MFUNGO WA SIKU 40, (MASAA 12 KUTWA)[SIKU YA 11]

UJUMBE MKUU: ROHO MTAKATIFU NA WEWE.

https://i1.wp.com/www.anchoryourlife.com/images/reach.jpg

SIKU YA KUMI NA MOJA: ROHO MTAKATIFU, MWALIMU WAKO WA MAISHA.

“Lakini huyo msaidizi, huyo ROHO MTAKATIFU, ambaye Baba atampeleka kwa jina langu, ATAWAFUNDISHA YOTE, NA KUWAKUMBUSHA YOTE NILIYOWAAMBIA.”
(Yohana 14:26).

“Kwa kuwa ROHO MTAKATIFU ATAWAFUNDISHA saa ile ile yawapasayo kusema.”
(Luka 12:12).

“Na watakapowachukua ninyi na kuwasaliti, msitafakari kwanza mtakayosema, lakini lolote mtakalopewa saa ile, lisemeni; maana si ninyi msemao, bali ni ROHO MTAKATIFU.”
(Marko 13:11).

“Ukawapa na ROHO YAKO MWEMA ILI KUWAELIMISHA, wala hukuwanyima mana vinywani mwao, tena ukawapa maji kwa ajili ya kiu yao.”
(Nehemia 9:20).

“Nanyi, Mafuta yale mliyoyapata kwake (Roho Mtakatifu), yanakaa ndani yenu, wala hamna haja ya mtu kuwafundisha; Lakini kama mafuta yake yanavyowafundisha habari za mambo yote, tena ni kweli wala si uongo, na kama yalivyowafundisha, kaeni ndani yake.”
(1Yohana 2:27).

MAMBO YA KUJIFUNZA

1. Mara baada ya kuokoka hauko peke yako, Mungu aliye hai yuko nawe kupitia Roho wake Mtakatifu (Yohana 14:16-17).

2. Roho huyu Mtakatifu anajua hatua za maisha yako, na amekuja kwako kukufundisha na kukuonyesha njia ya kuiendea katika kila eneo la maisha yako (Zaburi 32:8).

3. Huyu Roho wa Mungu ndani yako ni Mafuta maalum yanayokufundisha kila kitu maishani (1Yohana 2:27).

4. Mungu amekupa Roho wake Mtakatifu ili akuelimishe, akupe mana na maji (Nehemia 9:20).

5. Hata unapokuwa mahali ambapo hujui cha kusema au kufanya, Roho wa Mungu uliyepewa ni Mwalimu atakayekufundisha (Luka 12:12, Marko 13:11).

MAOMBI

1. Muombe Mungu akusaidie kutunza ushirika na Roho wake Mtakatifu, ili uweze kufaidi kila kitu alichonacho cha kukusaidia kwenye maisha.

2. Muombe Mungu akusaidie kukumbuka ukweli huu kwamba; Hauko peke yako, una mwalimu Roho Mtakatifu.

Advertisements

Karibu kwenye Tovuti ya Kikristo... hapa utapata mafunzo Mbali mbali ya kukujenga kiimani ,kifahamu,kimazingira na hata kitabia Karibu Tena

Tagged with: , ,
Posted in Mafunzo

Toa mawazo,maoni

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out / Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out / Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out / Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out / Change )

Connecting to %s

yaliyopita
Habari iliyotazamwa sana
Ungana nasi kwenye kurasa yetu  ya facebook na like page yetu-kuweza kutangaza neno la bwana na utabalikiwa sana..kwa kazi yako kuu kwani thawabu yako mbinguni ni tele

Andika E-mail kwenye box hapo chini kisha Bonyeza (jiunge Hapa)na uweze kujiunga na tovuti hii kupitia e-mail yako utakayojisajilia,tutaweza kukupa kila taarifa,habari zinazojili kwenye hii blog yetu asanteni

Join 2,212 other followers

Upcoming Events

No upcoming events

%d bloggers like this: