MFUNGO WA SIKU 40, (Masaa 12 kutwa nzima),(Day 3)

ABC KAHAMA & DETRIM,
Pamoja na Mwalimu Dickson Cornel Kabigumila,

UJUMBE MKUU: ROHO MTAKATIFU NA WEWE

SIKU YA TATU: ROHO MTAKATIFU NA AFYA YAKO.

https://i1.wp.com/mywellnessafrica.com/wp-content/uploads/2016/07/120116084646-pain-sleep-black-man-bed-headache-story-top.jpg“Lakini, ikiwa ROHO YAKE YEYE ALIYEMFUFUA YESU KATIKA WAFU anakaa ndani yenu, Yeye aliyemfufua Kristo Yesu katika wafu ATAIHUISHA NA MIILI YENU ILIYO KATIKA HALI YA KUFA, KWA ROHO WAKE ANAYEKAA NDANI YENU”
(Warumi 8:11).

MAMBO YA KUJIFUNZA;

1. Kila mtu aliyeokoka (kuzaliwa mara ya pili), ameokoka kwa NGUVU ZA ROHO MTAKATIFU, yaani Roho Mtakatifu ndiye aliyekuwa NGUVU YA KUTUZAA KATIKA UFALME WA MUNGU (Yohana 3:3,5).

2. Kila aliye mali ya Kristo, Aliyemuamini Yesu, ANAYE ROHO WA MUNGU ndani yake, ambaye ni kama MITO YA MAJI YALIYO HAI, yanayotiririka ndani ya Mwamini (Yohana 7:37-39).

3. Kila mtu aliyeokoka ANA ROHO YULEYULE ALIYEMFUFUA YESU NDANI YAKE, na kazi mojawapo aliyonayo ni KUHAKIKISHA MWILI WA ALIYEOKOKA UNAKAA KATIKA UZIMA NA AFYA ISIYO NA MIGOGORO (Warumi 8:11).

4. Usipojua Kweli hii ya kuwa HUYO ROHO WA MUNGU ULIYEMBEBA, NDIYE ALIYEMTOA YESU KIFONI, NA NDIYE ALIYEPONYA VIDONDA NA MAKOVU YOTE ALIYOKUWA NAYO BAADA YA KUPIGWA MIJELEDI, utabaki UKITESWA NA SHETANI NA MAGONJWA ILHALI TAYARI UNA MPONYAJI, ROHO MTAKATIFU NDANI YAKO (Hosea 4:6, Isaya 5:13, Yohana 8:32).

5. Mwili wako ni HEKALU LA ROHO MTAKATIFU (makazi halali ya Roho Mtakatifu), ukikubali MAGONJWA YAPANGE HUMO ni uamuzi wako!
Ulipaswa KUYAPAMBANISHA MAGONJWA MWILINI MWAKO NA MMILKI WA MWILI WAKO AITWAYE ROHO MTAKATIFU (1Wakorintho 3:16-17, 1Wakorintho 6:15,17).

ZINGATIA HAYA

1. Una Roho wa Mungu ambaye ni bingwa wa kutibu ugonjwa wowote mwilini mwako.

2. Roho Mtakatifu ndiye mmilki halali wa mwili wako, magonjwa na maradhi ni wahamiaji haramu, muambie Roho wa Mungu awashughulikie na kuwaharibu (1Wakorintho 3:16-17).

3. Hukupewa Roho wa Mungu kwa ajili ya kukusaidia kuomba tu bali kuhakikisha afya yako haiwi na mgogoro (Warumi 8:11).

UKIAMINI UGONJWA KULIKO KWELI YA NENO LA MUNGU, SHETANI ATAKUUA.

Siku njema,
Tukutane kesho day 4.

Advertisements

Karibu kwenye Tovuti ya Kikristo... hapa utapata mafunzo Mbali mbali ya kukujenga kiimani ,kifahamu,kimazingira na hata kitabia Karibu Tena

Tagged with: , , ,
Posted in Mafunzo

Toa mawazo,maoni

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out / Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out / Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out / Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out / Change )

Connecting to %s

yaliyopita
Habari iliyotazamwa sana
Ungana nasi kwenye kurasa yetu  ya facebook na like page yetu-kuweza kutangaza neno la bwana na utabalikiwa sana..kwa kazi yako kuu kwani thawabu yako mbinguni ni tele

Andika E-mail kwenye box hapo chini kisha Bonyeza (jiunge Hapa)na uweze kujiunga na tovuti hii kupitia e-mail yako utakayojisajilia,tutaweza kukupa kila taarifa,habari zinazojili kwenye hii blog yetu asanteni

Join 2,212 other followers

Upcoming Events

No upcoming events

%d bloggers like this: