​RAFIKI NATAKA UFANIKIWE, TENDEA KAZI HIZI SIRI:

Kwenye Maisha Ili Ufanikiwe Katika Jambo Lolote Lazima;
1.ULIJUE JAMBO HUSIKA KWA UNDANI (TAFUTA KUJUA KUHUSU HILO/ KUWA NA MAARIFA YA KUTOSHA KUHUSU HILO).

Yaani, “TAFUTA NAWE UTAONA” (Mathayo 7:7).

Zingatia Hili; “WASIO NA MAARIFA [WASIO NA TAARIFA SAHIHI] WANAANGAMIZWA” (Hosea 4:6).
2.UJUE NJIA/ NAMNA YA KULIPATA AU KULIFIKIA 

Yesu Aliwaambia Wanafunzi Wake, “NAMI NIENDAKO MWAIJUA NJIA” (Yohana 14:4).

Hawa Wanafunzi Wake Waliijua Njia Ila Hawakujua Kuwa Wanaijua, Ndipo Akawafafanulia “MIMI [YESU] NDIMI NJIA… KWELI NA UZIMA… MTU HAJI KWA BABA YANGU ISIPOKUWA KWA NJIA YA MIMI” (Yohana 14:6).

Zingatia Hili: “SI KILA NJIA UNAYOIONA MBELE YAKO NI NJIA SAHIHI HATA KAMA WATU WOTE AU WATU WENGI WANAITUMIA”

Biblia Inasema, “IKO NJIA IONEKANAYO KUWA SAWA MACHONI PA MTU; LAKINI MWISHO WAKE NI NJIA ZA MAUTI [KIFO NA UHARIBIFU]” (Mithali 16:25).

Ongeza Umakini Kwenye NJIA YAKO UNAYOITUMIA KUFIKA UNAKOENDA, HAKIKISHA MWISHO WAKE USIWE KIFO NA UANGAMIVU WAKO… MARA NYINGI “MTEGO UFUNIKWA KWA MAJANI MAZURI ILI ATAKAYEVUTIWA NAO AKANYAGE NA KUTUMBUKIA NA KUANGAMIA”
3.KUJUA NJIA HAITOSHI; CHUKUA HATUA YA KUTEMBEA KWENYE NJIA SAHIHI ULIYOIJUA

Kuna Watu Wamejaza “THEORIES” Na “FORMULAS” Za Kufanya Mambo Au Kufikia Mambo Kwenye Maisha Lakini “HAWANA UTHUBUTU” Wa “KUCHUKUA HATUA YA KUTEMBEA KWENYE HIZO KANUNI NA NJIA WANAZOZIJUA KICHWANI NA KUIMBA MDOMONI”

Kumbuka Hili, “MAARIFA, MBINU NA SIRI ZA MAISHA ZISIZOTENDEWA KAZI HAZIWEZI KUGEUZA MAISHA YA ALIYE NAZO”

Kila Mwaka WASOMI WANAHITIM NA DIPLOMA, DEGREE, MASTERS, PHD LAKINI “HAWAJUI NAMNA YA KUTEMBEA KWENYE HIZO NJIA [ELIMU] WALIZOPATA DARASANI, WANAISHIA KUWA MIZIGO KWA TAIFA”

Yesu Alisema, “NJIA IMESONGWA NAO WAIPITIAO NI WACHACHE” (Mathayo 7:13-14).

Siku Zote “MLANGO WA UTAJIRI, MAFANIKIO NA USTAWI NI MWEMBAMBA MNO, NA PIA UMESONGWA” Na Ndio Maana “WATU WACHACHE SANA WANAWEZA KUUONA” Lakini Pia Ni “WATU WACHACHE SANA ZAIDI WENYE UTHUBUTU KUUPITIA TENA KWA KUTUMIA NJIA HALALI NA KWA HAKI”

Ndiyo Maana Idadi Ya Wanaopita Kwenye Mlango Wa “UMASIKINI, KUSHINDWA, UHITAJI, UHABA NA UCHACHE” Ni Wengi Sana Maana “NJIA HII NI PANA NA HAIJASONGWA, NA NI RAHISI SANA KUIPITIA”
4.KUWA NA UTHUBUTU [UTAYARI] WA KUPITA KWENYE NJIA SAHIHI HAITOSHI; LAZIMA UJUE NAMNA YA KUPIGA HATUA KWENYE NJIA, LAZIMA UWE NA MWONGOZA HATUA KATIKA NJIA
Biblia Inasema, “MOYO WA MTU HUIFIKIRI NJIA YAKE [MIPANGO] BALI BWANA HUZIONGOZA HATUA ZAKE” (Mithali 16:9) 

Kwa Mtaji Huu Ni Dhahiri Kuwa “KUAMUA KUTEMBEA KWENYE NJIA HAITOSHI” Lazima Na Wewe “UWE NA UHUSIANO NA USHIRIKA WA KINA NA MWONGOZA HATUA ILI AKUSAIDIE UJUE NAMNA YA KUINGIA NA KUTOKA [HEKIMA] ILI USIJE KUCHELEWA AU KUKANYAGA PASIPOKUWA SAWA”

Na Hapa Ndipo Waliposhindwa Wengi, “WANATUMIA MUDA MWINGI KUANGALIA NJIA BADALA YA KUTUMIA MUDA WAO MWINGI NA ATAKAYEWAONGOZA HATUA KWA HATUA KWENYE NJIA”

Lazima Uchukue Maamuzi Ya Lazima Na Ya Dhati Kuwa “RAFIKI WA MUNGU [MWONGOZA HATUA KATIKA NJIA]” Ambaye “NENO LAKE NI TAA YA MIGUU YAKO [ILI UKANYAGE MAHALI SAWA] NA PIA NI MWANGA WA NJIA YAKO [NENO LA MUNGU NDILO LILILOJAA MAELEKEZO YA NAMNA YA KUITUMIA NJIA YAKO YA MAFANIKIO]” (Zaburi 119:105).

ILI KUWA RAFIKI WA MUNGU [MWONGOZA NJIA] LAZIMA UFANYE YAFUATAYO:
a) Lazima Uyatoe Maisha Yako Kwake [Lazima UOKOKE]- Warumi 10:9-10
b)Baada Ya Kuokoka Lazima UKUBALI KUISHI SAWA NA NENO LA MUNGU TU Hivyo Lazima ULISOME KWA BIDII, ULITENDE KILA SIKU KAMA MFUMO WAKO WA MAISHA MAPYA NDANI YA KRISTO YESU.

Wakolosai 3:17, Zaburi 119:9-11,105.
c)Lazima Udumu Kwenye Mafundisho Sahihi Yanayoilisha Imani Yako Na Kukutenga Na Mifumo Mibovu Ya Dunia Hii; “KUWA RAFIKI WA DUNIA NI KUWA ADUI WA MUNGU” (Yakobo 4:4).
d)Lazima Upate Muda Wa Kumwomba Mungu Na Kumshirikisha Mambo Yako Na Njia Zako Ili Aweze Kukufanikisha Na Kukusaidia Kupiga Hatua Sahihi Za Ushindi. LAZIMA UOMBE; ASUBUHI OMBA, MCHANA OMBA, JIONI OMBA, USIKU OMBA… OMBA BILA KUKOMA… OMBA SIKU ZOTE WALA USIKATE TAMAA…. Kwenye Kuomba, Unamkabidhi Mungu Mambo Yako Ili Akusaidie; USIPOOMBA UNAJIMALIZA!

“UMKABIDHI BWANA NJIA YAKO [KUPITIA MAOMBI], PIA UMTUMAINI [SHIKILIA RIPOTI YA NENO LILIVYOSEMA BILA KUANGALIA MAZINGIRA] NAYE BWANA ATAFANYA” (Zaburi 37:5).
e)Achana Na Marafiki Wanaokupeleka Kwenye Dhambi Na Maovu (Zaburi 1:1-3, 1Kor 15:33).
Haya Ndo Maisha; Nenda Ukafanikiwe Sasa Kama Ukiyatendea Kazi, 

Usipoyetendea Kazi, Kushindwa Hakukwepeki!

Mwalimu Dickson Cornel Kabigumila

Novemba 29, 2013.

Advertisements

Karibu kwenye Tovuti ya Kikristo... hapa utapata mafunzo Mbali mbali ya kukujenga kiimani ,kifahamu,kimazingira na hata kitabia Karibu Tena

Tagged with: , ,
Posted in Mafunzo

Toa mawazo,maoni

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out / Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out / Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out / Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out / Change )

Connecting to %s

yaliyopita
Ungana nasi kwenye kurasa yetu  ya facebook na like page yetu-kuweza kutangaza neno la bwana na utabalikiwa sana..kwa kazi yako kuu kwani thawabu yako mbinguni ni tele

Andika E-mail kwenye box hapo chini kisha Bonyeza (jiunge Hapa)na uweze kujiunga na tovuti hii kupitia e-mail yako utakayojisajilia,tutaweza kukupa kila taarifa,habari zinazojili kwenye hii blog yetu asanteni

Join 2,217 other followers

Upcoming Events

No upcoming events

%d bloggers like this: