BAADHI YA SABABU ZINAZOPELEKEA NDOA NYINGI KUVUNJIKA;

1.IBILISI, SHETANI YUKO KAZINI

Shetani Ni Adui Namba Moja Wa Ndoa. Unaweza Kuwa Unatumia Muda Mwingi Kuomba Upate Ndoa, Lakini Jiandae Kuomba Zaidi Kwa Ajili Ya Uhai Wa Ndoa Yako.
ALIVURUGA NDOA YA ADAMU NA MKEWE EVA Baada Ya Adamu Kumwacha Mkewe Peke Yake Na Adui Kutumia Huo Mlango Kuleta Matatizo. Mwisho Adamu Alirudi Kumlaumu Mungu Akisema “HUYU MWANAMKE ULIYENIPA NDIYE ALIYENIPONZA” Hii Ilikuwa Lawama, Lakini Ilikuja Baada Ya Adamu Kufungua Mlango Kwa Kutoambatana Na Msaidizi Wake Kwenye SHUGHULI ZA KULITUMIKIA KUSUDI LA MUNGU,
Njia Rahisi Ya Kumzuia Shetani Kwenye Ndoa Ni Kutompa Nafasi; IWENI WATU WA MSAMAHA, MKISAMEHEANA NINYI KWA NINYI KAMA KRISTO ALIVYOWASAMEHE NINYI.
Adui Pia Aliingia Kwenye Ndoa Ya Mtumishi Wa Mungu Ayubu, Mkewe Akamgeuka Na Kumwambia AMKUFURU MUNGU AFE!
SHETANI YUKO KAZINI, ANATAFUTA NDOA YA WAZEMBE FULANI (WASIOKESHA ILI KUMZUIA MWIZI ASIIBE) ILI AIHARIBU, BORA MUNGU ANGEKUFUNGUA MACHO YAKO UKAONA NAMNA ADUI ANAVYOIWINDA NDOA YAKO; PALE UNAPODHANI KUNA AMANI, NDIPO UHARIBIFU HUJA!

2.KUTOTIMIZA WAJIBU WENU KAMA MKE NA MME.

Watu Wengi Wanadhani Wanaingia Kwenye Ndoa KUPUMZIKA, Hawajui Kuwa WAMEONGEZA MAJUKUMU, Kuna Mtu Ameongezeka Anayehitaji UPENDO WAKO WA ZIADA Ambao Ulikuwa Hutoi. Akina Dada Wanasahau Kuwa Kuna Mtu Ambaye Ameongezeka Anayehitaji UMTII KAMA KUMTII KRISTO.
Lakini Pia Uwajibikaji Wa Mme KAMA KICHWA ( Kuona, Kusikia, Kunusa, Kuwaza, Kufikiri, Kufanya Maamuzi Na Kupitisha Maazimio Kama Kiongozi Mkuu Wa Familia), Na Swala La Mke Kujituma Kuwa Sawa Na Impsavyo Kwa Mujibu Wa Mithali 31:10-31.
Kutokana Na Wana Ndoa Wengi Kukazania Siku Ya Harusi Bila Kufikiri YAFAUATAYO NDANI YA NDOA, Ndio Maana Ndoa Nyingi Zinaanguka Kwa Urahisi.

3.WANANDOA AU MMOJA WAO KUPOTEZA USHIRIKA NA UHUSIANO NA MUNGU WA KARIBU.

Ndoa Ni Taasisi Iliyoanzishwa Rohoni Na Mungu Ambaye Ni Roho; Msingi Wake Lazima Uwe Wa Rohoni, Na Ujenzi Wake Toka Siku Ya Kwanza Ya Ndoa Unapaswa Kuwa Wa Kiroho Zaidi.
MKE NA MME LAZIMA MUWE NA MAOMBI YA PAMOJA, LAZIMA MUWE NA SIKU ZA KUFUNGA NA KUOMBA PAMOJA, LAZIMA MUWE NA UMOJA KATIKA KUMTUMIKIA MUNGU NA KUITEGEMEZA KAZI YA MUNGU PAMOJA; NDIYO MAANA HUWA NASISITIZA KWENYE MAFUNDISHO YANGU MENGI KUWA KABLA YA KUOA AU KUOLEWA NA MTU, HAKIKISHA KWANZA YUKO VIZURI SANA NA MUNGU.
Maana Akiwa Sawa Na Mungu, Atakutia Moyo Wakati Wa Changamoto, Atakuvuta Na Kukutegemeza Kwa BWANA, Na Utaimarika Na Kumfurahia Mungu Wako Zaidi.
KAMA MSINGI WA ROHONI WA NDOA YOYOTE UKO LEGELEGE, ANGUKO LAKE LINAKUJA!

4.MAKOSA YA KUCHAGUA MWENZI WA MAISHA KWA KUFUATA HISIA, HEKIMA NA MAWAZO YA WANADAMU PAMOJA NA VIGEZO VYA NJE ZAIDI KULIKO ALIVYO NDANI.

Wengi Huwa Wanapatwa Na Mshangao Au Kupigwa Na Butwaa Hasa Anapokuwa Tayari Ameingia Kwenye Ndoa Halafu Akagundua AMEOA LEAH BADALA YA RAHELI.
Kwa Hapo Hakuna Namna, Ndoa Ya Kikrsito HAIWEZI KUVUNJWA KWA SABABU KAMA HII, Lazima Ukubali Makosa Yako, Ujisamehe Mwenyewe, Umsamehe Mwenzako Na Uombe Kwa Mungu ALIMIMINE PENDO LAKE NDANI YAKO ILI UWEZE KUMPENDA HUYO MWENZIO KWA PENDO LA MUNGU, NA SI HISIA NA MAHABA TU TENA!
Jizoeze Kutafakari Na Kufikiri Namna Ambavyo Yakobo Alikubali HALI YA MAMBO NA KUMPOKEA LEAH Na Kuishi Naye Kama Mkewe Japo Alijua Ya Kuwa Hakuwa RAHELI.
Kumbuka Hata Kama Ni LEAH Hawezi Kukosa MEMA ALIYOBEBA; Kupitia Kwa LEAH Yalitoka Makabila 10 Kati Ya 12 Ya Israeli, Alikuwa Mama Wa Makabila Mengi.
Huyu LEAH Ndiye Aliyekuwa Mama Wa YUDA Ambaye Kupitia Kabila Hili, WAFALME WA TAIFA LA ISRAEL WALITOKA; NA KATIKA HUYU NDIPO ALIPOTOKA MWOKOZI YESU!
Ndani Ya LEAH Kuna Wafalme, Ndani Ya LEAH Kuna MWOKOZI. Usifanye UAMUZI WA HARAKA Kumwacha LEAH, Amebeba Mambo Makuu. Chukua Muda, Msome, Mjue Vizuri, Mwombee, Mpende Na Atakushangaza Kesho!

SIHITAJI KUWA NIMEOA ILI KUJUA HAYA; YAKO MAFUTA YANAYONIFUNDISHA; LIKO NENO AMBALO NI UZIMA WA MUNGU NDANI YANGU, NDANI YAKE IMO NURU, NAWEZA KUJUA KILA KITU MAANA YESU KRISTO NDANI YANGU NI HEKIMA YA MUNGU NA NGUVU YA MUNGU; NDANI YAKE HAZINA ZOTE ZA HEKIMA NA MAARIFA ZIMESITIRIKA!

Karibuni Harusini Kwangu 26/11/2016 Wote, Bila Kukosa!

Advertisements

Karibu kwenye Tovuti ya Kikristo... hapa utapata mafunzo Mbali mbali ya kukujenga kiimani ,kifahamu,kimazingira na hata kitabia Karibu Tena

Posted in Mafunzo
2 comments on “BAADHI YA SABABU ZINAZOPELEKEA NDOA NYINGI KUVUNJIKA;
  1. daniel kiondo says:

    ahsante sana kwa ujumbe mwingi tofautitofauti ambao kwa kweli unatujenga mno na tunainalika ila nasema kama ulivyosema shetani sio tishio ila dhanbi ndio tishio hapa kweli nakubali ila hebu nifafanulie hii nayo hivi unapofanya dhambi sio kama ni shetani amekuamlisha?au hapo ni mimi mwenyewe na sio shetani kweli?na kama ni mimi mwwnyewe ni kwa nini sasa nafanya dhambi?

  2. lillian kiwelu says:

    Hakika hii ni siri ambayo si rahisi kuielewa kama hutakua na utulivu,uzidi kubarikiwa baba angu na mafuta mabichi ya Roho Mtakatifu yawe juu yako kila siku.

Toa mawazo,maoni

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out / Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out / Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out / Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out / Change )

Connecting to %s

yaliyopita
Habari iliyotazamwa sana
Ungana nasi kwenye kurasa yetu  ya facebook na like page yetu-kuweza kutangaza neno la bwana na utabalikiwa sana..kwa kazi yako kuu kwani thawabu yako mbinguni ni tele

Andika E-mail kwenye box hapo chini kisha Bonyeza (jiunge Hapa)na uweze kujiunga na tovuti hii kupitia e-mail yako utakayojisajilia,tutaweza kukupa kila taarifa,habari zinazojili kwenye hii blog yetu asanteni

Join 2,212 other followers

Upcoming Events

No upcoming events

%d bloggers like this: