UNAZO RISITI ZA ADA ULIYOLIYOLIPIWA?KWANINI SASA URUDISHWE NYUMBANI KWA SUALA LA ADA?

Bwana Yesu Apewe sifa.
Karibu tupitie somo hili la RISITI ili tukumbuke kutembea na kuishi na risiti zetu za malipo yaliyokwisha kufanyika.https://i0.wp.com/parallelrealities.org/wp-content/uploads/2014/11/Dollarphotoclub_57355248x750-1-430x270.jpg

β—ΌHEBU TUPITIE HAPA.

πŸ”ΈSiku moja nilikua nikiongea na ndugu yangu mmoja katika Kristo,Akawa analalamika kuhusu suala la kuugua ugua na huku ameokoka.Ikafikia hatua akaniuliza au mimi sijasamehewa dhambi zangu zote?Akanipa na andiko ,Zaburi 103:3 inasema “AKUSAMEHE MAOVU YAKO YOTE , AKUPONYA MAGONJWA YAKO YOTE”.

πŸ”ΈAkaniambia si unaona hiyo Zaburi inavyosema,nadhani nitakua sijasamehewa makosa yote,maana imeandikwa akusamehe maovu yako yote na Akuponya magonjwa yote ila mm bado naumwa nadhani itakua bado kuna dhambi sijasamehewa.

πŸ”ΈKwakweli hiyo kauli mm ilinifanya nishangae na pia nicheke japo mwenzangu alikua akiongea katika hali ya usiliazi na kumaanisha anachokiongea.Maana sikutegemea kama anaweza kutumia mstari ule kujipa uhalali wa kuendelea kuumwa.Alijipa sababu ya pengine kwa nini anastahili kuumwa badala ya kutafuta kujua je anastahi kuumwa hata kama yupo kwa Kristo.?

πŸ’₯Bila Shaka utakubaliana na mimi kwamba huyu ndugu angesikia wametangaza sehemu kuna maombi ya kufuta dhambi zote zilizobakia ,haraka sana angehudhulia hayo maombi ili afutiwe dhambi zilizobaki😊😊😊😊

πŸ”ΈHebu Kama na wewe ulikua na mawazo hayo kama huyu ndugu yangu Nakuamuru yafute na uyaondoe haraka sana kichwani mwako,Sio ombi bali maadam tu umeokoka nakuamuru yaondoe na uyafute kabisa Katika Jina la Yesu na ninaamuru Kunyamaza kwa hiyo sauti danganyifu ndani yako inayokudanganya kwamba ww unastahili kuumwa kwakua kuna dhambi zako bado hazijafutwa

πŸ”ΈMOJA KWA MOJA IKABIDI TUINGIE DARASANI ILI KUPEANA MAARIFA .
πŸ”ΈTuungane kwa pamoja mimi na wewe unayedhani unastahili kuumwa,au unaumwa kwakua kuna dhambi unaweza kuwa haujasamehewa.

πŸ”ΈIsaya1:18 inawezekana umeuzoea huu mstari kuusoma mara kwa mara ila leo tuusome kwa pamoja,unasema”Haya Njooni tusemezane asema BWANA,dhambi zenu zijapokua nyekundu sana,zitakua NYEUPE KAMA THARUJI,zijapokua nyekundu kama bendera zitakua kama SUFU”

πŸ”ΈDaka hiyo,kwamba toka siku ya kwanza ulipoamua kwenda mbele za Bwana,kujisalimisha kwake,kusemezana nae(Kurudi kwake,kufanya sara ya Toba,Kumkiri Yesu Kristo kuwa ndiye Bwana na Mwakozi wa Maisha yako)toka ile siku ulifanywa kuwa safi,ulisamehewa dhambi zako zooote,hata kama ulikua mchafu kiasi gani ulifanywa kuwa msafi sana usiye na doa kama tharuji au Sufu.
Mpaka hapo Ondoa wazo la kusema labda kuna iliyobaki.

πŸ”ΈNa pengine utajitetea kwa kusema au labda anazikumbuka ndio maana naumwa(maana watu mnajitahidi kujitafutia sababu za kujihalalishia kuumwa).Hiyo kitu haipo hebu tupitie hapa kwa pamoja Isaya43:25 inasema “Mimi naam mimi ndimi nifutaye makosa yako kwa ajili yangu mwenyewe wala SITAZIKUMBUKA DHAMBI ZAKO”
Mungu Akisha kusamehe na kuzifuta dhambi zako hazikumbuki tena kwanza hazipo ,zishafutwa.(Naendelea kuondoa huo uhalali unaojiwekea ili mradi tuu uone kuugua ni kawaida noo).

πŸ”ΈNDUGU YANGU AKANIULIZA ,SASA KAMA MAMBO YAPO HIVYO KWANINI MM NAUMWA?(Kama vile ww unavyoweza kujiuliza kwanini nateswa na magonjwa?)

πŸ”ΈKabla ya kumpa sababu kwanini anaumwa ilibidi tupitie maandiko kwanza yanasemaje juu ya uhalali wa yeye kuumwa,jee anastahili kuumwa?Je magonjwa ni sehem yake ya maisha japo ameokoka?(Je magonjwa ni sehem yako japo umeokoka na hauishi maisha ya dhambi?)

πŸ”ΈNikampitisha hapa(tupitie kwa pamoja)Isaya 53:5 imeandikwa “Bali alijeruhiwa kwa makosa yetu,alichubuliwa kwa Maovu yetu,adhabu ya amani yetu ilikua juu yake NA KWAKUPIGWA KWAKE sisi tulipona.

πŸ”ΈTukapita na hapa tena(Twende pamoja)
Mathayo 8:15-17,hapo inaeleza na kuomesha jinsi Yesu alivyokua akiponya watu magonjwa yao na kuwafungua kutoka kila kifungo na ule mstari wa 17 unasema “Ili utimie ule unabii ulionenwa na Nabii Isaya akisema MWENYEWE ALITWAA UDHAIFU WETU NA KUYACHUKUA MAGONJWA YETU.”

πŸ’ͺπŸ’ͺHapo rafiki yangu akaanza kutabasamu na usoni mwake akaingiwa na tumain kwamba hee kumbe sipaswi kuumwaumwa mie(Kama vile ww usivyopaswa maana Yesu alichukua hiyo nafasi ya kusimama mbele ya magonjwa yako na kuyachukua ili mradi ww tuu uwe huru na uishi maisha yaliyojaa afya njema)

πŸ”ΈWaweza sema mbona hapo lakini sijaona alipopigwa na kuchubuliwa kwa hayo magonjwa niliyonayo kama inavyosema katika Isaya?
Ok hebu twende hapa Mathayo 27:27-31 ,ukipitia hapo kuanzia mstari huo wa 27 utaona jinsi gani Yesu alivyodhihakiwa ,kupigwa pigwa huku kichwan kavaa taji la miiba na ule mstari wa 31 unasema “Walipokwisha kumdhika wakalivua lile vazi wakamvika vazi lake WAKAMCHUKUA KUMSULUBISHA ”

πŸ”ΈHuko kwenye Kumsulubisha huko ndipo alipopigwa sana,Alipochubuliwa sana,alipoteswa sana,huko alipewa kila aina ya Mateso kwa ajili ya uponyaji wa kila eneo la maisha yako mpendwa wangu,huku alisulubiwa kwa ajili ya dhambi zako,magonjwa yako na kila aina ya madhaifu yako ilimradi wewe tuu leo uwe huru.

πŸ’₯1petro2:24 hapa Petro anawaambia na alikua akiongea na waamin kama wewe,waliokoka kama wewe,wana wa Mungu kama wewe,pengine nao walikua wakipitia hali ya magonjwa kama ww pamoja na kwamba wameokoka,akawaambia na kuwa kumbusha jamani eeh “Yeye mwenyewe alizichukua dhambi zetu katika mwili wake juu ya mti ,tukiwa wafu kwa mambo ya dhambi ,tuwe hai kwa mambo ya Haki,NA KWAKUPIGWA KWAKE MLIPONYWA”.

πŸ’₯Mpaka kufukia hapo tabasamu la ndugu yangu likawa dhahili kwangu na nikaona kila dalili ya muamko mpya ndani yake wa kuamini kwamba ni hakika Kristo alikufa kwa ajili yake na alipigwa kwa ajili yake na aliondoka na magonjwa yake yote(Kama vile ninavyokutaka ufurahi na utambue ww u mzima ,ndani yako huna uhalali wa kuishi na magonjwa)

πŸ’₯Nikamuuliza mpaka hapo jee unasababu halali ya ww kuendelea kuwa mgonjwa ambayo umeiona katika neno la Mungu kote tulipopitia?Akajibu kwa ujasiri wote kwamba hakuna uhalali wowote(Bila shaka hata ww unaafikiana nami kwamba huna uhalali wowote wa wewe kuumwa umwa,ww u mzima,kuumwa sio sehemu yako).

πŸ’₯ILA BADO AKANIULIZA LAKINI KWANINI NAUMWA?

πŸ”ΈNami bila kumjibu kiuinjilisti😊😊😊😊😊 nilimjibu kiualimu kama my Daddy Dickson.(Wewe pia nakujibu hivyo ili ujue nini tatizo).

πŸ”ΈKwakua ana mtoto yupo shule nilimuuliza swali,Je hivi ikitokea mwanao umeshamlipia ada shulen lakin akaja mwalimu mmoja na kumuambia mwanao kwamba Angel haujalipa ada ,pamoja na Angel kujitetea kwamba nilishalipiwa ada,lakin bado mwalim akamuambia haujalipa ada rudi nyumbani toka darasani jee Angel hatotoka na kukosa masomo na Kurudi nyumbani?
Akanijibu bila Shaka atatoka na kurudi nyumbani .Nikamuuliza jee kwann arudi nyumban naakati ameripa ada?Na jee akirudi kwako ww utafanyaje?AKAJIBU “NITAMPA RISITI AKAMUONESHE HUYO MWALIMU.”

πŸ’₯YAANI HILO JIBU ALILONIPA LILINIFANYA NIMPIGIE MAKOFI.
Kumbe Sasa Angel alisumbuliwa na Mwalumu na hata hakuwa na ujasiri wa Kusimama mbele ya mwalimu kwakua RISITI zake aliziacha nyumbani,risiti za Kumuonesha kwamba amekwishalipiwa ada?

πŸ’₯ANGEL BAADA YA KUCHUKUA RISITI AKARUDI SHULENI NA AKAWA NA UJASILI WA KUSIMAMA MBELE YA MWALIMU YULE ALIYEKUA AKIMSUMBUA,AKAMUONESHA ZILE RISITI NA MWALIMU TOKA HAPO AKAACHA KUMSUMBUA.

πŸ’₯Hapo tukapata jibu kwamba kumbe shida sio kulipiwa ada lakini jee ww uliyelipiwa unarisiti zako?Tatizo sio kuokoka na kuumwa jee unarisiti za Kuonesha Mbele y Huo Ugonjwa Kwamba Mimi nilishalipiwa Deni langu juu ya Suala la Magonjwa na Sina mkataba na wewe ugonjwa?

πŸ’₯Umeiacha wapi risiti yako?Risiti yako ni NENO halisi juu ya hicho unachopitia,jee Baba yako wa Mbinguni anasemaje juu ya Hiyo hali?Chukua hiyo Risiti Tembea nayo,Onesha kila sehem utakapotaka kusumbuliwa na Huyo Mwalimu Msumbufu nae Atanyamaza.

Shaloom
🍸A Blessed Son🍸
πŸ‡Deo DCKπŸ‡

Advertisements

Karibu kwenye Tovuti ya Kikristo... hapa utapata mafunzo Mbali mbali ya kukujenga kiimani ,kifahamu,kimazingira na hata kitabia Karibu Tena

Tagged with: , ,
Posted in Mafunzo

Toa mawazo,maoni

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out / Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out / Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out / Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out / Change )

Connecting to %s

yaliyopita
Ungana nasi kwenye kurasa yetu  ya facebook na like page yetu-kuweza kutangaza neno la bwana na utabalikiwa sana..kwa kazi yako kuu kwani thawabu yako mbinguni ni tele

Andika E-mail kwenye box hapo chini kisha Bonyeza (jiunge Hapa)na uweze kujiunga na tovuti hii kupitia e-mail yako utakayojisajilia,tutaweza kukupa kila taarifa,habari zinazojili kwenye hii blog yetu asanteni

Join 2,203 other followers

Upcoming Events

No upcoming events

%d bloggers like this: