JIFUNZE VITU VYA MUHIMU 


Siku Nikikukuta Unamwinua Shetani Na Kumtukuza Kwa Kauli Zako Nitachukua Kiboko Nikuchape Kabisa… Zile Kauli Za Kusema Shetani Ni Hatari Sana, Ana Nguvu Sana… Shetani Anashindana Na Yesu Na Nyingine Za Aina Hii Ni Za Watoto Wachanga!

Shetani Ni Malaika Tu Muasi, Si Zaidi Ya Hapo. Na Kubwa Zaidi Amepoteza Utukufu Wake Mara Baada Ya Kufukuzwa Mbinguni Na Mahali Pake Kuondolewa!

Ukisoma Ufunuo 12:7 Na Kuendelea, Tunaona Vita Iliyokuwa Mbinguni Wakati Shetani Alipoasi… Biblia Inamtaja Malaika Mmoja Tu Aitwaye Mikaeli, Aliongoza Malaika Wenzie Kumng’oa Shetani Na Malaika Zake Waasi… Mungu Hakushiriki Kabisa Katika Kumng’oa Shetani Mbinguni, Maana Shetani Si Saizi Ya Mungu, Ni Saizi Ya Malaika Tu… Mungu Alikaa Kama Mtazamaji Akishuhudia Jinsi Shetani Anavyopokea Kipigo!
Yesu Alipokuja Na Kufa Msalabani, Alishuka Hata Kuzimu, Akamnyanganya Shetani FUNGUO [Alama Ya Mamlaka Ya Kufunga Na Kufungua Mambo] Na Akatupatia Sisi Tumilki Na Kutawala Kwa Niaba Yake; Tunalolifunga, Linafungwa Mbinguni, Tunalolifungulia, Linafunguliwa Duniani… Shetani Si Tishio Kwetu. Kila Aliyeokoka Ana Kauli Ya Mwisho Dhidi Ya Shetani Na Majeshi Yake Yote (Luka 10:19), Inategemea Unayatumiaje Mamlaka Husika!
Shetani Hatakushinda Hata Siku Moja Mpaka Pale Utakapomfungulia Mlango Na Kumpa Nafasi… Ila Kama Ukimpinga Ukiwa Thabiti Katika Imani, Atakukimbia!

Ukaribu Wako Na Mungu Unaamua Kiasi Cha Nguvu Na Mamlaka Yako Dhidi Ya Shetani…” Basi Mkaribieni Mungu, Mpingeni Shetani Naye Atawakimbia” (Yakobo 4:7)!

Mwalimu Dickson Cornel Kabigumila

Advertisements

Karibu kwenye Tovuti ya Kikristo... hapa utapata mafunzo Mbali mbali ya kukujenga kiimani ,kifahamu,kimazingira na hata kitabia Karibu Tena

Tagged with: , ,
Posted in Mafunzo

Toa mawazo,maoni

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out / Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out / Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out / Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out / Change )

Connecting to %s

yaliyopita
Habari iliyotazamwa sana
Ungana nasi kwenye kurasa yetu  ya facebook na like page yetu-kuweza kutangaza neno la bwana na utabalikiwa sana..kwa kazi yako kuu kwani thawabu yako mbinguni ni tele

Andika E-mail kwenye box hapo chini kisha Bonyeza (jiunge Hapa)na uweze kujiunga na tovuti hii kupitia e-mail yako utakayojisajilia,tutaweza kukupa kila taarifa,habari zinazojili kwenye hii blog yetu asanteni

Join 2,215 other followers

Upcoming Events

No upcoming events

%d bloggers like this: