UMAARUFU

(JIFUNZE KIJANA MWENZANGU)!

https://scontent.xx.fbcdn.net/v/t1.0-9/13876327_10153965966794302_214139700307414021_n.jpg?oh=cb070aa1027e886a81f3f6d961e0e372&oe=589D809F

Haha haha hahaha hahaha
haha haha hahaha hahaa
Ndivyo anavyoanza Raphael JoachimLyela halafu anaendelea…

Ni hivi, umaarufu. Kutaka kuwa maarufu unaweza hata ukavalishwa chupi na ukapigwa picha. Ukiwa maarufu na ili usishuke kiwango unaweza ukavalishwa hata sketi au gauni na wewe ni mkaka na ukapigwa picha na picha yako ukaisambaza mwenyewe. Umaarufu wa kipepo na kishetani ndio unaowafanya watu wamwage damu za ndugu zao ili kupata fedha. Ni aina hii hii ya umaarufu ndio inawafanya vijana kuingia kwenye dili za madawa ya kulevya na kujikuta wanatolewa kafara kama mbwa koko. Umaarufu umewafanya vijana wawe na nywele kama vichaa WAKISINGIZIA FASHION. Kumbuka FASHION INAYODHALILISHA UTU WAKO NI UCHAWI WA KIWANGO CHA MPUMBAVU NDANI YA KAPU LA UJINGA. Umaarufu. Kwani nani asiependa kuwa maarufu?

Je, wewe ni maarufu kuliko Lucifer Shetani?
Je, wewe ni maarufu kuliko dhambi?

Vyote ni maarufu ila umaarufu wake haujawahi kuvibadilisha kuwa kitu kizuri. FUMBO LA IMANI.

Umaarufu umewafanya watu waseme uongo ili wapate walichoamini kuwa ni tiketi ya kupata TUZO YA UJINGA iliyofungwa ndani ya KAPU LA KUTOKUJITAMBUA. Umaarufu umewafanya watu wamtumikie shetani kwa kujua au kutokujua. Umaarufu umewafanya watu wasijali sana UTU wa mtu kuliko mali na fedha. Umaarufu umewafanya watu watembee bega moja juu na lingine chini mpaka wakawa vilema wa kudumu. UMAARUFU UNAWEZA KUIGIZWA NA KUTENGENEZWA HATA KWA TUZO.

Umaarufu umewafanya wadada, wanaotaka kuwa na watu maarufu kuwa maarufu katika dhambi na kuchezewa kwa UBORA WA UJINGA WAO uliofungwa ndani ya UPUMBAVU wa NYUMBA YA BISKUTI. NANI ASIEPENDA KUJULIKANA?

Umaarufu sio mmbaya. UBAYA UKO NDANI YA MTU. Ila umaarufu mmbaya hutengenezwa kwa lengo la kumuharibu mjinga mmoja hivi anaetaka kusifika na kufahamika sana kuliko kujitambua. Angalia na chunguza watu maarufu, WENGI HAWASEMI TU ila maisha wanayoishi wasingependa wayaishi milele na milele lakini watafanyaje sasa na wameshakula SAMBUZA kwenye sinia la Mfalme Ahabu? Maisha ya umaarufu yanawatesa, ingawa mwanzoni waliyatafuta sana kwa udi na uvumba. Lakini wengi ni WAPWEKE SANA ndani ya vyumba vyao vya ndani.

Nilianza kwa kucheka as if ninalolisema ni jambo la kuchkesha ila INANIUMA sana kuona vijana WAKIPONDA MALI KUFA KWAJA na kuyaponda maisha yao na kuharibu HATMA yao. Wengine wanakufa kwa UKIMWI na madawa na kuuwawa na ukahaba na uasherati. INANIUMIZA sana kila ninaposikia vijana wanapotea kwa ujinga wa giza kiasi hicho na wengine kujiingiza ndani ya USAGAJI NA USHOGA ili kupata pesa na ili waendeshe magari ya kifahari.

Bwana Yesu ana haja na wewe kijana. Kama sio wewe unaesoma basi yupo mwingine anaesubiri umtumie asome. ITAKUSAIDIA NINI KUPATA VYOTE DUNIANI UNAPOISHI KWA KITAMBO NA UKAUKOSA UZIMA WA MILELE? Badili tabia. Badili nia. Mkubali Yesu awe BWANA NA MWOKOZI wa maisha yako leo.

UMAARUFU NA MUNGU HAKUJUI NI BORA UANZE UPYA LEO.

Mungu Kwanza.
FICHUKA.
YESU KANIWEZA.
FROM STREETS TO CORRIDORS.
Raphael JL:

Advertisements

Karibu kwenye Tovuti ya Kikristo... hapa utapata mafunzo Mbali mbali ya kukujenga kiimani ,kifahamu,kimazingira na hata kitabia Karibu Tena

Tagged with:
Posted in Mafunzo
2 comments on “UMAARUFU
 1. veronicamajaliwa40 says:

  Ameee ohhooo haleluhaj 

  Sent from my Samsung device

 2. Ribe Kanani says:

  HAKIKA NIMEBARIKIWA

  2016-10-15 21:16 GMT-07:00 YesuniBwana :

  > yesunibwana posted: “(JIFUNZE KIJANA MWENZANGU)! Haha haha hahaha hahaha > haha haha hahaha hahaa Ndivyo anavyoanza Raphael JoachimLyela halafu > anaendelea… Ni hivi, umaarufu. Kutaka kuwa maarufu unaweza hata > ukavalishwa chupi na ukapigwa picha. Ukiwa maarufu na il” >

Toa mawazo,maoni

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out / Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out / Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out / Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out / Change )

Connecting to %s

yaliyopita
Habari iliyotazamwa sana
Ungana nasi kwenye kurasa yetu ya facebook na like page yetu-kuweza kutangaza neno la bwana na utabalikiwa sana..kwa kazi yako kuu kwani thawabu yako mbinguni ni tele

Andika E-mail kwenye box hapo chini kisha Bonyeza (jiunge Hapa)na uweze kujiunga na tovuti hii kupitia e-mail yako utakayojisajilia,tutaweza kukupa kila taarifa,habari zinazojili kwenye hii blog yetu asanteni

Join 2,212 other followers

Upcoming Events

No upcoming events

%d bloggers like this: