MFUNGO WA SIKU 40, (MASAA 12 KUTWA)[SIKU YA 10]

UJUMBE MKUU: ROHO MTAKATIFU NA WEWE

https://i1.wp.com/www.anchoryourlife.com/images/reach.jpg

SIKU YA KUMI: ROHO MTAKATIFU NA UBORA WA MAOMBI YAKO.

“Kadhalika ROHO naye hutusaidia udhaifu wetu, kwa maana HATUJUI KUOMBA ITUPASAVYO, lakini ROHO MWENYEWE HUTUOMBEA kwa kuugua kusikoweza kutamkwa. Na yeye aichunguzaye mioyo aijua NIA YA ROHO ILIVYO, KWAKUWA HUWAOMBEA WATAKATIFU KAMA APENDAVYO MUNGU.”
(Warumi 8:26-27).

“Kwa sala zote na maombi, mkisali kila wakati katika ROHO, Mkikesha katika jambo hilo na kudumu katika kuwaombea watakatifu wote”
(Waefeso 6:18).

“Nami nitawamwagia watu wa nyumba ya Daudi, na wenyeji wa Yerusalemu, ROHO YA NEEMA NA KUOMBA…”
(Zekaria 12:10).

“Bali ninyi, wapenzi, mkijijenga juu ya imani yenu iliyo takatifu sana, NA KUOMBA KATIKA ROHO MTAKATIFU.”
(Yuda 1:20).

MAMBO YA KUJIFUNZA

1. Neema na maombi ni Roho ya Mungu mwenyewe (Zekaria 12:10), Yesu alijaa Neema na Kweli (Yohana 1:14), lakini pia alikuwa amejaa maombi (Waebrania 5:7).
Kila mtu wa neema ni mtu wa maombi.

2. Njia rahisi ya kuongeza neema juu ya maisha yako ni kuwa mwombaji, na vyote hivi viko chini ya Roho wa neema na anayetusaidia kuomba, Roho Mtakatifu (Waebrania 10:29, Warumi 8:26-27, Waebrania 4:16).

3. Uombaji unaomgusa Mungu na kuleta mpenyo na majibu haraka na yaliyo bora ni ule unaofanywa na Roho Mtakatifu ndani yetu (Warumi 8:26-27).

4. Kuomba katika Roho Mtakatifu ni muhimu sana katika kujenga imani yetu iliyo takatifu sana (Yuda 1:20).

MAOMBI

1. Muombe Roho Mtakatifu akusaidie kila wakati uwe mtu wa maombi (Waefeso 6:18).

2. Muombe Mungu akumwagie Roho ya neema na maombi, ili uweze kutembea katika neema na kuomba ikupasavyo (Zekaria 12:10).

Umebarikiwa sana,

Advertisements

Karibu kwenye Tovuti ya Kikristo... hapa utapata mafunzo Mbali mbali ya kukujenga kiimani ,kifahamu,kimazingira na hata kitabia Karibu Tena

Tagged with: ,
Posted in Mafunzo

Toa mawazo,maoni

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out / Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out / Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out / Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out / Change )

Connecting to %s

yaliyopita
Habari iliyotazamwa sana
Ungana nasi kwenye kurasa yetu  ya facebook na like page yetu-kuweza kutangaza neno la bwana na utabalikiwa sana..kwa kazi yako kuu kwani thawabu yako mbinguni ni tele

Andika E-mail kwenye box hapo chini kisha Bonyeza (jiunge Hapa)na uweze kujiunga na tovuti hii kupitia e-mail yako utakayojisajilia,tutaweza kukupa kila taarifa,habari zinazojili kwenye hii blog yetu asanteni

Join 2,212 other followers

Upcoming Events

No upcoming events

%d bloggers like this: