anadai ndio sababu ya yeye kuacha kuchukua hatua kuelekea mafanikio, MTU HUYU NI MVIVU”
(Mithali 22:13).

“Mtu yeyote ALIYEFUNGA NDOA NA GODORO, anafanya kazi ya kugeuza mbavu zake, kama mlango unavyogeuka kwenye bawaba, MTU HUYU NI MVIVU”
(Mithali 26:14).

“Mtu anayependa kusukumwa sukumwa, kusimamiwa simamiwa, kuelekezwa elekezwa, kuambiwa ambiwa mambo ambayo alipaswa kujiambia, kujielekeza, kujisukuma, kujisimamia, MTU HUYU NI MVIVU”
(Mithali 6:6-8).

“Mtu asiyefikiri kuhusu kesho, na kuweka mikakati ya kuikabili hiyo kesho, anasubiri vitu vitokee bila mipango na maandalizi, MTU HUYU NI MVIVU”
(Mithali 6:6-8).

“Mtu yeyote ambaye mambo yake yako shaghalabaghala, hayana mipangilio, hayana unadhifu, uzuri na ubora, MTU HUYU NI MVIVU”
(Mithali 24:30-34).

“Mtu yeyote anayeuhurumia mwili wake, na anapenda kujihurumia hurumia, badala ya kuutesa mwili na matakwa yake ya muda mfupi, MTU HUYU NI MVIVU”
(Mithali 20:4).

“Mtu yeyote ambaye ukijaribu kumulekeza yampasayo ili afanikiwe, anajitia mjuaji na anakupa sababu nyingi za kwanini haiwezekani, badala ya kwanini aweze, MTU HUYU NI MVIVU”
(Mithali 26:16).

NAIAMURU ROHO CHAFU YA UVIVU IKUTOKE KWA JINA LA YESU.

Advertisements

Karibu kwenye Tovuti ya Kikristo... hapa utapata mafunzo Mbali mbali ya kukujenga kiimani ,kifahamu,kimazingira na hata kitabia Karibu Tena

Tagged with: , ,
Posted in Mafunzo

Toa mawazo,maoni

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out / Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out / Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out / Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out / Change )

Connecting to %s

yaliyopita
Habari iliyotazamwa sana
Ungana nasi kwenye kurasa yetu  ya facebook na like page yetu-kuweza kutangaza neno la bwana na utabalikiwa sana..kwa kazi yako kuu kwani thawabu yako mbinguni ni tele

Andika E-mail kwenye box hapo chini kisha Bonyeza (jiunge Hapa)na uweze kujiunga na tovuti hii kupitia e-mail yako utakayojisajilia,tutaweza kukupa kila taarifa,habari zinazojili kwenye hii blog yetu asanteni

Join 2,212 other followers

Upcoming Events

No upcoming events

%d bloggers like this: