MAJANGA KWENYE MITANDAO

(SOMA NI YA MUHIMU SANA)

https://i2.wp.com/curationsoft.com/ckeditor/userfiles/black%20twitter.jpg

Sio kila unayemwona humu mtandaoni ni mwanadamu wa kawaida.Wengine ni majini,wengine ni watu lakini mawakala wa shetani,wengine ni mizimu,wengine ni marafiki kabisa tunawajua lakini shetani anawatumia humu.Wengi wapo kutuharibu vijana,wengine watakujia faragha na kukufundisha tabia chafu,wengine ni wachawi,wengine watakutongoza na utajikuta huna nguvu ya kukataa,kila unapotaka kujitoa unashindwa,wengine ni misukule inayoishi,wengine wapo kupandikiza roho za uzinzi ndani yako ndio maana ulikutana na mtu mtandaoni akakufundisha kujichua sehemu za siri,au punyeto kwa lugha rahisi,kuna watu wanapoteza ndoa zao kwasababu ya kukutana na watu mitandaoni.Kuna watu wamejifunza kuingiliwa kinyume na maumbile humu humu,wengine wamepewa roho za kuwashinda watumishi wa Mungu kwa kuwatengenezea mazingira ya uzinzi,hasira,tamaa nk.
Wengine ni kama wajasiamali lakini wanauza vitu vya kuzimu,utashangaa umenunua mkufu lakini toka uanze kuuvaa matatizo hayaishi,wengine ni wasichana wadogo lakini wanajikuta wanapenda mahusiano na watu wazima mno.
Shetani yuko kazini mjitazame sana,humu mtandaoni ni kichaka cha watu waovu.Watu wema ni asilimia mbili tu.Yaani kuna watu wema kabisa wawili katika kila rafiki zako mia moja mtandaoni.Ndio maana kila siku unatongozwa na kila mtu anasema anakupenda.Je uliumbwa kuwa cha wote?Huu ni uonho wa ibilisi.

Acha kuteseka,njoo kwa Yesu ufunguliwe.Wengi mtaficha lakini nataka nikwambie muda wako wa uponyaji ni sasa sio kesho wala kesho kutwa.Ni saa hii.Nasema ni saa hii usiahirishe uamuzi wa kubadilika,usione aibu msaada ni kwa Bwana.

Wengine mkilala mnaota mko na wanawake au wanaume mkifanya mapenzi,wengine hata kinyume na maumbile yenu,na asubuhi mkiamka mnakuta mbegu kabisa katika hali halisi,wengine mnajikojolea kitandani hata leo,maisha yenu yamejaa aibu na simanzi,wengine kuna tabia kila mkiacha zinarudi.Nawaambia hakuna namna ya kuchomoka zaidi ya kumwangukia Mungu.Yesu ndiye njia,kweli na uzima. Wengine mnateswa na kafara kuna damu za wanyame zinanena laana,nuksi,mikosi huko kwenye madhabahu za kichawi,wengine mnaota mnakimbizwa kila usiku, wengine mmeolewa na kila mimba inaharibika,wengine nguvu za kiume zimeisha kisa punyeto,wemgine mmeoa ila ulikosa radha na mkeo ukajaribu nje na toka hiyo siku umepoteza nguvu za kiume, nataka nikwambie ulilalala na jini,mchawi ama wakala wa shetani,wengine mkipata pesa hazikai zinatumika tu hovyo,mkiwa hamna mnakuwa na mipango mkizipata mnafanya mambo mengine kabisa.Yesu yuko kuwapa mwanzo mpya.Yesu anabisha mioyoni mwenu.Mungu anawatazama.
Mwingine yeye anateswa na roho ya usagaji,anatamani kuwa mwanaume wakati ni binti.Hatari hii,huna amani na hayo maisha,Yesu yuko kukupa amani.

Hii sio kawaida kuna namna imetendeka, kuna agizo limetoka kuzimu kukuharibu lakini natangaza tumaini jipya leo.
Yesu anaokoa.Yesu anaponya.
Wengine mmeibiwa nyota zetu,vibali vya kupendwa na kuheshimika,wengine mlitakiwa kuwa na nyadhifa kiuongozi lakini kuna watu wamezichukua,na kila karama maishani zimetekwa.Huwezi tena kufaulu darasani wala kuelewa,huwezi tena na huna hamu kujisomea.Umefungwa usioe wala kuolewa ,naam nimeinuka kusema rudisha,Shetani ataachia alichokuibia.Yesu ndiye Bwana wa Vita.

Unachukiwa kazini,nyumbani wamekuchoka,umegeuka kahaba ,chizi,masikini wa kutupwa,mshirikina…usikate tamaa. Yesu anaweza kukufungua.
Inuka leo,inuka umtazame Bwana naye atakufungua kwa rehema na neema zake.
U mtu huru wewe,u mshindi wewe.Epuka hukumu,epuka kuonewa,epuka kudhurumiwa.
Yesu yuko kukuondolea mzigo wako leo kama tu utasema NDIO.
Imeandikwa na Jofrey Josephat Kaigarula

Kama umekutwa na haya mambo na ungependa kufunguliwa na kusaidika, msaada upo, Yesu atanitumia kukusaidia.

Advertisements

Karibu kwenye Tovuti ya Kikristo... hapa utapata mafunzo Mbali mbali ya kukujenga kiimani ,kifahamu,kimazingira na hata kitabia Karibu Tena

Tagged with: ,
Posted in Mafunzo

Toa mawazo,maoni

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out / Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out / Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out / Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out / Change )

Connecting to %s

yaliyopita
Ungana nasi kwenye kurasa yetu  ya facebook na like page yetu-kuweza kutangaza neno la bwana na utabalikiwa sana..kwa kazi yako kuu kwani thawabu yako mbinguni ni tele

Andika E-mail kwenye box hapo chini kisha Bonyeza (jiunge Hapa)na uweze kujiunga na tovuti hii kupitia e-mail yako utakayojisajilia,tutaweza kukupa kila taarifa,habari zinazojili kwenye hii blog yetu asanteni

Join 2,219 other followers

Upcoming Events

No upcoming events

%d bloggers like this: