UAMINIFU: SIRI YA KUTOKA KIMAISHA

NATAKA SIKU MOJA UWE NA KAMPUNI YAKO, BIASHARA YAKO, AU NAWE UWE NA VITEGA UCHUMI VYAKO; KAMA HAUTAKUWA MWAMINIFU KWENYE MALI, KAMPUNI AU AJIRA ULIYOPO, MUNGU HATAKUFANYA UFANIKIWE!

https://i0.wp.com/beardpictures.com/wp-content/uploads/2015/01/smiling-black-man-.png

“Na Kama Hamkuwa Waaminifu Katika Mali Ya Mtu Mwingine, NI NANI ATAKAYEWAPA ILIYO YA KWENU WENYEWE?” (Luka 16:12),
Hili Ni Swali Analouliza Yesu Kwako Wewe Ambaye Una Ndoto Au Malengo Ya Kuwa Na Biashara Yako Lakini Kwa Sasa Unafanya Kazi Kwenye Biashara Ya Mtu Mwingine.
Hili Ni Swali Analouliza Yesu Kwako Wewe Ambaye Sasa Una Ndoto Ya Kuwa Na Kampuni Yako Lakini Uko Kikazi Kwenye Kampuni Ya Mtu Mwingine.
Hili Ni Swali La Yesu Kwako Wewe Ambaye Umeajiriwa Lakini Una Ndoto Za Kuja Kuwa Mwajiri Siku Moja.
Hili Ni Swali Analouliza Yesu Kwako Wewe Ambaye Uko Chini Ya Huduma Fulani, Lakini Una Maono Ya Kuwa Na Huduma Yako Siku Moja.
JIBU RAHISI KWENYE SWALI HILO LA BWANA YESU NI HILI;
Kama Wewe Si Mwaminifu Kwenye Hiyo Ajira Uliyopo; Unachelewa Kuripoti Kazini, Unakuwa Wa Kwanza Kuondoka, Haujitumi Kazini Eti Usije Kumnufaisha Huyo Mmilki/ Mwajiri… Hakika Unajiweka Kwenye Wakati Mgumu Sana!
Kama Mungu Akikuhurumia Ukapata Hiyo Kampuni, Ukawa Mwajiri Basi Utakuwa Na WAFANYAKAZI/ WAAJIRIWA Ambao Watakuwa Na UTENDAJI MBOVU KAMA WAKO!
Biblia Inatuambia “KILA TUFANYALO TULIFANYE KWA MOYO NA BIDII KAMA KWA BWANA; SI KAMA WENYE KUTAFUTA SIFA KWA WATU”
Lakini Ni Ngumu Sana Kwa Mungu Kukuamini Wewe Na Kukupa “MALI YAKO MWENYEWE” Na Tatizo Litakuwa Limetokana Na “MBEGU MBAYA YA KUTOFANYA KAZI YAKO KWA UAMINIFU KANA KWAMBA UNALIPWA NA MUNGU [KAMA KWA BWANA]”

Yusufu Alipokuwa Kwa Potifa;
Alifanya Kazi Kwa Ubora Wa Juu Sana, Kwa Bidii, Nguvu Zote, Na Uaminifu Mkubwa; Potifa Akaanza Kufanikiwa Na Kustawi Kuliko Hapo Mwanzo.
Yusufu Hakufanya Kazi Kwa Kinyongo, Alifanya Kana Kwamba Ni Kazi Yake Mwenyewe.
Halafu Mungu Akamwamini Na Kumpandisha Ngazi Hatua Kwa Hatua Kufikia Hatua Ya Kuwa Waziri Mkuu Misri!

Daudi Alipokuwa Chini Ya Mfalme Sauli;
Alifanya Kila Kitu Kwa Ubora, Nguvu, Akili Na Uaminifu Wa Juu,
Hata Sauli Alipotaka Kumuondoa Bado Mungu Alimlinda Na Kumtetea,
Daudi Alipata Nafasi Nyingi “ZA KUMWANGUSHA BOSS WAKE SAULI” Lakini “HAKUTHUBUTU KUMGUSA” Katika Maeneo Yote “ALIMTENDEA MEMA MWAJIRI WAKE”

 

Yakobo Alipokuwa Kwa Mjomba Labani;
Yakobo Alifanya Kazi Yake Kwa Bidii, Nguvu, Na Uaminifu Wote,
Hakuwahi Kuacha Kufanya Kazi Yake Kana Kwamba Ni Yake,
Ingawa Labani [Mwajiri] Alimdhulumu Na Kumbadilishia MSHAHARA KWA HILA [Mara Nyingi] Lakini Alidumu Kuwa Mwaminifu Na Kutumikia Mkataba Wake Kwa Miaka 14 Yote Aliyokuwa Mwajiriwa.
Hakufanya Kazi Kwa Ulegevu, Wala Hakumfanyia Hila Mwajiri Wake,
Na Mungu Akampa Neema Kuwa Mwajiri Wa Wengi Pia.

UAMINIFU WAKO KWA MWAJIRI WAKO; KUFANYA KAZI ILE KANA KWAMBA NI YAKO, KUTAKUFANYA UPATE KIBALI KWA MWAJIRI WAKO, LAKINI ITAKUWA MBEGU YA MUNGU KUKUPA YAKO!

Advertisements

Karibu kwenye Tovuti ya Kikristo... hapa utapata mafunzo Mbali mbali ya kukujenga kiimani ,kifahamu,kimazingira na hata kitabia Karibu Tena

Tagged with: , ,
Posted in Mafunzo

Toa mawazo,maoni

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out / Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out / Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out / Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out / Change )

Connecting to %s

yaliyopita
Habari iliyotazamwa sana
Ungana nasi kwenye kurasa yetu  ya facebook na like page yetu-kuweza kutangaza neno la bwana na utabalikiwa sana..kwa kazi yako kuu kwani thawabu yako mbinguni ni tele

Andika E-mail kwenye box hapo chini kisha Bonyeza (jiunge Hapa)na uweze kujiunga na tovuti hii kupitia e-mail yako utakayojisajilia,tutaweza kukupa kila taarifa,habari zinazojili kwenye hii blog yetu asanteni

Join 2,212 other followers

Upcoming Events

No upcoming events

%d bloggers like this: