NJIA YA UHAKIKA YA KUFANIKIWA KWENYE MAISHA

Kuna Njia Moja Rahisi Ya Kukufanya Ufanikiwe Na Kustawi Kwenye Maisha; Njia Hiyo Ni KUWA NA MAJIBU YA MASWALI NA MAHITAJI YA WATU WENGINE WANAOKUZUNGUKA!
Kupitia Watu Haohao Unaowasaidia Au Kuwasogeza Mahali Kupitia Kidogo Unachowafanyia, Kuna Siku Na Wao Watakuwa Msaada Kwaki Kutimiza Ndoto Na Maono Yako; MTAJI MKUBWA WA KUKUFANIKISHA WEWE NI WATU, NA HAUTAWEZA KUWAPATA WATU KAMA HAUNA MAJIBU YA MASWALI NA CHANGAMOTO ZAO!

Yusufu Aliweza Kwenda IKULU KUWA WAZIRI MKUU Baada Ya Kuwa AMEWASAIDIA WALE WAFANYAKAZI WAWILI WA FARAO WALIOKUJA NA NDOTO ZAO [MASWALI] WASIZOZIJUA; Alipozitatua, Baada Ya Miaka 2 Yule Mmoja ALIMTAJA MBELE YA MFALME; Alisababisha Aitwe Toka Gerezani Kwenda KUTATUA CHANGAMOTO YA MFALME, NA MWISHO WA SIKU AKAWA WAZIRI MKUU!

Daudi Alikuwa Amepeleka Chakuila Kwa Ndugu Zake, Waliokuwa Kwenye Uwanja Wa Vita.
Alipofika Kule Akakuta KUNDI ZIMA/ JESHI ZIMA Limepoteza Amani Na Tumaini Kwa Kuwa LIMESHINDWA KUTATUA CHANGAMOTO IITWAYO GOLIATI… Daudi Alichukua Hatua YA kUJITOLEA KUTATUA HILO TATIZO Na Mwisho Wa Siku Akawa MTU MKUU NA MFALME WA ISRAELI Kupitia KUTATUA TATIZO NA CHANGAMOTO YA WENGINE!

Mungu Ametuumba Na Kutuweka Hapa Duniani, Lakini Mafanikio Na Ustawi Wetu Amevifunga Ndani Ya Maisha Ya Wengine. Hii Ndiyo Sababu Biblia INAHIMIZA SANA Kuhusu KUISHI VIZURI NA WATU Maana Kupitia Wao Tunaweza Kupata Miujiza Yetu; Maono Yetu Na Ndoto Zetu Zinaweza Kuwa Halisi Kama TUKIWA MAKINI NA KUWA NA USHIRIKA MZURI NA WATU!

Yesu Anasema, ” WAPENI WATU VITU; NANYI MTAPEWA….KIPIMO CHA KUJAA NA KUSHINDILIWA NA KUSUKWASUKA…NDICHO WATU WATAKACHOWAPIMIA VIFUANI MWENU” (Luka 6:38).
Kile Unachoweza Kuwatendea Wengine Na Kuwasogeza Hatua, Wafanyie, Na Wao Kupitia Hiyo MBEGU YAKO, Kuna Siku UTAVUNA Kipimo Cha KUJAA, KUSHINDILIWA NA KUSUKWASUKWA!

Yesu Alisistiza Kuhusu Mahusiano Mema Na Watu, Maana Anajua Siri Hii, Naye Anasema, ” YALE YOTE MNAYOPENDA KUTENDEWA NA WATU WENGINE, NINYI KWANZA WATENDEENI WAO” (Mathayo 7:12).

Kwa Msisitizo, Biblia Inatuambia, “TAFUTENI KWA BIDII KUWA NA AMANI NA WATU WOTE, NA HUO UTAKATIFU, AMBAO PASIPO HUO HAKUNA ATAKAYEMWONA MUNGU” (Waebrania 12:14).
Kufanikiwa Hapa Duniani Inategemea Na Namna Ambavyo UMEKUWA BARAKA KWA WENGINE, Kupitia Kwao Nawe UTAFANIKIWA NA KUTIMIZA KUSUDI LAKO… Na Kuingia Mbinguni, Kumwona Mungu Ni Matokeo Ya Kuwa Watakatifu!

Hivyo “USICHOKE KUTENDA MEMA, KWA KILA MTU KWA KADRI UPATAVYO NAFASI, HASAHASA JAMII YA YA WAAMINIO”
Usiwe Na Ubaguzi Kwenye Kusaidia Watu, Hata Kama Haufahamiani Nao, Hata Kama Ni Wageni Kwako, Wewe Wapokee Na Kuwatendea Mema… Maana “WENGINE PASIPO KUJUA WAMEWAPOKEA MALAIKA”

Advertisements

Karibu kwenye Tovuti ya Kikristo... hapa utapata mafunzo Mbali mbali ya kukujenga kiimani ,kifahamu,kimazingira na hata kitabia Karibu Tena

Tagged with: , ,
Posted in Mafunzo

Toa mawazo,maoni

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out / Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out / Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out / Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out / Change )

Connecting to %s

yaliyopita
Habari iliyotazamwa sana
Ungana nasi kwenye kurasa yetu  ya facebook na like page yetu-kuweza kutangaza neno la bwana na utabalikiwa sana..kwa kazi yako kuu kwani thawabu yako mbinguni ni tele

Andika E-mail kwenye box hapo chini kisha Bonyeza (jiunge Hapa)na uweze kujiunga na tovuti hii kupitia e-mail yako utakayojisajilia,tutaweza kukupa kila taarifa,habari zinazojili kwenye hii blog yetu asanteni

Join 2,212 other followers

Upcoming Events

No upcoming events

%d bloggers like this: