MFUNGO WA SIKU 40, (MASAA 12 KUTWA)[SIKU YA 9]

UJUMBE MKUU: ROHO MTAKATIFU NA WEWE.

https://i0.wp.com/allsmilescleft.com/wp-content/uploads/2015/06/woman_praying.jpgSIKU YA TISA: ROHO MTAKATIFU NA AKILI YA KIUNGU.

“Lakini imo roho ndani ya mwanadamu, NA PUMZI ZA MWENYEZI HUWAPA AKILI”
(Ayubu 32:8).

“BWANA akanena na Musa na kumwambia, angalia nimemwita kwa jina lake Bezaleli mwana wa Uri, mwana wa Huri, wa kabila ya Yuda; NAMI NIMEMJAZA ROHO YA MUNGU, KATIKA HEKIMA, NA MAARIFA, NA UJUZI, NA MAMBO YA KAZI YA KILA AINA, ILI ABUNI KAZI ZA USTADI, KUWA FUNDI WA DHAHABU NA FEDHA, NA WA SHABA, NA KUKATA VITO KWA KUTIWA MAHALI, NA KUCHORA MITI, NA KUFANYA KAZI YA USTADI IWAYO YOTE…”
(Kutoka 31:1-5).

“MUNGU AKAMPA Suleimani, hekima, NA AKILI NYINGI SANA, na moyo mkuu, kama mchanga ulioko pwani.”
(1Wafalme 4:29).

MAMBO YA KUJIFUNZA

1. Kuna aina kadhaa za akili;
-Akili za kawaida za kuzaliwa (common sense),
-Akili za darasani (Intellectual literacy),
-Akili za maisha (Accumulated knowledge due to life experience),
-Akili za Kiungu (Divine understanding).

2. Akili za kuzaliwa (common sense) zinakupa matokeo sawa na ya wanadamu wengine wote (common results).

3. Akili ya darasani, ina faida ukiweza kuigeuza maarifa ya maisha, lakini wengi wameishia kufaulu mitihani lakini hawajui cha kufanya mtaani.

4. Akili ya maisha, inaweza kukupa matokeo makubwa mno kuliko akili ya kuzaliwa na akili ya darasani, lakini nayo kuna wakati inafika mwisho, inagonga ukuta; Mfano Petro na ujuzi wake wote wa kuvua samaki, alichemka kupata matokeo usiku kucha, Lakini Yesu mwenyewe akili ya Kiungu alipokuja kwake alimsaidia kupata matokeo hata nje ya kanuni alizozoea (Luka 5:1-11).

5. Hii si akili ambayo kila mtu anayo, ni akili ambayo inaletwa na Upako maalum wa Roho Mtakatifu (Pumzi ya mwenyezi), ili kumfanya mtu afanye vitu ambavyo hakusomea, hakuvipata chuo chochote lakini anavijua automatic kwa sababu ya Roho Mtakatifu (Pumzi ya Mwenyezi) anayempa akili (Ayubu 32:8, Kutoka 31:1-5).

6. Wako wengi waliokuwa na akili hii ya Kiungu kwenye Biblia na ambao waliweka rekodi mbali, mfano Yusufu (Mwanzo 41:38-39), Bezaleli na Oholiabu (Kutoka 31:1-11), Daudi (1Samweli 18:5), Suleimani (1Wafalme 4:29), Wana wa Isakari (1Nyakati 12:32), Ayubu (Ayubu 32:8), Danieli na wenzake watatu (Danieli 1:17) na wengine wengi, NA KATIKA SIKU HIZI ZA MWISHO, MUNGU ANAIACHILIA HII KITU JUU YA WOTE WENYE MWILI, ILI KANISA ZIMA LITEMBEE KATIKA VIWANGO VISIVYOWAHI KUWAKO KAMWE (Yoeli 2:28, Matendo 2:17-18).

7. Roho Mtakatifu uliyenaye ndiye aliye na akili hii ambayo inakupa kufanya mambo ambayo macho hayajawahi kuona, mambo ambayo masikio hayajawahi kuyasikia, mambo ambayo mioyo ya wanadamu wa kawaida haijawahi kufikiri yapo au yanawezekana (1Wakorintho 2:9-13).

MAOMBI

1. Muombe Mungu aliyewagusa watu wengine kwenye Biblia na kuwapa akili zisizokuwa za sayari hii, akuguse na kukupa akili hii ya Kiungu ili umzalie matunda kwa viwango vya juu mno!

2. Muombe Roho Mtakatifu akupe akili ya kuweza kudaka hata mafumbo na mambo ya siri ya Mungu (1Wakorintho 2:9-13).

3. Muombe Mungu akujaze Roho wake kama ilivyokuwa kwa Bezaleli na Oholiabu, ufanye vitu ambavyo hukuvisomea wala hukufundishwa na mtu yeyote ila Roho Mtakatifu (Kutoka 31:1-11).

Umebarikiwa sana,

Advertisements

Karibu kwenye Tovuti ya Kikristo... hapa utapata mafunzo Mbali mbali ya kukujenga kiimani ,kifahamu,kimazingira na hata kitabia Karibu Tena

Tagged with: , , ,
Posted in Mafunzo

Toa mawazo,maoni

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out / Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out / Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out / Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out / Change )

Connecting to %s

yaliyopita
Habari iliyotazamwa sana
Ungana nasi kwenye kurasa yetu  ya facebook na like page yetu-kuweza kutangaza neno la bwana na utabalikiwa sana..kwa kazi yako kuu kwani thawabu yako mbinguni ni tele

Andika E-mail kwenye box hapo chini kisha Bonyeza (jiunge Hapa)na uweze kujiunga na tovuti hii kupitia e-mail yako utakayojisajilia,tutaweza kukupa kila taarifa,habari zinazojili kwenye hii blog yetu asanteni

Join 2,212 other followers

Upcoming Events

No upcoming events

%d bloggers like this: