MFUNGO WA SIKU 40, (MASAA 12 KUTWA)[SIKU YA 7]

UJUMBE MKUU: ROHO MTAKATIFU NA WEWE.

https://i1.wp.com/www.limerickpost.ie/site/wp-content/uploads/bigstock-Praying-hands-70114342.jpgSIKU YA SABA: ROHO WA MUNGU NA UPENDO WA KIMUNGU NDANI YAKO.

“…kwa maana PENDO LA MUNGU LIMEKWISHA KUMIMINWA KATIKA MIOYO YETU NA ROHO MTAKATIFU TULIYEPEWA SISI”
(Warumi 5:5).

“Lakini TUNDA LA ROHO NI UPENDO…”
(Wagalatia 5:22).

MAMBO YA KUJIFUNZA;

1. Amri kuu ni upendo; kumpenda Mungu na kumpenda kila mtu (rafiki au adui) kama nafsi zetu.
Aliyetimia katika upendo ametimia katika amri zote, maana sheria ya upendo ina nguvu kuliko sheria zote za torati.

2. Upendo ni deni pekee ambalo Mungu ameruhusu tuendelee kuwiwa/kudaiwa, kila siku tuna deni la kumpenda na kuwapenda watu wote wema na waovu (Warumi 13:8).

3. Kila mtu aliyeokoka amekwisha kumpokea Roho Mtakatifu, na huyu Roho wa Mungu amekwisha kulimimina Pendo lake mioyoni mwetu. Hatuwezi kujitetea kwamba hatuwezi kuwapenda baadhi ya watu walio wabaya au waliotuumiza, KILA ALIYEOKOKA AMEMIMINIWA PENDO LA MUNGU LA KUWEZA KUMPENDA MTU YEYOTE KWA UPENDO WA MUNGU, NI SUALA LA MIMI NA WEWE KUKUBALI UKWELI HUO NA KUANZA KUTEMBEA KATIKA UPENDO (Warumi 5:5, 1Korintho 13:1-10).

4. Maandiko yanasema kiwango chako cha kumjua Mungu kinapimwa na kiwango chako cha upendo: YEYE ASIYEPENDA HAMJUI MUNGU (1Yohana 4:8).

5. Kati ya matunda yapasayo toba unayopaswa kuyazaa na yakawa maishani mwako kila siku ni upendo, tunda mojawapo na lililo kuu alilokupa Roho wa Mungu ni upendo, tembea katika upendo (Wagalatia 5:22).

MAOMBI

1. Muombe Roho Mtakatifu akusaidie kutembea katika upendo maana ni kweli tayari ameshaumimina ndani yako.

2. Muombe Roho Mtakatifu aondoe kila kitu moyoni mwako kinachokuzuia kutembea katika upendo.

3. Muombe Roho Mtakatifu akupe uaminifu katika kumpenda Mungu na kila mtu anayemleta maishani mwako.

Umebarikiwa,

Advertisements

Karibu kwenye Tovuti ya Kikristo... hapa utapata mafunzo Mbali mbali ya kukujenga kiimani ,kifahamu,kimazingira na hata kitabia Karibu Tena

Tagged with: , ,
Posted in Mafunzo

Toa mawazo,maoni

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out / Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out / Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out / Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out / Change )

Connecting to %s

yaliyopita
Habari iliyotazamwa sana
Ungana nasi kwenye kurasa yetu  ya facebook na like page yetu-kuweza kutangaza neno la bwana na utabalikiwa sana..kwa kazi yako kuu kwani thawabu yako mbinguni ni tele

Andika E-mail kwenye box hapo chini kisha Bonyeza (jiunge Hapa)na uweze kujiunga na tovuti hii kupitia e-mail yako utakayojisajilia,tutaweza kukupa kila taarifa,habari zinazojili kwenye hii blog yetu asanteni

Join 2,212 other followers

Upcoming Events

No upcoming events

%d bloggers like this: