NAMNA YA KUFANYA VITU VIKUBWA VITOKEE KATIKA MAISHA YAKO.

Utangulizi:

~Watu wengi wana vitu Ndani yao lakini wengi wao hawavifanyi kwa kutoa sababu mbalimbali kama vile; ningesoma sana ningekua hivi, ningekua na pesa ningefanya hivi nk.

Capture.PNG

Ushuhuda wa mwalimu Dickson

Anasema alianza kidogo katika utumishi wake, hakua na mtu anayemjua licha ya kwamba alikua na kitu Ndani yake. Hakupata platform kwa hiyo akaanzia Facebook ( KUTHUBUTU) . Kwa wakati huo (2009) facebook ilitumika kutengeneza marafiki tu lakini yeye aliamua kuwa anapost jumbe za Neno la Mungu na hata kunakiri baadhi ya jumbe za watumishi mbalimbali.
Hakukua na watu wanaolike au hata kucoment lakini aliendelea ( KUTOKATA TAMAA)
*Baadaye alianza kuona response ya watu katika comment na likes na mwaka 2012 akajitokeza mtu aliyejitolea kufungua blog na baadae website (www.yesunibwana.org ) kwa ajili ya kuhamishia masomo ili yasipotee kule na sasa inatembelewa na watu wengi (Wastani wa watu 200,000 kwa mwaka, kwa takwimu za WORDPRESS kwa mwaka jana), Mungu alitumia mtu yule kujitolea baada ya yeye kuchukua hatua hata kama hakua na pesa , hasingesubiri kuwa na umati kama Mwakasege Bali alianzia pale alipokuwa.
**Anzia pale ulipo , chukua hatua hata kama Mwanzo wako ni mdogo mwisho wako utaongezeka sana..Ayubu 8:7.

Chukua hatua ya kwanza ndipo Yesu ataingilia kati.

~Ushuhuda unaendelea ..

Mwalimu anasema alipokua anasoma wakienda kwenye makongamano alikua na daftari lake la marafiki wa mwalimu , wakati wa mapumziko aliwafuata watu na kujitambulisha na kuomba mawasiliano nao na baadae kuwa anawatumia masomo nk. Aliomba nafasi za kuhudumu na kushiriki bible study nao , alifanya kitofauti kila alipopewa nafasi hali iliyosababisha aanze kualikwa kuhudumu. Hapa alitengeneza nafasi( TENGENEZA NAFASI/CREATE OPPORTUNITY)
*Usisubiri kuitwa jipeleke katika maono yako.
Hata katika wakati wa field alifanya hivyo hivyo na kujikuta marafiki wale ndiyo wanaomsapoti hata Leo, na hata Huduma katika redio nk.

“Kuna hatua ndogo sana kati yako na mafanikio yako”

*Hajiri hakujua kama pembeni yake kulikuwa na maji maana tayari alishakata tamaa juu ya mtoto wake Ishmaeli (Mwanzo 21:16-19).

* Zaburi 119:130 kufafanusha Maneno ya Bwana hututia Nuru na kumfahamisha mjinga.

Ndiyo maana malaika alipomwambia (Neno la Ufunuo) Hajiri alimpa mtoto maji na wakaishi.

* Mungu anayefuatilia mtu mwenye ndoto Kama Ishmael mtoto wa Hajiri hawezi kuacha kufuatilia maisha yako hata kama utakosea.

* Ukitenda kosa na ukapata mtu wa kukuonya au ukajiskia hatia Ndani yako basi Roho Mtakatifu bado yupo na Mbingu bado zinakuhitaji.
*Isaya 43:25
Mungu hutusamehe dhambi zetu na hazikumbuki tena.

* Katika suala la msamaha wa dhambi watu hufuata hisia kuliko Neno.

* Neno huanza kabla ya amani au hisia maana amani huletwa na Neno.

*Mungu sio shabiki wa hisia bali Neno lake
Yeremia 1:12..Huangalia Neno lake ili alitimize.

Hesabu 23:19..yeye sio mwanadamu hata aseme uongo.

**Wakristo wengi ni “sense lead” na sio “Spirit lead”, A matured Christian ni yule anayefanya vitu tofauti na anavyojisikia.

Hata kama hajiskii kufunga,kuomba,kusoma Neno nk.,hutafuta nafasi na mazingira kama kuweka nyimbo za kuabudu ,kusoma au kusikiliza mafundisho ya watumishi wa Mungu nk.

**Baraka za Ibrahim zinaambatana nasi maana sisi tu uzao wake. Mwanzo 12:1-3

**Mwanzo 12:3..Mungu anabariki na kukuza majina yetu.

Ni kusudi la Mungu kukuza majina yetu maana sisi ni Nuru..Mathayo 5:14.

***Mwl’s declaration:

“Kila kilichochelewesha majina yetu kukua kimeshindwa kwa Jina la Yesu”

*Galatia 3:7&9, 29
Walio na Imani ndiyo wana wa Ibrahim nao hubarikiwa pamoja naye.
*Kila ahadi aliyopewa Ibrahim ni haki ya kila mmoja wetu na lazima tudai.
* Vitu vya rohoni huwa transfered kutoka kizazi hadi kizazi. Kama kuna laana asipotokea mtu wa kuivunja itaendelea kutafuna vizazi hadi vizazi.
Hivyo na Baraka za Ibrahim lazima ziambatane nasi.

KWA NINI VITU VITOKEE?

**Tunatakiwa kutengeneza mahali palipobomoka
Isaya 58:12
~Wakati mwingine Mungu hutupa nafasi ya kuandaa vitu kwa ajili ya vizazi vingine.

~Watu wengi ni heaven minded wanafikiria tu kwenda mbinguni badala ya kuujenga ufalme wa Mungu wakiwa bado duniani ,kutenda mambo makuu katika ufalme.
(Mathayo 6:9-10, Danieli 11:32b, Zaburi 60:12).
~”Mungu anataka tuestablish vitu ambavyo vitakuwa sample ya mbinguni tukiwa hapa duniani”

* Efeso 2:19
Sisi ni wenyeji pamoja na watakatifu na sio wageni hivyo mbinguni tutaenda tu, sasa tufanye mambo makuu hapa duniani yatakayomtukuza Mungu tuliyembeba.

* Luke 15:11-32
Mwanampotevu alijua ana haki katika urithi wa baba yake just by the virtue of being a son.

*Mathayo 25:31-46
Mungu atatuhukumu kwa jinsi tunavyodeal na watu kama wenye shida nk. Hivyo lazima tuwe na fedha ili tuguse maisha ya watu wengi kwa fedha hizo.
~ Huwezi kutoa usichonacho.
~Mungu hufanya supply ya abundance na sio daily basis.
~Tunabarikiwa ili kuwa Baraka kwa wengine, maisha yetu yaguse na watu wengine wengi..MF. Kenneth Copeland na TB Joshua .

*Pesa haibadilishi tabia ya mtu Bali hudhihirisha tabia ya mtu.

* Maombi yetu yawe reflected pia kwa watu wengine tusiombe maombi ya ubinafsi.

* Shetani akijiinua anatupa lifti maana yuko chini ya miguu yetu.
(Luka 10:19, Rumi 16:20).
* Katika mambo yote mabaya au mazuri Mungu hufanya kazi pamoja nasi akitupa mema Warumi 8:28.

Kiri Neno la Mungu kila siku.
*Wafilipi 1:6
Aliyeianzisha kazi njema ataikamilisha.

***Whatever is going on in this world does not concern you since you are the temple of the Holy Ghost and Citizen of heaven.

****The more you accumulate power from the Holy Ghost through speaking in tongues the more powerful you become.

Hata Yesu alikuwa katika hatua, baby Jesus aliyezaliwa katika holi la ng’ombe, matured hadi miaka 30, Spirit filled Jesus (miaka 30 hadi 33), The Risen and glorified Jesus tunayemuabudu milele!

##Kama wewe ni raia wa mbinguni , supply yako inatoka mbinguni.

* Sisi tu ishara na ajabu zitokazo kwa Bwana,Isaya 8:18.
*Usikubali kuwa pungufu wa ishara na maajabu.
Yohana 14:12..
Mambo yote aliyoyafanya Yesu unaweza kuyafanya na hata zaidi.
~Ukitaka kufahamu mambo aliyoyatenda Yesu soma vitabu vyote vya injili.
~Funga na omba hiyo nguvu,funga kukusanya nguvu.
FAST TO GET NOT TO SWEAT.

******
MAMBO YA KUFANYA ILI KUFANYA VITU VITOKEE.
*1⃣ Uelewe uumbaji wako.
Kwamba umeumbwa kwa sura na mfano wa Mungu. Tumeitwa kutiisha na kutawala kila kitu hapa duniani. Mwanzo 1:26-28.

~ Tuna nguvu kuliko changamoto tulizonazo.

~Sura ya Mungu iko Ndani yetu.

~Baraka zake ziko juu yetu
Mithali 10:6

~Baraka zimeshawekwa kwetu, Speak it to see it!

Yusufu alifanya mambo makubwa though alikua mdogo, lazima atokee mtu wa kuvunja chain mbaya ili Baraka zianze.

~Dare to take the first step..anza kama mtumwa baadae uwe waziri mkuu kama Yusufu.
~Amua kuwa mtu wa kutatua matatizo ya watu, hata kama you can make money out of it lakini bado utakua unatatua changamoto fulani, Eg.Huduma ya M-pesa karibu inasaidia watu kutokwenda umbali mrefu lakini pia you are making money.

“KILICHOMFANYA MUNGU APUMZIKE SIKU YA SABA SIO KWAMBA ALIKUA AMEMALIZA UUMBAJI BALI KWA KUWA ALIKUWA AMETENGENEZA MWANADAMU ALIYEKUWA NA UWEZO WA KUFANYA VITU VITOKEE.”

~Ukitaka kitu kitokee katika maisha yako kiseme. Talk it and you will see it.
~Tunaangalia njia tulizonazo katika Neno la Mungu na sio mazingira magumu tuliyomo.
~Ukiona unasema kitu cha kiungu na watu wanakucheka hawakuelewi jitenge nao.

*2⃣ Elewa sababu ya kuumbwa
Mwanzo 1:28, tunatakiwa kuzaa na kuongezeka.
~kama ni duka likue na kuzaa mengine na hata kufikia supermarket .
~Ukianzisha kitu, usiishie kuanzisha, kipanue nikamate kila sehemu, NDANI YAKO IKO BARAKA YA KUONGEZEKA (KUZIDISHA UNAVYOVIANZA)!
~Jifunze kwa watu waliofanikiwa.
*Zaburi 8:1-6, Zaburi 115, Mungu ametutawaza juu ya kazi zake zote.

***Resources 5 za kukufanikisha ulizonazo tayari;

~Uhai
Mhubiri 9:4, Mathayo 6:25-26 .
Kuna tumaini kwa walio hai.
maisha (uhai) ni bora kuliko chochote!
Wanao acha rekodi mpya ni walio hai na si mzito… Unaweza kutumia uhai wako kuacha alama!

~Muda
Ayubu 14:1,Mhubiri 3:1
Kila jambo na wakati wake, siku ni chache.
Ukomboe wakati, chezea vizuri na muda na si kucheza muda!
Ukiuchezea muda, nao utayachezea maisha yako.

~Watu
Isaya 43:3-4,Isaya 60:11, Hebrews 12:14, Luka 6:38.

Kuna watu wamebeba Baraka zetu , Bwana atainua watu kwa ajili ya maisha yetu na utajiri wa mataifa utatujia, kuwa na amani na watu wote ni chanzo cha kufanikiwa duniani, kipimo tunachopimia watu ndicho tutakachopimiwa.
Watu ni maisha na maisha ni watu.
Washirika wanahitaji mchungaji, na mchungaji anahitaji washirika!
Wateja wanahitaji muuza bidhaa na muuza bidhaa anawahitaji wateja!

~Maamuzi
Kumb 30:19, Acts 10:38 Mungu ametupa uwezo wa kufanya maamuzi na wala hana upendeleo.
*Maamuzi yanaamua maisha yetu
*Mungu haingilii kamwe maamuzi yetu, ametuacha tuchague na kuamua kila kitu maishani mwetu.
*Utumie vizuri uhuru wa kuamua
“Amua vema upate mema”

~Nafasi ya kumjua Mungu kibinafsi
Ayubu 22:21, Daniel 11:32
#The more you grow deeper in God ,the more you reign in your life.
#The one who kneels before God will make anything to kneel in his life.
#The book of Acts of apostles could have not been written if the apostles would have not acted!
(Smith Wigglesworth).

*3⃣ Jielewe umeumbwaje;
Yohana 1:1-5, Ebr. 11:3

Tumeumbwa kwa Neno la Mungu. Lililo hai ,lenye nguvu na makali kuliko upanga wenye makali kuwili.
~Wewe ni Neno la Mungu katika udhihirisho.
Zab 82:6 sisi ni miungu wadogo
Yohana 3:31 ajaye kutoka juu yuko juu ya yote.
Yohana 1:1-5 Kila kitu kiliumbwa kwa Neno
~Nimepuliziwa pumzi ya Mungu nayo hutupa akili Ayubu 32:8.
TAYARI NIMEUMBWA NA NGUVU YA KUFANYA VITU VITOKEE!

*4⃣Nimeumbwa kuishi kutoka Ndani kwenda Nje na sio kutoka Nje kwenda Ndani;

Yoh 7:38, Mithali 23:7, Mithali 4:23, 1Sam 16:9, Mwanzo 6:5.

Mungu hataki hasara ndiyo maana anatufundisha ili tupate faida Isaya 48:17.
*Maisha ni kile kilichoko moyoni
* Maisha ni mawazo uliyonayo ndani
*Maisha ni picha za unayoona ndani yako
*Chemchemi za maisha hutoka ndani kuja nje
*Unachokiona ndani ndo wewe halisi

5⃣ Nina Mungu ambaye anaweza kurejesha kila kilichopotea iwe kwa uzembe wangu au kwa Kuonewa na shetani;

Acts 5:2, Yeremia 18:-1-6, Ufunuo 21:4-6, Isaya 64:8
~Mungu aliwarudishia destiny zao akina Elisha ,Daudi, Gideon nk.
1Falme19:14-16, Waamuzi 6:11-14

*6⃣ Nguvu inahitajika ili kuzalisha kitu chochote hapa duniani;

Hata mwanamke anapotaka kuzaa hutumia nguvu na hii huanza tangu katika maamuzi.

~Seasons are determined by faith and not by time.

Mwanamke aliyetoka damu kwa miaka, kwa imani aliponywa siku moja.
Isaya 66:9,Isaya 37:3, kumb 8:18, Yoh 16:21-22

*****
JINSI YA KUTUNZA NGUVU ZA MUNGU.

1⃣ Kufunga
Isaya 58:5-12

Kwanini kufunga?

~Kutafuta USO wa Mungu Isaya 58:5-,12 na Kutoka 33:12-17

~Kutafuta Ufunuo 2corth 4:-2-4

~Kutafuta nguvu za Mungu (Zaburi 105:4)

2⃣Mikesha
Hata ya binafsi
(Saa 6 hadi 9 usiku)
2Corth 11:27
Acts 12:5-17
Acts 16:25-31
*Hukumu hufanyika usiku, hivyo mkesha huleta breakthroughs.

*Imba,sifu omba kesha, tenga muda wako na Bwana nyakati za usiku usilale kama wengine.

3⃣Usomaji wa kina wa Neno la Mungu. Soma na tafakari.
Omba Roho Mtakatifu akupe mafunuo katika Neno .
Isaya 34:16, Mithali 25:2 ,1 Corth 2:9-13
TAFUTA NA UTAPATA MAANA KILA MTU ANA PACKAGE YAKE.

(Somo hili nilifundisha mwaka jana kwenye semina ya mabinti na akina mama pale Baptist Magomeni, ni mwaka mmoja uliopita, lakini ni bora sasa kuliko mwaka jana)!
Destined To Reign International Ministries,
www.yesunibwana.org
Ambwene Michael ya GK hii

Advertisements

Karibu kwenye Tovuti ya Kikristo... hapa utapata mafunzo Mbali mbali ya kukujenga kiimani ,kifahamu,kimazingira na hata kitabia Karibu Tena

Tagged with: , , ,
Posted in Mafunzo
3 comments on “NAMNA YA KUFANYA VITU VIKUBWA VITOKEE KATIKA MAISHA YAKO.
  1. Paul Mbeho says:

    Very trustfull

  2. Ev.R.Kanani says:

    Nimeisoma Leo nipotoka kazini hadi nikaona Sina haja ya kupika na kula lakini kwanza nimalize hii charge Hakika nimechaji maisha yangu.Mungu azidi kukufanya kuwa mtu Mkuu.

Toa mawazo,maoni

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out / Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out / Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out / Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out / Change )

Connecting to %s

yaliyopita
Habari iliyotazamwa sana
Ungana nasi kwenye kurasa yetu  ya facebook na like page yetu-kuweza kutangaza neno la bwana na utabalikiwa sana..kwa kazi yako kuu kwani thawabu yako mbinguni ni tele

Andika E-mail kwenye box hapo chini kisha Bonyeza (jiunge Hapa)na uweze kujiunga na tovuti hii kupitia e-mail yako utakayojisajilia,tutaweza kukupa kila taarifa,habari zinazojili kwenye hii blog yetu asanteni

Join 2,215 other followers

Upcoming Events

No upcoming events

%d bloggers like this: