MFUNGO WA SIKU 40, (MASAA 12 KUTWA)[SIKU YA 6]

 

UJUMBE MKUU: ROHO MTAKATIFU NA WEWE

http://www.deidrehavrelock.com/wp-content/plugins/vslider/timthumb.php?src=%2Fwp-content%2Fuploads%2F2013%2F09%2F11.png&w=560&h=250&zc=1&q=80

SIKU YA SITA: ROHO MTAKATIFU NA SIRI ZA KUKUFANYA UWE MTU WA AJABU DUNIANI.

“Lakini, kama ilivyoandikwa, MAMBO AMBAYO MACHO HAYAKUONA, MASIKIO HAYAKUSIKIA, WALA HAYAKUINGIA MIOYONI MWA MTU AWAYE YOTE, MAMBO AMBAYO MUNGU AMETUANDALIA SISI TUMPENDAO. Lakini MUNGU AMETUFUNULIA MAMBO HAYO KWA ROHO. Kwa maana Roho huchunguza yote HATA MAFUMBO YA MUNGU (SIRI ZA NDANI MNO ZA MUNGU)… Lakini sisi tumepewa ROHO WA MUNGU, MAKUSUDI TUPATE KUYAJUA YALE TULIYOKIRIMIWA BURE NA MUNGU…”
(1Wakorintho 2:9-13).

“Kwa maana NAYAJUA MAWAZO NINAYOWAWAZIA NINYI, NI MAWAZO YA AMANI WALA SI YA MABAYA, KUWAPA NINYI TUMAINI KATIKA SIKU ZENU ZA MWISHO…”
(Yeremia 29:11).

MAMBO YA KUJIFUNZA;

1. Kuna aina ya maisha na kiwango cha maisha ambacho hajawahi kuishi au kukiwaza mtu yeyote ambacho Mungu amekikusudia kiwe chetu tumpendao, na ni Roho Mtakatifu pekee anaweza kukichukua moyoni kwa Mungu na kukileta maishani mwetu.

2. Baada ya kuokoka na kumpata Roho Mtakatifu, huyu Roho Mtakatifu anafanya kazi ya kutusaidia kujua mambo ambayo Mungu ametukirimia, ili kutusaidia kuishi maisha ya kiwango sahihi tunachostahili.

3. Kuna mawazo na mipango maalum kwa kila mtu ambayo tayari Mungu amempangia na kumuwazia kila mtu, lakini bila Roho Mtakatifu, hauwezi kuyajua.

4. Kila mtu mkuu kwenye Biblia ameweka rekodi kubwa na kufanya mambo makubwa kwa sababu ya Roho Mtakatifu kumpa siri za kumtofautisha na dunia yake.

MAOMBI;

1. Muombe Roho Mtakatifu achukue siri kutoka kwa Mungu na Bwana Yesu kuhusu maisha yako, na akupashe habari (Yohana 16:13-15).

2. Muombe Roho Mtakatifu akusaidie kuzijua siri za Ufalme wa Mungu zitakazokusaidia kuwa mtu mkuu (Marko 4:11).

Nikutakie siku njema,

Mwalimu Dickson Cornel Kabigumila
ABC & DETRIM,

Advertisements

Karibu kwenye Tovuti ya Kikristo... hapa utapata mafunzo Mbali mbali ya kukujenga kiimani ,kifahamu,kimazingira na hata kitabia Karibu Tena

Tagged with: , , , ,
Posted in Mafunzo

Toa mawazo,maoni

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out / Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out / Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out / Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out / Change )

Connecting to %s

yaliyopita
Habari iliyotazamwa sana
Ungana nasi kwenye kurasa yetu  ya facebook na like page yetu-kuweza kutangaza neno la bwana na utabalikiwa sana..kwa kazi yako kuu kwani thawabu yako mbinguni ni tele

Andika E-mail kwenye box hapo chini kisha Bonyeza (jiunge Hapa)na uweze kujiunga na tovuti hii kupitia e-mail yako utakayojisajilia,tutaweza kukupa kila taarifa,habari zinazojili kwenye hii blog yetu asanteni

Join 2,212 other followers

Upcoming Events

No upcoming events

%d bloggers like this: