MFUNGO WA SIKU 40, (MASAA 12 KUTWA)[SIKU YA 4]

WA ABC KAHAMA & DETRIM,
WA MWALIMU DICKSON CORNEL KABIGUMILA NA MARAFIKI.

UJUMBE MKUU: ROHO MTAKATIFU NA WEWE

SIKU YA NNE: ROHO MTAKATIFU ANAWEZA KUKUSIMAMISHA TENA.

https://i1.wp.com/www.clipartkid.com/images/420/christian-women-praying-lord-teach-me-to-pray-KlA5rW-clipart.jpg“Naye aliposema nami, ROHO IKANIINGIA, IKANISIMAMISHA; Nikamsikia Yeye aliyesema nami.”
(Ezekieli 2:2).

“Ndipo ROHO ILE IKANIINGIA, IKANISIMAMISHA KWA MIGUU YANGU…”
(Ezekieli 3:24).

MAMBO YA KUJIFUNZA

1. Kila neno au maneno yana roho ya Ibilisi au ya Mungu nyuma yake.
Hiyo roho au Roho inaweza kumuingia mtu.
Ikiwa ya Mungu ITAKUINUA NA KUKUSIMAMISHA TENA KWENYE MIGUU YAKO. Ndiyo maana unaweza kusikia mafundisho, mahubiri, somo au kusoma kitabu cha mtumishi wa Mungu na UKATIWA NGUVU NA KUSIMAMA TENA MAHALI AMBAPO ULIKUWA UMEKWISHA KATA TAMAA.
Vivyo hivyo kuna maneno unaweza kuletewa au kusikia na kuanzia muda ule amani ikapotea, ukaingiwa na uchungu, tumbo likaanza kuuma, pressure ikapanda, mapigo ya moyo yakaenda mbio, ukashindwa kupumua… UJUE roho chafu IMEKUINGIA ILI KUKUANGUSHA AU KUKUMALIZA kupitia maneno au habari mbaya ulizosikia, kusoma au kuambiwa.
UWE MAKINI, USIRUHUSU KILA MANENO YAINGIE NDANI YAKO.

2. Neno la Mungu ni ROHO NA UZIMA (Yohana 6:63).
Kadri unavyojipa muda kusikiliza mafundisho, kutazama mafundisho, kusoma mafundisho, kusoma vitabu vya watumishi wa kweli wa Mungu, kusoma na kutafakari NENO LA MUNGU, kuna ROHO WA UZIMA anaingia ndani yako kukusimamisha na kukutia nguvu kwenye eneo husika.
Ongeza bidii ya kukaa kwenye mafundisho na Neno la Mungu, kuna Roho inakuingia na kukusimamisha.

3. Utendaji wa Roho wa Mungu (kuja na kukuinua) unategemea bidii yako ya kusikia SAUTI YA NENO LA MUNGU.
Ezekieli anasema, Mungu aliposema naye, ndipo Roho ilipomwingia na kumsimamisha kwa miguu yake.
Kama unataka kusimama katika eneo lolote ulilokuwa umeanguka au kuporomoka, fungua mlango wa Neno la Mungu kuingia ndani yako ili Roho wake atende kazi ndani yako na kukuinua.
Roho wa Mungu hawezi kufanya lolote bila Neno la Mungu (Waefeso 6:17).
Mtengenezee Roho Mtakatifu mazingira ya kukusimamisha kwa miguu yako, kwa kukaa na Neno na mafundisho sahihi muda mwingi.

MAOMBI

1. Muombe Roho Mtakatifu akusaidie kuzijua siri na mafumbo ya Mungu, ili kupitia hizo ufanye mambo ambayo macho hayajawahi kuona, masikio hayajawahi kusikia na ambayo hayajawahi kuwa moyoni mwa mtu yeyote (1Wakorintho 2:9-13).

2. Muombe Roho Mtakatifu akusimamishe kwa miguu yako kila unapokutana na Neno la Mungu (Ezekieli 2:2, Ezekieli 3:24).

3. Muombe Roho Mtakatifu akusaidie kuitwaa ngao ya imani na kuzima mishale yote ya moto ya adui, inayopitia kwenye maneno mabaya dhidi yako (Waefeso 6:16).

Nikutakie siku njema,
Umebarikiwa,
Tukutane kesho day 5,
Mwalimu Dickson Cornel Kabigumila,
Makanisa ya ABC na DETRIM.

Advertisements

Karibu kwenye Tovuti ya Kikristo... hapa utapata mafunzo Mbali mbali ya kukujenga kiimani ,kifahamu,kimazingira na hata kitabia Karibu Tena

Tagged with: , , ,
Posted in Mafunzo
One comment on “MFUNGO WA SIKU 40, (MASAA 12 KUTWA)[SIKU YA 4]
  1. EZEKIEL SIMON MHONZWA says:

    Nimepokea,Nimeelewa, na Nitalifanyia kazi.Nitamfanya Roho Mtakatifu asikie Sauti ya Neno la Mungu.Amen.Tia Ishara na Ajabu-ABC.

Toa mawazo,maoni

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out / Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out / Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out / Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out / Change )

Connecting to %s

yaliyopita
Habari iliyotazamwa sana
Ungana nasi kwenye kurasa yetu  ya facebook na like page yetu-kuweza kutangaza neno la bwana na utabalikiwa sana..kwa kazi yako kuu kwani thawabu yako mbinguni ni tele

Andika E-mail kwenye box hapo chini kisha Bonyeza (jiunge Hapa)na uweze kujiunga na tovuti hii kupitia e-mail yako utakayojisajilia,tutaweza kukupa kila taarifa,habari zinazojili kwenye hii blog yetu asanteni

Join 2,215 other followers

Upcoming Events

No upcoming events

%d bloggers like this: