MFUNGO WA SIKU 40, (MASAA 12 KUTWA)[SIKU YA 5]

ABC KAHAMA & DETRIM,
MWALIMU DICKSON CORNEL KABIGUMILA NA MARAFIKI.

UJUMBE MKUU: ROHO MTAKATIFU NA WEWE.

https://i0.wp.com/www.christchurchcolumbia.org/v1/wp-content/uploads/2016/03/Dollarphotoclub_92483283.jpgSIKU YA TANO: ROHO MTAKATIFU KIONGOZI WAKO.

“Lakini yeye atakapokuja, HUYO ROHO WA KWELI, ATAWAONGOZA NA KUWATIA KATIKA KWELI YOTE….”
(Yohana 16:13).

“Kwa maana wale wote WANAOONGOZWA NA ROHO WA MUNGU hao ndio wana wa Mungu…”
(Warumi 8:14).

“Nao walipokuwa wakifunga na kumfanyia Mungu ibada, ROHO MTAKATIFU AKASEMA, nitengeeni Sauli na Barnaba kwa ajili ya ile kazi niliyowaitia…”
(Matendo 13:2).

“Naye Yesu hali amejaa Roho, alirudi toka Yordani, AKAONGOZWA NA ROHO…”
(Luka 4:1).

MAMBO YA KUJIFUNZA;

1. Bila uongozi wa Roho Mtakatifu, hautaishi kwa kiwango cha MWANA WA MUNGU, utakuwa na maisha madogo kama ya wanadamu wengine wasiomjua Mungu (Warumi 8:14).

2. Bila uongozi wa Roho Mtakatifu hautaweza kuyajua mapenzi ya Mungu kwako na mipango aliyonayo kwako, maana Yeye pekee huchukua mbinguni yampasayo mtu na kumletea (Yohana 16:13-15).

3. Yesu mwenyewe amefanikiwa kuweka rekodi ya aina yake kwa sababu ya uongozi wa Roho Mtakatifu, mimi na wewe hatuwezi kuwa watu wa aina yake bila uongozi wa Roho Mtakatifu (Luka 4:1, 14).

4. Bila uongozi wa Roho Mtakatifu ni ngumu sana kujua hatua na njia ipi ya kuifuata kati ya nyingi maishani mwetu (Isaya 48:17).

MAOMBI;

1. Omba Mungu akusaidie uwe msikivu na mtiifu kwa Roho Mtakatifu na maelekezo yake kwako.

2. Muombe Roho Mtakatifu akusaidie kuyajua mawazo mema na ya amani, aliyonayo Mungu juu yako.

Nikutakie siku njema,
Ubarikiwe sana,

Mwalimu Dickson Cornel Kabigumila
ABC & DETRIM,

Advertisements

Karibu kwenye Tovuti ya Kikristo... hapa utapata mafunzo Mbali mbali ya kukujenga kiimani ,kifahamu,kimazingira na hata kitabia Karibu Tena

Tagged with: , ,
Posted in Mafunzo

Toa mawazo,maoni

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out / Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out / Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out / Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out / Change )

Connecting to %s

yaliyopita
Habari iliyotazamwa sana
Ungana nasi kwenye kurasa yetu  ya facebook na like page yetu-kuweza kutangaza neno la bwana na utabalikiwa sana..kwa kazi yako kuu kwani thawabu yako mbinguni ni tele

Andika E-mail kwenye box hapo chini kisha Bonyeza (jiunge Hapa)na uweze kujiunga na tovuti hii kupitia e-mail yako utakayojisajilia,tutaweza kukupa kila taarifa,habari zinazojili kwenye hii blog yetu asanteni

Join 2,212 other followers

Error: Twitter did not respond. Please wait a few minutes and refresh this page.

Upcoming Events

No upcoming events

%d bloggers like this: