Uvivuni Kipaji

HII ITAKUSAIDIA SANA;

Ukitaka kujua sifa ya mvivu, UKAMWONE anavyoamka kitandani,
Atakwambia uuuh, mgongo unauma, kiuno kinauma, mikono haina nguvu, halafu anahisi njaa saa 12:00 asbh,

Mithali 19 :15 Uvivu humtia mtu katika usingizi mzito; Na nafsi yake mvivu itaona njaa.

ANGALIA HII PIA

Mithali 24 :30 Nalipita karibu na shamba la mvivu, Na shamba la mizabibu la mtu asiye na akili.
[Jamaa anazungumzia aina mbili ya mashamba, 1. Shamba la mvivu, 2. Shamba la mtu asiye na akili – hawa watu nao ni ndugu]

31 Kumbe! Lote pia limemea miiba; Uso wake ulifunikwa kwa viwawi; Na ukuta wake wa mawe umebomoka.

32 Ndipo nilipoangalia na kufikiri sana; Naliona, nikapata mafundisho. [HUYU JAMAA ALIPOLIONA SHAMBA LA MVIVU,NA SHAMBA LA MTU ASIYE NA AKILI AKAPATA MAJIBU, MSTARI WA 33]

33 Bado kulala kidogo, kusinzia kidogo, Bado kukunja mikono upate usingizi!

Jamaa aligundua kuwa tatizo la mtu mvivu na mtu asiye na akili ni hilo kwenye mstari wa 33

34 Hivyo, umaskini wako huja kama mnyang’anyi, Na uhitaji wako kama mtu mwenye silaha.

[Yaan biblia iko wazi kuwa umasikini wa mvivu unakuja kama mnyang’anyi na uhitaji wake kama mtu mwenye silaha]

uvivu na umasikini ni mapacha wasiofanana ila, wanafanya birthday siku moja.

Check na hii,
Hahaha

Mithali 26 :14 Kama vile mlango ugeukavyo katika bawaba zake; Kadhalika mtu mvivu katika kitanda chake.

15 Mtu mvivu hutia mkono wake sahanini; Kwamchosha kuupeleka tena kinywani pake.

Biblia inasema mvivu ni kama bawaba ya mlango,
Akiamka anageuka upande huu ANAENDELEA KULALA, akiamka tena anageuka upande mwingine ANAENDELEA KULALA.

Sasa ndio utajua
Kama una visifa vinafanana na hivi, basi ujue uhitaji wako utakuja kama mtu mwenye silaha,

Uvivu ni roho unayoweza kuithibiti kabisa kabisa, ukiona inakusumbua uombewe ufunguliwe maana itakufanya kuwa maskini.

Uvivu ni tabia ya mwili,
Na ikijaa sana, unaona mpaka na akili zinakuwa na uvivu hata wa kufikiri,

Na ikiendelea sana itakufanya hata na mbinguni usiingie aisee!
Usiusikie mwili, hata kama unauma,

You need to make an aggressive decisions to overcome laziness.

Kisa kakosa kazi, basi analala mpaka saa 6 mchana, duuh
Sasa ukitoka hapo, unasema una pepo la kukataliwa,

Pepo la kukataliwa ni pepo linalofanya kazi ndani ya wavivu.

Niishie hapa

God bless you
Ibrahim Amasi

Advertisements

Karibu kwenye Tovuti ya Kikristo... hapa utapata mafunzo Mbali mbali ya kukujenga kiimani ,kifahamu,kimazingira na hata kitabia Karibu Tena

Tagged with: , ,
Posted in Mafunzo
One comment on “Uvivuni Kipaji

Toa mawazo,maoni

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out / Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out / Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out / Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out / Change )

Connecting to %s

yaliyopita
Ungana nasi kwenye kurasa yetu  ya facebook na like page yetu-kuweza kutangaza neno la bwana na utabalikiwa sana..kwa kazi yako kuu kwani thawabu yako mbinguni ni tele

Andika E-mail kwenye box hapo chini kisha Bonyeza (jiunge Hapa)na uweze kujiunga na tovuti hii kupitia e-mail yako utakayojisajilia,tutaweza kukupa kila taarifa,habari zinazojili kwenye hii blog yetu asanteni

Join 2,215 other followers

Upcoming Events

No upcoming events

%d bloggers like this: