MFUNGO WA SIKU 40, (MASAA 12 KUTWA)[SIKU YA 12]

UJUMBE MKUU: ROHO MTAKATIFU NA WEWE

https://i1.wp.com/media.salemwebnetwork.com/cms/IB/31797-praying-woman-outside-1200.630w.tn.jpg

SIKU YA KUMI NA MBILI: ROHO MTAKATIFU MUUMBAJI

“Waipeleka ROHO YAKO, WANAUMBWA. Nawe waufanya upya uso wa nchi.”
(Zaburi 104:30).

“ROHO YA MUNGU IMENIUMBA, NA PUMZI ZA MWENYEZI HUNIPA UHAI.”
(Ayubu 33:4).

“Malaika akajibu akamwambia, ROHO MTAKATIFU ATAKUJIA JUU YAKO, NA NGUVU ZAKE ALIYE JUU ZITAKUFUNIKA KAMA KIVULI; kwa sababu hiyo HICHO KITAKACHOZALIWA kitaitwa kitakatifu, Mwana wa Mungu.”
(Luka 1:35).

MAMBO YA KUJIFUNZA;

1. Roho wa Mungu ni muumbaji tangu Mwanzo, alikuwa akiyaumba yote aliyotamka Mungu (Mwanzo 1:2-3).

2. Roho huyu muumbaji, ndiye aliyemuumba Yesu katika tumbo la Mariamu (Luka 1:35).

3. Huyu Roho Mtakatifu ndiye aliyekuwa anaumba macho ya vipofu, masikio ya viziwi, ngozi na viungo vya wakoma na kila muujiza wa uumbaji ambao YESU na Mitume walifanya!

4. Huyu Roho wa Mungu ameletwa kwako ili kila kitu maishani mwako kiumbwe na dunia yako iwe nyingine, mtumie vizuri (Zaburi 104:30).

MAOMBI

1. Muombe Roho Mtakatifu akuumbe upya, akuumbie moyo mpya na roho iliyotulia ndani yako (Zaburi 51:10).

2. Muombe Roho Mtakatifu ayaumbe upya maisha yako (Ayubu 33:4, Zaburi 104:30).

Umebarikiwa sana,

Advertisements

Karibu kwenye Tovuti ya Kikristo... hapa utapata mafunzo Mbali mbali ya kukujenga kiimani ,kifahamu,kimazingira na hata kitabia Karibu Tena

Tagged with: , , ,
Posted in Mafunzo

Toa mawazo,maoni

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out / Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out / Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out / Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out / Change )

Connecting to %s

yaliyopita
Habari iliyotazamwa sana
Ungana nasi kwenye kurasa yetu  ya facebook na like page yetu-kuweza kutangaza neno la bwana na utabalikiwa sana..kwa kazi yako kuu kwani thawabu yako mbinguni ni tele

Andika E-mail kwenye box hapo chini kisha Bonyeza (jiunge Hapa)na uweze kujiunga na tovuti hii kupitia e-mail yako utakayojisajilia,tutaweza kukupa kila taarifa,habari zinazojili kwenye hii blog yetu asanteni

Join 2,212 other followers

Upcoming Events

No upcoming events

%d bloggers like this: