UNAPOANZA MWEZI WA SITA WA 2017.

 

MAMBO YA KUFANYA;

1. Kaa chini andika malengo yako ya mwezi mzima.

i)Malengo ya kiroho

*Utaomba mara ngapi kwa siku?
Na kila round ya maombi, utaomba dakika ngapi au masaa mangapi?
Utaombea nini kwa kila round ya maombi kwa siku?
KAA CHINI JIBU MASWALI HAYA NA KUANDIKA KWENYE NOTEBOOK AU DAFTARI!

ii) Utafunga mara ngapi kwa kila wiki ya mwezi June?
Masaa 12 mara ngapi na masaa 24 mara ngapi?
ANDIKA CHINI KWENYE NOTE BOOK

iii) Utaangalia videos ngapi za mafundisho kwa kila siku moja ya June?
Kwa wiki utaangalia videos ngapi?
Utakazana kuangalia videos za topic gani?
-Utakatifu
-Imani
-Uongozi
-Huduma
-Mahusiano na ndoa
-Fedha na Mafanikio ya Kibiblia
-Maono na kusudi
-Malezi ya Kibiblia
– Roho Mtakatifu (karama na huduma zake)
LAZIMA UANDIKE HAYA YOTE CHINI KWENYE NOTE BOOK ILI UANZE KUYAKIMBIZA KAMA MALENGO YAKO YA JUNE!

iv) Utasoma vitabu vingapi?
*Kwa siku sura ngapi?
*Kwa wiki vitabu vingapi?
*Kwa mwezi vitabu vingapi?
*Utasoma vitabu vya topic zipi?
*Utasoma vitabu vya mwandishi gani?
*Utanunua au kudownload vitabu vingapi June?
VITABU SI OMBI KWA MTU ANAYETAKA KUACHA ALAMA.
Daniel 9:2, Isaya 33:6.

v) Biblia
*Utasoma sura ngapi kwa siku?
*Utasoma sura ngapi kwa wiki?
*Utasoma sura ngapi kwa Mwezi?
HAKIKISHA UNAANDIKA SUMMARY YA KILA SURA ULIYOSOMA;
Umejifunza nini?
Umepata ufunuo gani?
Maandiko gani ya kuweka moyoni (kuyashika)?

vi) Zaka na Matoleo (sadaka)!
*Toa zaka kamili na kwa wakati
*Ni vema ujizoeze kupandisha kiwango chako cha sadaka kila mwezi.

-Sadaka za kawaida (hiari)
-Sadaka za wahitaji
-Sadaka za Injili (kusapoti kazi ya Mungu)
-Sadaka za shukurani
Nakadhalika.

2. Malengo ya Kiuchumi

i) Kipato
*Utaingiza pesa kwa njia gani (nini chanzo chako cha fedha)?
*Je unaweza kuviongeza mwezi huu wa June?
*Unauza huduma au bidhaa gani?
*Akina nani ni wateja wako?
*Akina nani ni washindani wako?
*Upi ni ubora na upi ni udhaifu wa bidhaa au huduma yako?
Unautatuaje udhaifu na kuimarisha ubora wako?
*Unawafikiaje wateja wako (watumiaji na wanunuzi wa bidhaa zako)?
*Unawatunzaje na kuboresha mahusiano yako na wateja wako?
*Unadhani kipi utafanya mwezi huu kikupe matokeo tofauti na ya May?

Matumizi
*Unatumiaje pesa unayoingiza, kwa siku, wiki na mwezi?
*Unadhani utumiaji wako wa pesa utaifanya iongezeke au itakufanya ukopekope na kuomba omba?
*Umegawanya pesa yako kwenye mafungu kabla ya matumizi?;
-Zaka na sadaka
-Uwekezaji
-Matumizi ya lazima
-Dharura
Kama umetenga hivi je umegawa asilimia ngapi kwa kila kundi?
ANDIKA HAYA SI YA KUSOMA TU.
“Ili uwe bwana juu ya pesa, lazima ujue hata shilingi yako ya mwisho inaingiaje na kutumikaje… Ni yupi kati yenu anayepoteza shilingi yake moja asiyepekua na kutafuta kwa taa mpaka aipate?”
UKIHESHIMU NA KUTUNZA TAKWIMU ZA KILA SHILINGI INAYOPITA MIKONONI MWAKO, MUDA SI MREFU UTAKUWA BWANA JUU YA PESA!
JIFUNZE NA LAZIMISHA KUANDIKA!
*Andika mapato na matumizi ya kila shilingi yako (MPE NA MTOE)!

3. Malengo ya Kifamilia (mahusiano)
*Utakuwa na muda kiasi gani kwa siku na mme/mkeo?
*Utaomba na kusoma naye Neno mara kila siku (ibada ya pamoja)?
*Utakaa muda gani na watoto wako kila siku, wiki na mara ngapi kwa mwezi?
USIJISAHAU, MSINGI MKUBWA WA MAFANIKIO NI MAHUSIANO.
Mahusiano mazuri na Mungu (kiroho), na mahusiano mazuri na watu wako!
USIWE MJINGA TAFUTA MUDA WA FAMILIA YAKO.

TUMIA SIKU HII YA LEO, KUWAZA, KUTAFAKARI, KUJIBU MASWALI NILIYOKUULIZA, NA KUNUNUA NOTEBOOK KUANDIKA MALENGO YANAYOELEWEKA!

Maandiko:

“Je ni yupi kati yenu atakaye kujenga mnara asiyekaa kwanza chini na kuhesabu gharama (kupanga mipango, malengo na mikakati) kwamba atamaliza au la? Ili asije kuishia njiani, watu wakamcheka…”
(Luka 14:28-30).

“Au kuna mfalme gani, akitaka kwenda kupigana na Mfalme mwingine, asiyeketi kwanza na kufanya shauri (kupanga mikakati na mbinu), kwamba yeye pamoja na askari elfu kumi ataweza kukutana na yule anayekuja juu yake na askari elfu ishirini?…”
(Luka14:31-32).

“Maandalio ya moyo (kupanga mipango) ni ya mwanadamu, bali jawabu la ulimi hutoka kwa Bwana”
(Mithali 16:1).

“Moyo wa mtu huzifikiria njia zake (hukaa chini na kupanga) bali Bwana huziongoza hatua zake”
(Mithali 16:9).

“Umkabidhi Bwana njia yako (mipango yako), Pia umtumaini (umwamini), naye atafanya (atavifanya vitimie)”
(Zaburi 37:5).

Kuweka malengo, kupanga na kuandika ni wajibu wako.
Halafu viombee na kujiwekea nidhamu kuvifanya, baada ya muda mkono wa Mungu utavifanya vitimie (Ayubu 22:28)!

Siku njema na mwezi mwema!

Mwalimu Dickson Cornel Kabigumila,
Destined To Reign International Ministries,
ABC CHURCH GLOBAL.

Advertisements

Karibu kwenye Tovuti ya Kikristo... hapa utapata mafunzo Mbali mbali ya kukujenga kiimani ,kifahamu,kimazingira na hata kitabia Karibu Tena

Posted in Mafunzo
One comment on “UNAPOANZA MWEZI WA SITA WA 2017.
  1. Mikali says:

    Najifunza sana..ubarikiwe mtumishi

Toa mawazo,maoni

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out / Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out / Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out / Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out / Change )

Connecting to %s

yaliyopita
Ungana nasi kwenye kurasa yetu  ya facebook na like page yetu-kuweza kutangaza neno la bwana na utabalikiwa sana..kwa kazi yako kuu kwani thawabu yako mbinguni ni tele

Andika E-mail kwenye box hapo chini kisha Bonyeza (jiunge Hapa)na uweze kujiunga na tovuti hii kupitia e-mail yako utakayojisajilia,tutaweza kukupa kila taarifa,habari zinazojili kwenye hii blog yetu asanteni

Join 2,215 other followers

Upcoming Events

No upcoming events

%d bloggers like this: