UKWELI KUHUSU BABA WA KIROHO-2

https://i2.wp.com/media.salemwebnetwork.com/cms/CCOM/4382-bible%20prayer%20bw%20EDIT.630w.tn.jpg

1. Anakuwa na uzoefu binafsi katika ushirika na Mungu, na anakuwa ametengeneza NJIA ZAKE (Mitazamo, Kanuni, Tabia) ZILIZO KATIKA KRISTO (Zilizo sawa na mafundisho sahihi ya Neno la Mungu na Maneno yenye uzima ya Bwana wetu Yesu Kristo), na Wanae huzifuata njia zake hizo zilizo katika Kristo!
“Kwa sababu hii nimemtuma kwenu Timotheo, aliye mwanangu mpendwa, mwaminifu katika Bwana, ATAKAYEWAKUMBUSHA NJIA ZANGU ZILIZO KATIKA KRISTO, kama nifundishavyo kila mahali katika kanisa”
(1Wakorintho 4:17).
Angalizo:
Ufuate njia za Baba yako wa kiroho zilizo katika Kristo Yesu, zinazosadifu Injili.
Usibebe lugha yake, hasira zake, na mambo yake binafsi ambayo yaweza kuwa udhaifu wake kwa sababu ya mazingira aliyokulia, mambo aliyopitia nakadhalika.
Chukulia mfano, Baba yako wa kiroho alikuwa teja au mvuta bangi kijiweni na kibaka, halafu ameokoka, lakini kuna vitu viko ndani yake hasa lugha, tembea, namna anavyokabili pressure za maisha, na wewe unayabeba hayo ukidhani ni ukiroho kumbe ni athari alizonazo toka kwenye past yake, kuwa makini usijekuwa kituko.
Fuata njia zake zilizo katika Kristo tu, kile afundishacho katika kanisa kila mahali na si tabia au mitazamo yake inayokinzana na Neno la Mungu na mafundisho yenye uhai ya Yesu Kristo!

2. Anaelewa kwamba yeye si Mwili mzima wa Kristo bali ni kiungo tu katika mwili mkubwa wa Kristo, hivyo HAJUI KILA KITU NA HANA KILA CHAKULA CHA KUWAJENGA WATOTO WAKE.
Hivyo anatambua na kuwakubali Watumishi wengine wa Mungu, na hasimami kupambana nao akiona wana kitu asichokuwa nacho, bali akiona kitu cha thamani anawaruhusu Wanae wakichukue kwa WALIMU KUMI ELFU walio katika Kristo Yesu.

“Kwa kuwa ijapokuwa MNA WALIMU KUMI ELFU KATIKA KRISTO, walakini HAMNA BABA WENGI. Maana mimi ndimi niliyewazaa ninyi katika Kristo kwa njia ya Injili”
(1Wakorintho 4:15).
Baba wa Kiroho asiyekiri wazi kuwa hana kila chakula wanachohitaji kanisa na akawatambulisha kwa Walimu wengine (watumishi wengine), kuna walakini mahali.
Hatuna kila kitu, tunajua kwa sehemu, sehemu nyingine Mungu kaziwekeza kwa watumishi wake wengine.
Kila baba sahihi wa kiroho atakuelekeza kujifunza kwa wengine, na utamsikia akiwakubali wanaofanya asichofanya yeye.
Hana muda wa kuanza ligi na watumishi wengine wa Mungu.

3. Baba yeyote wa kiroho, anawaruhusu wanae wa kiroho Wamfuate yeye kama yeye anavyomfuata Kristo.
Hawaambii wamfuate yeye tu, BALI ANAMTAMBULISHA YESU KWA WANAE, na wanae wanamfuata Yeye kama yeye anavyodumu kumfuata Kristo. Akikorofisha, wanae wanaweza kugundua maana wanamfuata baba lakini jicho likiwa kwa Yesu na Neno lake!
“Mnifuate mimi kama mimi ninavyomfuata Kristo”
(1Wakorintho 11:1).
Kuwajenga wanao wa kiroho kwa Yesu na Neno lake kutawafanya wakue kufikia kimo cha Kristo na si kuwa kama wewe.

Advertisements

Karibu kwenye Tovuti ya Kikristo... hapa utapata mafunzo Mbali mbali ya kukujenga kiimani ,kifahamu,kimazingira na hata kitabia Karibu Tena

Tagged with: , , ,
Posted in Mafunzo

Toa mawazo,maoni

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out / Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out / Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out / Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out / Change )

Connecting to %s

yaliyopita
Habari iliyotazamwa sana
Ungana nasi kwenye kurasa yetu  ya facebook na like page yetu-kuweza kutangaza neno la bwana na utabalikiwa sana..kwa kazi yako kuu kwani thawabu yako mbinguni ni tele

Andika E-mail kwenye box hapo chini kisha Bonyeza (jiunge Hapa)na uweze kujiunga na tovuti hii kupitia e-mail yako utakayojisajilia,tutaweza kukupa kila taarifa,habari zinazojili kwenye hii blog yetu asanteni

Join 2,212 other followers

Upcoming Events

No upcoming events

%d bloggers like this: